Msiupende Ulimwengu
15 Msiupende ulimwengu wala mambo yaliyoko ulimwenguni. Kama mtu ye yote akiupenda ulimwengu, kumpenda Baba hakumo ndani yake. 16 Kwa maana kila kitu kilichomo ulimwenguni, yaani, tamaa ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima, havitokani na Baba bali hutokana na ulimwengu. 17 Nao ulimwengu unapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele;
Starehe za Walimwengu
Kwa walimwengu mtazamo ni kuwa yafurahie maisha katika hali yeyote ile hata kama maisha yanakufanya ulie kwa ugumu wake lakini wewe uonyeshe ulimwengu kuwa unasababu elfu moja za kifurahia kwa staili yeyote kama picha hii hapa juu inavyoonyesha; starehe kwanza halafu mengine baadae; Mungu tutamkimbilia “ BAADAE” baada ya starehe, bado tuna muda wa kutosha;
Jumapili hii tutafakari leo hii, asubuhi hii, sasa hivi tukiulizwa na Muumba wetu je unapendelea kupita daraja gani kumfikia yeye?
1. Daraja la uzima ambalo linakwenda moja kwa moja kwake na kwa Muda mfupi kama Waraka wa Yakobo unavyotufundisha;
2. Daraja la anasa na malimwengu linavyojieleza ambalo huna uhakika wa kumfikia yeye kwa wakati muuafaka kabla milango ya mbinguni haijefungwa;
No comments:
Post a Comment