WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Sunday, July 21, 2013

UJUMBE WA JUMAPILI YA LEO - IMANI NYALAMOYO KAPINGA

 
Mara nyingi shetani amekuwa akitufanya tupoteze muda mwingi kuwahukumu na kuwasema wengine vibaya kwa makosa yao wanayofanya.

Halafu akatusahaulisha tusione makosa yetu wenyewe na tusijibidiishe kutafuta namna ya kutubu na kujirekebisha.


-Hivi tunakumbuka kweli kuwa kila mtu atahukumiwa kwa dhambi zake na si za mtu mwingine?


-Je ni kweli tumekuwa vipofu sana kiroho na kimwili tukasahau kuwa hata sisi wenyewe tunakosea mara nyingi tu tena makosa yaleyale ambayo tunayowasema wengine? na wala hatujishughulishi kutafuta namna ya kujirekebisha.


Warumi 3-7

Wewe, rafiki, unayewahukumu wale wanaofanya mambo kama hayo ambayo hata wewe pia unayafanya, je unadhani utaiepa hukumu ya Mungu? Au labda unaudharau wema wake mkuu, uvumilivu wake na saburi yake na umeshindwa kutambua kwamba wema wake huo una shabaha ya kukuongoza upate kutubu?

Lakini unao ugumu na ukaidi wa moyo, na hivyo unajilundikia adhabu kwa Siku ile ambayo ghadhabu ya Mungu na hukumu zake za haki vitadhihirishwa. Siku hiyo Mungu atamlipa kila mmoja kufuatana na matendo yake.

No comments:

Post a Comment