Familia ya Marehemu Mzee Robert Jaka wa Forest Hill - Morogoro, inapenda kutoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kumuuguza na hatimaye katika kuifariji familia wakati wa msiba wa mpendwa wao Mzee Robert Jaka, aliyefariki tarehe Jumapili ya tarehe 22.01.2012 na kuzikwa Jumatano ya tarehe 25.01.2012 katika makaburi ya Kola-Morogoro.
Kwa kuwa si rahisi kuwataja wote, familia inapenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani kwa Madaktari na wauguzi wote wa hospitali za Mkoa Morogoro na Regency ya jijini Dar-es-salaam: Pia tunawashukuru Magereza Makao Makuu; Chuo Kikuu cha Dar-es-saalam kwa msaada wao wa hali na mali.
Shukrani za pekee pia ziuendee uongozi wa kanisa katoliki parokia ya Mtoni Kijichi-Dar-es-salaam na Mtakatifu Patrick Morogoro kwa msaada wa kiroho.
Tunaomba wote mzipokee shukrani zetu hizi za dhati na kwamba Bwana awabariki kwa moyo mliounyesha kwa familia.
Mkesha wa msalaba utakuwa tarehe 13.04.2012 kuamkia tarehe 14.04.2012 (Jumamosi) ambayo itakuwa ni siku ya msalaba wenyewe.
Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe [Ayub. 1:21]
Denis Londo
Habari kwa Hisani ya Mjengwa Blog;
Kwa niaba ya Utawala wa Mungupamojanasi na Ukadirifu Blogs: tunatoa pole zetu kufuatia kifo cha mzee wetu Robert Jaka kilichotokea huko Morogoro; Daima tutaendelea kukumbuka daima: yale yote uliyotufanyia wakati wote wa uhai wako, hayo yote yataendelea kuwa hazina ambayo umeijenga mioyoni mwetu na haitaondoka kamwe;
Sisi tulikupenda sana sana lakini mwenyezi Mungu amekupenda zaidi kwani yeye ndiye aliyekuumba na akakufanya Baba Bora wa kuigiwa mfano umemaliza kazi yako hapa dunia kwa mafanikio makubwa;
kitabu cha Ufunuo 20:4 kinatukumbusha kuwa “Atafuta kila chozi, kutoka katika macho yao. Mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu, kwa maana mambo ya kwanza yamekwisha kupita.’’
Mioyo yetu bado kwa miaka yote hii imejaa majeraha, kwani tunakosa kicheko chako, busara zako; maelekezo yako; ushauri na busara zako;
Tunawaomba wanafamilia na ndugu kuendelea kuwa na umoja katika kipindi hiki chote kigumu;
Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi
Amina
No comments:
Post a Comment