WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Friday, July 22, 2016

JE YATUPASA KULIPIZA KISASI DHIDI YA WENZETU KATIKA MAISHA YETU;


July 22

Warumi 3:10

Tafakari ya leo Kwa hakika mwanandamu anahitaji upeo mkubwa wa nuru ya kiroho ambayo itaweza kumfanya azike tamaa zake na hisia zote za kulipiza kisasi; tunatakiwa kuwa na uwezo wa kujizuia na hasira, kuzikandamiza hasira, chuki kwa moyo mpana na kujenga daraja la msamaha.  Kusamehe mtu ambaye amekukosea, kuwapenda ndugu na jamaa ambao wameukata uhusiano pamoja nawe, na kuwa mkarimu kwa yule ambaye aliwahi kukunyima, kukutukana, kukusababishia hasira,kukudharau, kukudhalilisha na kadhalika sio jambo rahisi. Tumewaona hata watumishi wa Mungu ambao wanaielewa sana bibilia wakishindwa kabisa kuktekeleza kanuni hii.

Tafakari yetu inatukumbusha umuhimu wa kumsamehe yule aliyekutendea yasiyo sahihi hutusaidia kutupatanisha na Muumba wetu; vile vile msamaha hudumisha mshikamano wa udugu ambao umeharibiwa. Kwa kusamehe tunaandaa njia ya kumwendea Mungu; Lakini  pasipo  imani  haiwezekani  (Waebrania 11:6). Inatufundisha kuwa mtu  amwendeaye Mungu  lazima  aamini  kwamba  yeye  yuko,  na  kwamba  huwapa  thawabu wale wamtafutao,”. Msamaha hutujengea wa kumwendea na Kuishi na Mungu katika Imani.

Kama ilivyoandikwa hakuna mwenye haki, hata mmoja” (Warumi 3:10). Mungu yuko tayari na anasubiri kumsamehe mtu anaye omba msamaha imeelezwa katika Zaburi 86:5 "Kama wewe Bwana u mwema, umekuwa tayari kusamehe, na mwingi wa fadhili kwa watu wote wakuitao". Daudi aliweka wapi tumaini lake la msamaha? Tukisoma Zaburi 51:1 "Ee Mungu unirehemu sawasawa na fadhili zako kiasi cha wingi wa rehema zako uyafute makosa yangu. Mathayo 6:14-15 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao na Baba wenu wa mbinguni atawasamehe ninyi bali msipowasamehe watu makosa yao wala Baba yenu hatawasamehe makosa yenu." Wale wamesamehewa husamehe. imeandikwa Waefeso 4:32 "Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma ninyi mkasameheane kama na Mungu katika kristo alivyowasamehe ninyi."

Tafakari inasisitiza neno kusamehe kwa kweli hakuhesabu makosa. imeandikwa Mathayo 18:21-22 "Kisha petero akamwendea akamwambia Bwana ndugu yangu anikose mara ngapi nami ni msamehe? hata mara saba? Yesu akamwambia sikwambii mara saba bali hata saba mara sabini." Katika kusamehe Yesu ametukomboa kutoka kwa dhambi na mshahara wa dhambi. Wakolosai 2:13-14 inatueleza kuwa "Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu aliwafanya hai pamoja naye akisha kutusamehe makosa yote akisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake iliyo kuwa na uwadui kwetu akiondoa isiwepo tena akaigongomea msalabani."
Zaburi 51:7-12 "Unisamehe nami nitakuwa safi, unioshe nami nitakuwa mweupe kuliko dheluji unifanye kusikia furaha na shangwe, mifupa ilio ponda ifurahi. usitiri uso wako usitazame dhambi zangu uzifute hatia zangu zote Ee Mungu uniumbie moyo safi uifanye upya roho iliyo tulia ndani yangu usinitenge na uso wako wala roho wako mtakatifu usiniondolee unirudishie furaha ya wakovu wako unitegemeze kwa roho ya wepesi."
Zaburi 32:1-6 "Heri aliyesamehewa dhambi na kusitiriwa makosa yake heri Bwana asiyemhesabia upotovu, ambaye rohoni mwake hamna hila niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa kwa kuugua kwangu mchana kutwa na kwa maana mchana na usiku mkono wako ulinilemea jasho langu likakauka hata nikawa kama nchi kavu wakati wa kaskazi nalikujulisha dhambi yangu wala sikuuficha upotovu wangu nalisema nitayari maasi yangu kwa Bwana naweukanisamehe uoptovu wa dhambi yangu kwa hiyo kila mtu mtauwa akuombe wakati unapopatikana hakika maji makuu yafurikapo hayatamfikia yeye."
Tafakari yetu inaonyesha umuhimu wa kuwa mnyonge wa moyo wako mbele ya Mungu na wala kutambua hatia yangu, haijafika hali ya kwanza ya kukubalika. Tunahitaji kuokolewa kutoka katika aina zote za tabia zetu mbaya pamoja na misukumo ya ndani inayotushurutisha kufanya mambo fulani mabaya: kama vile, kusema uongo, hasira inayomfanya mtu atukane watu, tamaa mbaya za mwili, uchungu, kutaja machache tu.
Hatuwezi kujiokoa wenyewe kutoka katika dhambi au kuigeuza tabia yetu kwa kujitegemea wenyewe kama vile Simba asivyoweza kuamua awe mwana-kondoo (Warumi 7:18). Dhambi ina nguvu nyingi kuliko nia yetu ya kufanya yale tuyatakayo. Lakini Kristo anaweza kukufanya wewe uwe "imara kwa uweza wake, kwa kazi ya Roho wake katika utu [wako] wa ndani" (Waefeso 3:16). Anafanya kazi yake ili kuondoa tabia zetu ziletazo uharibifu na mahali pake kuweka tabia hizi nzuri: upendo, amani, furaha, upole, uwezo wa kujitawala (Wagalatia 5:22,23). Kristo anaishi maisha yake kupitia ndani yetu, kisha tunapokea uponyaji wa kiroho, tunarejeshwa katika maisha mapya, na kuwezeshwa kuishi maisha hayo mapya.
Ni jambo la muhimu sana kujua kuwa hakuna dhambi ambayo ni ya kutisha sana asiyoweza kuisameka Yesu anatamani sana kwamba kila mmoja wetu hatimayeawe na uhusiano mzuri na Yule aliyemkosea na kumsababishia majeraha ambayo yamejenga chuki ambayo inahitaji msamaha. Yesu anataka tupokea msamaha na utakaso wa Mungu ni; katika  imani jambo ni  rahisi na la maana sana kama tunavyofurahia kumpokea motto mdogo aliyezaliwa na kumkumbatia. Lakini kutokana na ubinadamu wetu, majivuno, kiburi, masengenyo inatuwia vigumu sana kutoa msamaha wa kweli pale tunapokosewa, tunakuwa na kiburi ambacho kinatufanya kuona kuwa Yule aliyetukosea hastaili msamaha wetu; lakini kama tunayafuata mafundisho ya yesu na mifano ambayo ametutolea katika Bibilia Takatitifu tunatakiwa tuondoe ugumu katika mioyo yetu na kuuvaa unyenyekevu kama yeye alivyovaa unyenyekevu na kuuvua Umungu kwa ajili ya makosa yetu, na alikuja kukaa nasi na ametutengenezea daraja la msamaha ambalo kila mwanadamu lazima alipite ili kuweza kukamilisha safari yake ya kwenda mbingu.
Hii ndio tafakari yetu ya leo hebu jitafakari kwa nini umekuwa na kiburi cha kushindwa kabisa kumsamehe, jirani yako, ndugu yako ambao wamekukosea kutokana na ubinadamu wao, usijali amekukosea mara ngapi angalia je wewe uko tayari kumsamehe wakati wowote ule na mara ngapi?- amina
Emmanuel Turuka



Thursday, July 21, 2016

UFALME WA MUNGU UKO NDANI YAKO


July 21

Luka 17:20-21

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa ufalme wa Mungu uko ndani yako; mafarisaya walimuuliza Yesu je ufalme wa Mungu utakuja lini? Yesu aliwajibu kuwa ufalme wa Mungu hauji kwa kuangalia vitu na matukio yanayoonekana isopokuwa ufalme wa Mungu uko ndani yenu; hata pale Philipo alipomwuliza yesu awaonyeshe baba nasi tutaridhika; Yesu alimjibu kuwa nimekuwa nanyi muda huu wote na bado hamjemjua baba? Yeyote aliyeniona mimi amemwona Baba; mimi niko ndani ya baba na baba ndani yangu; na yeyote anayeamini katika neno langu ameamini kwa baba aliyenituma;

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa jukumu letu inatakiwa tujiangalie zaidi undani wa matendo yetu na  sio matendo yetu au mwonekano wetu wan je katika maisha ya kumtumikia Mungu; Mwonekano wetu wa nje unalinganishwa na jinsi tunavyojiangalia katika kioo na kujiona kitaswira tuko vipi na daima tunachukua muda wa kujirekebisha ili tuweze kuonekana watanashati. Ni jambo nzuri hivyo kama tukiweza kuchukua juhudi hizo katika taathimini ya ndani itakuwa jambo nzuri sana; ni wazi kuwa katika mazingira ya maisha yetu leo hii; maisha yetu yametawaliwa na utitili wa mambo; maisha yetu yamekabiliwa na majukumu yetu ya kila siku, kazi ambazo lazima tuzimalize kwa wakati, mahitaji ambayo tunayaona ya lazima; na tama zetu za kila siku mabazo tunatamani kuzikamilisha; ni wazi kabisa na rahisi kabisa kama binadamu kupoteza mwelekeo katika utitili huu wa maisha; Luka 15:17  ni kama mtu ambaye ameshituka kutoka katika ndoto mbaya na kutisha pamoja na kutokwa na jasho lakini itamchukua muda ili akili yake iweze kurudi tena;

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa  katika khali ya kupotea inapelekea mambo mawili  ulinzi wa uwongo ambao unakudhoofisha wewe mwenyewe; hatimaye unajipoteza mwenyewe kuna mambo mawili yatajitokeza mosi ni kujijua aina ya mtu uliyezoea kuwa na pili  na unajipoteza kabisa  katika uhalisia wako.  Je unakumbuka hadithi ya mwana mpotevu  alifika mahali akajitambua yeye mwenyewe kuwa amepotea; tabu zote ambazo alizipata ni matokeo ya tama ambazo alifikiri kuwa atapata maendeleo makubwa katika maisha yake matokeo yake kuwa aliishia kupotea na kurudi nyuma kimaendeleo na kimaisha. Utambuzi wa kwanza ambao humjia mtu mabaye amepotea anapojitambua kuwa alikuwa amepotea ni khali ya kujijutia kwa namna gani alianguka na kushinda kufika pale alipokuwa amekusudia kufika, ananza kujenga woga  kwa nini amefanya hivyo alivofanya. Je unakumbuka Samsoni alipoamka na kujikuta mikononi mwa maadui na sio mikononi mwa Mungu? Au unamkumbuka Yona alivyotapikwa na samaki ukingoni mwa pwani; ndio maana lazima tukubali kuwa kitu kikubwa hapa duniani sio wapi tunaposimama bali ni katika mwelekeo gani tunakwenda: na tutafurahi zaidi pale tukapofika mwisho wa safari yetu katika utukufu wa Mbinguni;

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa kitu kikubwa na cha msingi sana katika maisha yetu ni  kuwa na furaha ambayo inatupa sisi nafasi ya kutenda; furaha ambayo inatupa sisi kitu cha kutumaini na ikumbukwe kuwa mtu yeyyote anaweza kupata furaha hasa pale ambap anapata kamba ya wokovu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ya kumvusha. Tukumbuke jinsi Samsoni pamoja na kuwa kipofu baada ya kutekwa na maadui kwa sababu ya Delila lakini kwa kumtumaini na kujuta makosa yake Mungu alimrejeshea nguvu zake kwa dhumuni hasa la kuwaangamiza wafipipi ambao walikuwa wamemeteka na kumtesa. Yona pamoja kuwa alikuwa gizani kwenye tumbo la samaki kwa vile aligundua kosa lake wokovu wa Mungu na mwanga wa wokovu ulimrudia kwa mara ya pili na kuanza kuhubiri.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa mtu lazima aishi kwa malengo na madhumuni na kama lengo au dhumuni likipotea basi  maisha yake yanakuwa hayaeleweki ndipo tunapohitaji msaada wa Mungu katika kufanikisha dhumuni la maisha yetu. Pale ambapo tunashindwa kujitambua unakuwa umepotea kiroho, macho yako yanakuwa yamefungwa masikio yako yanakuwa yamezibwa, na ni Mungu pekee yake ambaye anaweza kuleta muujiza katika wakati kama huu. Ni wkati ambapo neema ya Mungu inahitajika. Tumkumbuke Daudi alipopotelea katika dhambi lakini ujio wa Mungu Katika maisha yake uliweza kumrudishia furaha na amani. Amani ya kweli upendo wa kweli na maisha ya neema ya kweli hayawezekani bila uwepo wa Mungu. Mungu ni kila kitu kwetu na katika maisha yetu ya kweli.
Ni ujumbe mzito ambao unahitaji utambuzi wa kweli. Hii ndio tafakari yetu ya leo. Amina

Emmanuel Turuka




Sunday, July 17, 2016

NANI WA KUABUDIWA;

July

Tafakari ya leo tuendelee kukumbuka kuwa Mungu ndiye tumaini letu na yeye ndiye tunayemwabudu na kumkimbilia katika furaha na shida zetu.

Saturday, July 16, 2016

WEWE NI MUNGU

July
Tafakari yetu leo tutafakari wimbo huu ukuu wa Mungu katika maisha yetu;

Thursday, July 14, 2016

KWA NINI UNAMWOGOPA MTU MWINGINE?



July 14

Tafakari ya leo tunaangalia tatizo la kumwogopa mtu mwingine katika maisha yetu kama wakristo; kama wewe ni mfuasi wa Yesu basi hutakiwi kumwogopa mtu mwingine yeyote ambaye hawezi kuua roho; kama katika maisha yako utakuwa unafanya maamuzi yako kwa kumwogopa mtu au watu wengine basi wewe unatatizo kubwa sana la kiimani. Kama tabia hiyo ikikutokea basi unatakiwa kucha kuwaangalia watu wengine katika kutimiza mahitaji yako; bali tunatakiwa tumtazame Mungu ndiye pekee mtoaji wa mahitaji yetu; kwa kufanya hivyo utajisikia vizuri mwenyewe bila kufuata maoni ya wengine.

Tafakari yetu leo inatukumbusha ili kujiridhisha katika maamuzi yako jambo la kwanza unatakiwa ujiulize kuwa wewe ni nani? Na ukumbuke kuwa wewe umepewa na mwenyezi Mungu neema ya kupendwa na yeye; tulivyoumbwa tuliumbwa watupu na Mungu kwa mapendo yake ametujaza na Baraka ya upendo. Kama wewe umejazwa na upendo wa Mungu kwa nini sasa unakubali kutawaliwa na watu wengine katika mawazo yako? Binadamu mwingine yeyote yule hana nguvu ya kutawala akili yako isipokuwa Mungu tu. Ndio maana Yesu alivyosema kuwa unapojiona kuwa unatabia ya aina hiyo yeye ana njia ya kutokea; basi tunatakiwa kumruhusu Yesu kujaza sisi na upendo wake ambao hauna mipaka lakini kama tutakuwa tayari kutekeleza mipango ya Mungu na sio mipango ya binadamu tunatakiwa kuwa tayari katika kutimiza utukufu wa mungu na sio matamanio yetu. Ili tuweze kujihakikishia kuwa tuko imara na hatumwogopi mtu yeyote lazima maisha yetu tuyaweke chini ya msingi wa uangalizi wa Yesu hapo hatutakuwa na sababu ya kumwogopa mtu yeyote na tutajihakikishia furaha ya kweli;

Tafakari yetu inatuonya kuwa hatutakiwi kabisa kutawaliwa na mawazo, woga ; mwonekano dhidi ya watu wengine kuwa watasemaje ; najua mara nyingi tatizo linakuwa pale wanapotaka kunufaika na kile ambacho wao wanancho na pengine mimi au wewe huna au sina na unatamani upate huko ukifikiri kuwa Mwenyezi Mungu hawezi kukupa wewe hiyo Baraka. Tunapo mwamini na kumtumaini mungu yeye Baraka zake anazitoa kwa namna ya ajabu na pekee kabisa. Hivyo hata pale tunaposoma bibilia katika msingi huu ndipo tunapoona jinsi gani tunavyowaogopa binadamu wengine. Tuangalie mifano kutoka Mwanzo 12:10-20 au Mwanzo 20: I-2 AU Hesabu 14:11 DEUt 1:17 Zaburi 56:3-4 Matahayo 10:28 1 petro 3:14

Lazima tutambue kuwa woga wa kweli wa kumwogopa Mungu ni kupitia maungamo; Mathayo 22:16 kwa kuungama dhambi zetu Mungu kupitia bwana wetu Yesu Krsito anaondoa woga kabisa; tunatakuwa kujitathimini wenyewe kwa kujiridhisha kuwa mungu ni wa ajabu katika maisha yetu na hatuna sababu ya kumwogopa yeyote isipokuwa yeye; woga kwa Mungu ni chanzo cha maarifa. Mungu lazima aogopwe kwa sababu yeye ni chanzo cha  haki; chanzo cha upendo; na mafanikio yetu. Zaburi ya 77: 13

 Ili tuweze fanikiwa lazima tuishi katika mafundisho ya Mungu; tujiepushe  kwa kikombe cha  ubinafsi  na baada yake tunatakiwa tujazwe na kikombe cha roho wake ili kitupe ujasiri wa kuweza kushinda woga na kuwa tayari kuungama dhambi zetu ili kujipatanisha na Mungu. Bibilia inatufundisha kuwa watu wamegawanyika katika makundi makubwa matatu; maadui, majirani na wafuasi wa kristo. Jambo kubwa katika makundi hayo yanayoleta tofauti ni upendo upendo huleta kila kitu; tunawahitaji watu ili tuweze kuwauliza maswali; je tunawahitaji watu ili kukamilisha haja zetu? Wafilipi 2:3 auwarumi 13:8. Tukumbuke kuwa woga ni tatizo la jumla kwa binadamu.

Hii ndio tafakari yetu ya leo

Emmanuel Turuka


Wednesday, July 13, 2016

JE UNAMWONA SHETANI ANAKUNYEMELEA

July 13


Katika maisha yetu ya kawaida pamoja na mafanikio yetu tunakila sababu ya kuacha kujivunia mafanikio yetu dhidi ya wenzetu; tunatakiwa tuwe wanyenyekevu ili Mwenyezi Mungu aweze kutubariki zaidi na zaidi; lakini sio kuwa watu wa kujiona na kuwadharau wengine eti tu kwa sababu unao uwezo wa kifedha.

Saturday, July 9, 2016

NANI WA KUMLINGANISHA NA MUNGU

July 9


Tafakari yetu leo hebu jiulize unaweza kumlinganisha Mungu na chochote; Kwa haraka tu hakuna cochote cha kumlinganisha na Mungu yeye ni Alfa na Omega ni mwanzo na mwisho, Mfalme wa nyakati zote; mfalme wa wafalme; mwanga wa ajabu na hakuna awezaye kuyajua mapito yake;

amina

UMETAFAKARI UPENDO WA MUNGU?

July 8


Tafakari ya leo tutafakari upendo wa Mungu na Njinsi anavyotupenda sisi wanadamu; Ni wajibu wetu kutafakari katika upana wake na kutimiza wajibu wetu ili upendo huu uwe ndio taa na nuru yetu;

Amina