WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Friday, July 13, 2012

MUNGU AMETENDA MAAJABU KWA DADA YETU FLORA KASAMBALA


  • TUNAMSHUKURU MUNGU  KWA NEEMA YA UPONYAJI

  • ASANTE KWA  KUUNGANA NASI KATIKA MAOMBI

  • AMA KWELI TUMWACHE MUNGU AITWE MUNGU





Mama yetu mpendwa Marina Kasambala anapenda kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa muujiza wa uponyaji wa Binti yake mpendwa Mama yetu, Dada Yetu, Ndugu yetu na Rafiki yetu Mpendwa Flora Kasambala (Mama Albert); kwa jinsi mkono wa Mungu ulivyoweza kumponya na kuendelea kumpigania mpaka sasa akiendelea kupata neema ya uzima kama zawadi ambayo tunamwomba Mwenyezi Mungu atujalie kila siku.

Mama Marina (Bibi) wakati wote wa kumuuguza Dada yetu Flora alimwambia Mungu Mimi si kitu! Mungu ndiye; kama Zaburi 30:2-3 inanyosema; Ee BWANA, nilikuita unisaidie na wewe umeniponya. Ee BWANA, umenitoa kuzimuni,  umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti. Kwa hakika Mungu amekuwa tulizo letu katika kipindi hiki chote cha kumuuguza Dada yetu Flora kama Bibilia inavyotufundisha kupitia Isaya 53:4 “Hakika magonjwa yetu Yeye Mwenyewe aliyabeba, na maumivu yetu aliyachukua.” Na Mathayo 8:17 inasema; “Yeye Mwenyewe alichukua udhaifu wetu na kuyabeba maradhi yetu”

Kama binadamu tunasahau kuwa tulishapewa ufunuo kuwa Maradhi ni moja tu ya matokeo ya anguko, lakini tangu mwanzo Mungu anaahidi wokovu na neema; tukisoma Kitabu cha Ebr 12:2 kinafafanua zaidi kuhusu hili pale kinavyotueleza kuwa  tunapokabiliwa na matatizo ya afya tunatakiwa                                       
kuacha kuangalia ugonjwa na badala yake tumwangalie Yesu. Hatuwezi kuangalia sehemu mbili kwa wakati mmoja kama kinyonga. Yatupasa kuchagua; ama tuangalie magonjwa yetu au tuangalie ahadi ya Mungu. Mama yetu Marina pamoja na familia yake, Rhoda Kasambala, Suma Kasambala na Stella Baake pamoja na familia zao  wakati huu waliangalia ahadi ya mungu kama ilivyotokea kwa Ayubu ambaye alivumilia mateso makali yasiyoelezeka mpaka hatimaye akaponywa na kupokea baraka mara mbili; na kuthibitisha maneno ya Malaki 4:2 yasemayo kwamba Bwana ana uponyaji katika mbawa zake.               


Leo hii dada Flora Kasambala baada ya kupona anarudi, na kwa sauti kubwa anamtukuza Mungu, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Luka 17:15-16.

Wakati wa shida kulingana na udhaifu wetu wa kibinadamu tunasahau maagizo ya Mungu wetu kupitia mitume wake kama kitabu cha Mathayo 21:22 kinavyotukumbusha chochote mtakachoomba katika sala, mtapata, kama mkiwa na imani. Nayo: kitabu cha Mtume Marko 9:29 kinatukumbusha kuwa Maombi ndio msingi wa mafanikio yote; 11:24 Yoyote myaombayo katika sala, aminini ya kwamba mtayapokea, na yatakuwa yenu; na na kitabu cha Yohana 14:13-14 kinasisitiza kuwa mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana na mkiniomba neno lolote kwa jina langu nitalifanya’. Tunamshukuru Mungu kwani Mama yetu Marina pamoja na familia yake yoye na ndugu na marafiki walitekeleza agizo hili.

Familia ya Mama Marina Kasambala inapenda kutoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki wote waliopo Marekani, Tanzania, Canada na Malaysia kwa ushirikiano wao katika maombi na misaada mingine ya hali na mali wakati wote wa kumwuguza Dada yetu Flora kwa misingi ya maagizo ya bibilia. Mungu aendelee kuwabariki na kuwapa heri katika Maisha yenu ya kila siku.

Tunamaliza kwa maneno ya Mtume Pulo kwa 1Wakorinto 15: 57-58 “Lakini, shukrani kwa Mungu, ambaye ametupa ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. Na hivyo, Ndugu zangu wapenzi, kuwa imara namsiyumbe, Muwe daima katika kazi ya Bwana, kujua kwamba kazi yako si bure katika Bwana”.

Asante Mungu kwa neema hii ya pekee ya uponyaji kwa Dada Yetu Mpendwa Flora Kasambala.

AMEN.

No comments:

Post a Comment