Petro aligeuka na kumwona yuke mwanafunzi ambaye Yesu alikuwa
akimpenda sana; akumuuliza je na huyu vipi? Je kama mimi nataka kumwacha huyu
mpaka nitakaporudi wewe inakuhusu nini? Wewe nifuate mimi Yohana 21:21-22.
Tafakari yetu juma hili Yesu anatukumbusha umuhimu wa kuwa na kiasi katika
kutaka kujua mambo ya watu wengine; Tunatakiwa kuwa watu wenye hekima na kujali
Zaidi mambo yetu, tufanye kile ambacho yatupasa sisi kufanya; 1Wateselonike 4:11
tena mjitahidi kutulia na kutenda shughuli zenu,na kufanya kazi kwa mikono yenu
wenyewe kama tulivowaagiza.
Tunakumbushwa
sana kujitathimini na kuacha kuingilia maisha ya watu wengine; kwa msingi huu
kwamba tukiangalia sana wale ambao wako sana katika maisha ya watu
wengine; basi hawana thamani kabisa hata katika maisha yao ya kila siku; wako
tayari kunena ya watu wengine na kutoa hukumu ambayo imejaa hisia kulingana na
wao wanavyotaka iwe; kwa maneno mengine wanaweza kuwa chanzo cha mafarakano
katika maisha ya watu wengine katika jamii kwa ujumla. 2 Watesolonike 3:11 Maana
twasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao
wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine;
Lakini wale ambao siku zote wao wako katika maisha ya
Kimungu Luka 2:49 Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa
imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu?
hawatakuwa na muda wa kutumia muda wao katika mambo ya watu wengine, daima
watakuwa wakitembea katika busara ya Mungu na kutenda mambo yao kwa haki na
uadilifu wa pekee. Wakorinto 4:5 basi ninyi msihukumu jambo kabla ya wakati
wake; tukumbuke kuwa kila mtu anatakiwa kuwa tayari kuhangaika na mambo
yanayomhusu yeye mwenyewe; Katika jamii yetu, tukumbuke kuwa kuna watu
ambao wao kazi yako kubwa ni kulaumu na kukosoa tu hawawezi kuona kitu au jambo
nzuri lolote kutoka kwa wengine; na pengine ukibahatika kuona nini kinaendelea
katika maisha yao utashangaa kwa nini wako msitari wa mbele kuhukumu wenzao;
pengine maisha yao na hukumu ambazo wanazitoa kwa wengine hazilingani kabisa.
Tafakari yetu leo inaendelea kutukumbusha kuwa tunapoteza
muda wa kufanya mambo yetu mazuri yampendezayo Mungu kwa kujihusisha na mambo ya watu
wengine; lakini utagundua kuwa jinsi kuwahukumu wengine
katika mambo ambayo hayana msingi ndivyo tunavyowasaidia wao kufanikiwa Zaidi
na kuwa karibu na Mungu na kufanikiwa Zaidi. Tunatakiwa kuanza kusafisha nyumba zetu kabla hujeanza kuona uchafu katika nyumba ya wengine kwa kutumia ulimi wetu.
Na pale
tunapogundua kuwa maisha hayako vizuri yarekebishe na tuyasimamie na sio
kutumia muda mwingi katika kuhangaika na maisha ya watu wengine. Kwa nini uwe
na uchungu na maisha ya watu wengine? La msingi ni vizuri tukajifunza kutilia
mkazo maisha yetu na kuziondoa changamoto zetu za maisha. Ni rahisi kwetu kuona
Kibanzi katika jicho la wenzetu na kushindwa kuona boriti katika jicho lako au
langu;
Kwa kweli wakati mwingine inatakiwa tuamue kufunga masikio na kuziba
macho ili tuweze kusonga mbele; chochote ambacho tutafanya hakitaweza
kumridhisha kila mtu na kila mtu atatoa hukumu yake; kama tusipokuwa makini hao
ni waharibifu wa safari yako ya maisha; midomo yetu imejaa masengenyo na
majigambo; midomo yetu inapinga uumbaji wa Mungu dhidi ya wenzetu; maneno kama
mbaya, hana elimu ya kutosha; hana kazi nzuri; mwone kwanza: je haya maneno
yanaashiria nini katika uumbaji wa Mungu; Je Yesu alipokuja kutukumbo sisi
kutoka katika misha ya dhambi aliangalia vitu hivyo? Jibu hapana alitukomboa
sisi kulingana na njisi tulivyo bila kuangalia ukubwa au uwingi wa dhambi zetu; na jambo njema pamoja na mapungufu yetu sote tumepokea kipimo
sawa.
Tukisoma Injili ya Mathayo 7:5 Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika
jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la
ndugu yako.
inatukumbusha kuwa sisi tuko makini sana katika kuhakiki maisha ya watu wengine
na mapito yake; swali la kujiuliza je sisi tunafanikiwa vipi na kupata kibali
cha kuwahukumu wengine? Au nasi tumekuwa katika kundi la wanafiki kwa kupenda
tu kuhukumu? Tunatakiwa kuwa kioo cha matendo yetu na busara yetu kuwa mfano
kwa wengine? Tusome sana neno la mungu;
Tukisoma
kitabu cha Zakaria 4:10 Maana ni nani
aliyeidharau siku ya mambo madogo? Kwa kuwa watafurahi, nao wataiona timazi
katika mkono wa Zerubabeli; naam, hizi saba ndizo macho ya Bwana; yapiga mbio
huko na huko duniani mwote. katika
maisha vitu vinakuwa taratibu havilipuki tu kutoka kusikojulikana. Kila
mafanikio yanahitaji uwajibikaji na uvumilivu.
je unaona raha gani kuongelea mambo mabaya juu myu mwingine? kwa nini usiongelee mazuri au pale alipokosea usimrekebishe kwa upole na kwa busara iliyojaa unyenyekevu? itakuwa ni jambo la kufurahia kwa wakati huu wa mfungo na toba ni kujifunza kutenda kila jambo kwa haki kama Yesu alivyotutendea na uthibitisho wa hili ni kitendo cha kukubali kufa msalabani kwa wokovu wetu;
ushauri wangu kama unatenda jambo njema na unahukumiwa ni wakati wa kushukuru sana kwani unafanya jambo nzuri ambalo linawaumiza na wanataka kukurudisha nyuma; kumbuka ukiwaruhusu na kuwapa nafasi ya kukukatisha tamaa ujue kuwa nawe mwisho wako utakuwa umefika. Kama Yesu angesikiliza kelele zote za walimu wa sheria na wayahudi ambao walikuwa wanampinga; sisi tusingeweza kupata wokovu wetu huu ambao tunaufurahia leo. La msingi ukikabiliwa na mtihani wa aina hii simama kidete na ujipanga vizuri kwani ushindi wako unakaribia. Methali 18:21 mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; na wao waupendao watakula matunda yake.
je unaona raha gani kuongelea mambo mabaya juu myu mwingine? kwa nini usiongelee mazuri au pale alipokosea usimrekebishe kwa upole na kwa busara iliyojaa unyenyekevu? itakuwa ni jambo la kufurahia kwa wakati huu wa mfungo na toba ni kujifunza kutenda kila jambo kwa haki kama Yesu alivyotutendea na uthibitisho wa hili ni kitendo cha kukubali kufa msalabani kwa wokovu wetu;
ushauri wangu kama unatenda jambo njema na unahukumiwa ni wakati wa kushukuru sana kwani unafanya jambo nzuri ambalo linawaumiza na wanataka kukurudisha nyuma; kumbuka ukiwaruhusu na kuwapa nafasi ya kukukatisha tamaa ujue kuwa nawe mwisho wako utakuwa umefika. Kama Yesu angesikiliza kelele zote za walimu wa sheria na wayahudi ambao walikuwa wanampinga; sisi tusingeweza kupata wokovu wetu huu ambao tunaufurahia leo. La msingi ukikabiliwa na mtihani wa aina hii simama kidete na ujipanga vizuri kwani ushindi wako unakaribia. Methali 18:21 mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; na wao waupendao watakula matunda yake.
Inasikitisha sana leo kuona jamii na jumuia zetu zinatawaliwa na
nguvu ya masengenyo; wivu na undumila kuwili . hivyo kwa kweli kama tunapenda
kufurahia maisha mazuri lazima tujiepushe sana kuutumia ulimi wetu katika
kusema mambo mabaya juu ya wenzetu. Metali 6:17 mambo ambayo yanamchukiza sana
bwana Macho ya kiburi, ulimu wa uongo na mikono imwagayo damu isiyo na hatia.
Tukumbuke kuwa tunapokuwa tuko midumo juu tayari kuwahukumu na
kuwalaumu na kuwahukumu wenzetu, Mungu kamwe hana muda wa kutusikiliza yeye
wakati huu anafanya kama hatusikii na utuandalia adhabu, mfano wa Yesu na kundi la watu
waliompelekea mwanamke alifumaniawa katika tendo la unzinzi. Pamoja na kufafanua
sheria zote kuhusiana na kosa hilo Yesu alikaa kimya kama vile hawasikii,
aliponyanyuka aliwauliza swali kama kuna mmoja wenu asiye na dhambi awe wa kwanza kumrushia mama huyu;
Yohana 8:7. Fundisho hapa ni moja tu hukumu kama wewe hujetenda dhambi yeyote
ile; tujenge upendo wa kweli kati yetu upendo ambao huubagui; hii ndio tafakari
yetu ya wiki hii.
Amina
Amina AMINA
Emmanuel
Turuka
2017