- TUTAKUKUMBUKA DAIMA
Kuna
msemo wa kale unaosema kuwa kifo kinatufungulia mlango na kutupeleka
sehemu ambayo hatuifahamu; lakini Yesu katika mahubiri yake aliupinga
mtanzamo huu pale aliposema katika John 11:25-26 “Mimi ndiye huo ufufuo
na uzima. Yeye aniaminiye Mimi, hata akifa atakuwa anaishi 26 na ye yote
aishiye nakuniamini hatakufa kabisa hata milele”. Mtume Paulo yeye
anatufundisha katika sura ya 14:8 kuwa 8 Kama tunaishi, tunaishi kwa
Bwana, nasi pia tukifa twafa kwa Bwana. Kwa hiyo basi, kama tukiishi
au kama tukifa, sisi ni mali ya Bwana.
Lakini
pamoja na uthibitisho wote huu kifo sio rafiki mzuri hata kidogo katika
maisha yetu kwani hata tukisoma kutoka katika kitabu cha Marko 14: 36
yesu aliwaambia wafuasi wake kuwa “Moyo wangu umejawa na huzuni kiasi
cha kufa. Kaeni hapa na mkeshe.” 35 Akaenda mbele kidogo, akajitupa
chini kifudifudi akaomba akisema, kama ikiwezekana saa hiyo ya mateso
imwepuke. 36 Akasema, “Aba c Baba, mambo yote yawezekana Kwako.
Niondolee kikombe hiki, lakini si kama nitakavyo Mimi, bali mapenzi Yako
yatimizwe.’’
Kulingana
na ubinadamu wetu tukio lolote la kifo halizoeleki hata kama utakuwa ni
shupavu kiasi gani, kifo ni tendo ambalo halina kipimo kabisa,
Ni takribani miaka kumi na tisa (19) imepita toka Mwenyezi Mungu alipokuita katika
makao yake ya milele; tulijiuliza maswali mengi; na tulipotamani majibu majibu yalikuja nusu nusu LAKINI tulifarajika na jambo moja kubwa la
kumshukuru Mungu kwa kumjalia maisha mema hapa dunia katika kipindi
chote cha uhaki wake, kwani alifanikiwa kutimiza majuku yake kwa kiasi
kikubwa na kulingana na neema na maagizo yake; ukiondoa ubinadamu wetu;
Je tunapowakumbuka wapendwa wetu yatupasa tufanye nini sasa?
- Tujitathimini uhalisia wa maisha yetu mbele yake kwa kujali zaidi matendo yetu na kuangalia mbele ili tuweze kusafiri katika mstari ulionyoka kama marko 8:62 62 Yesu akamwambia, “Mtu ye yote atiaye mkono wake kulima, kisha akatazama nyuma, hafai kwa Ufalme wa Mungu.”
Unakumbukwa
sana na Mke wako mama yetu mpendwa Anna M. Kinunda na watoto wako
wote, wakwe, wajukuu wako, vitukuu, marafiki na kila mtu.
Sisi
tulikupenda daima lakini mwenyezi Mungu alikupenda zadi kwani yeye
ndiye aliye toa na yeye ndiye aliyetwaa kama anavyotufundisha kutoka Kitabu
cha ufunuo 20:4 kinatukumbusha kuwa 4 Atafuta kila chozi, kutoka
katika macho yao. Mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio,
wala maumivu, kwa maana mambo ya kwanza yamekwisha kupita.’’
No comments:
Post a Comment