UKOSEKANAJI WA UHALISIA KATIKA FILAMU ZA KITANZANIA.
- TATIZO NI UHABA WA ELIMU KATIKA SANAA YA FILAMU?
- TATIZO NI TEKINOLOJIA NDOGO?
- TATIZO NI KULEWA SIFA NA HATIMAYE KUTOKUWA MAKINI KATIKA UIGIZAJ?I
Mr Emmanuel Myamba katika moja ya washa aliwahi sema kuwa “Ni wazi ukiangalia filamu zetu zinakosa weledi katika uandishi wa miswada, uongozaji, uhariri na hata uumbaji wa wahusika. Lazima tukubali udhaifu huu turekebishe” aliendelea kueleza kuwa “Nimekuwa katika tasnia ya filamu kwa muda sasa lakini kuna changamoto nyingi katika tasnia ya filamu, na jambo ambalo nimeliona ni wasanii kukosa ujuzi kitaaluma katika utendaji wa filamu kwa ujumla, kwa mantiki hiyo nikaamua kufungua chuo hiki kwa ajili ya wasanii maskini wasio na uwezo wa kulipa ada kubwa katika vyuo vilivyopo, lakini pia kutoa nafasi kwa wale ambao wanafanya kazi lakini taaluma imekuwa shida kwao, na mwito ni mkubwa kweli,”
“Tatizo kubwa la wasanii wa Tanzania kushindwa kufaidika na vipaji na ujuzi wao, ni kukosa elimu ya kutosha ya mambo ya sanaa, kwa mantiki hiyo nikaamua kufungua chuo hiki kwa ajili ya wasanii, nimeapa kwamba nitaweka ada ndogo ili wasanii wachanga au kwa ujumla tuseme wasio na uwezo mkubwa wa kifedha waweze kusoma hapa,”
Kati ya waigizaji wanaoigiza kwa hisia na kuvutia nyoyo za mashabiki hapa Tanzania basi hutakosa kumtaja Emmanuel Myamba a.k.a Pastor Myamba ambaye mara nyingi tumezoea kumuona akiigiza kama mchungaji au mtu mwenye maadili ya dini.
Mimi kama mdau wa senema za kibongo ninamkubali sana msanii huyu hasa katika kipaji chake cha kuigiza katika hali ya uhalisia wa maudhui ya kidini na kweli amefanikiwa kuvaa uchungaji wa kweli ambao ni zaidi ya movie wakati ni movie tu. Kutokana na kipaji hicho na umakini wa uigizaji wake wadau wengi tunajua kuwa Myamba ni mchungaji ambaye anakanisa lake, lakini kumbe sio, yeye ni mwigizaji na muumini wa kawaida tu. Hali hii sis wadau wa filamu ndio tunatamani kuangalia filamu zenye uhalisia wa namna hii. Katika kundi hili wasanii kama Dr. Cheni, JB, Wema Sepetu na Shamso Ford ni baadhi ya waigizaji ambao wanakuwa makini katika katika uigizaji wao;unaweza kufurahi nao au kulia nao ukifikiri kile kinachochezwa ni ukweli mtupu, kumbe sio ni falamu tu.
Swali ninalojiuliza hapa nini ambacho kinakosekana kwa wasanii wengi hata wale waanzilishi wa Tasnia hii? je tatizo ni nini? Je ni kweli swala la elimu linachangia kama?
Pastor Myamba alivyoshauri kuwa “ni vyema kupata elimu kwani elimu inakufanya ujiamini juu ya unachokifanya na kwa umakini zaidi”.
Nina Imani kuwa kusaka maarifa ya namana ya kutengeneza sinema zenye uhalisia na visa litasaidia sana kuleta ushindani sio tu wa ndani bali wa limataifa; ikumbukwe kuwa filamu ambazo zinakosa uhalisia zinapunguza mvuto, na hivyo kuwafanya watazamaji kuishiwa na hamu ya kuziangalia filamu hizo na kuwakosesha kipato na kuongeza umasikini miongoni mwa wasanii.
Kama Gayo alivyowahi kushauri kuwa “Ikiwa tutaendelea kutengeneza filamu zisizo na weledi, zenye visa vilevile na zenye kusukumwa na wasambazaji au haja ya kuchuma fedha za haraka tu watu watatuchoka na baadaye soko litakufa”.
Hivyo kilio cha elimu kwa wasanii kimekuwa ni kilio cha wadau wengi hapa Gayo anasisitiza kuwa “Pia wasanii na watendaji wengine wanapaswa kupatiwa mafunzo, kwangu mafunzo ndiyo kitu cha kwanza muhimu kwa mtu yeyote yule katika kumuongezea stadi zake za utendaji. Kwa jumla kuna upungufu mkubwa wa mafunzo ya fani mbalimbali za sanaa, ikiwemo filamu. Wasanii wengi wanajifunza kwa kuiga wenzao. Ingawa hii ni moja ya njia za kujifunza, tatizo lake ni kuwa huchukua muda mrefu na haina hakika kama kinachoigwa ni sahihi au la”.
Je ni kweli sekta hii ni ya watu ambao hawajasoma? Mimi ninasema hapana? Isipokuwa ni sekta ambayo wahusika wake baada ya kushika pesa kidogo hunogewa na hawataki kujiendeleza kwa kujipanua katika elimu ya uigizaji; na kwa hiyo ufanisi wa kazi umekuwa wa chini mno.
Msanii Myamba ametuletea changamoto nzuri ya kuanzisha chuo cha filamu Tanzania kuppitia chuo hiki wasanii wataweza kukabiliana na changamoto za uandaji wa filamu kwa wasanii kukubali kujiongezea ujuzi na masilahi bora.Kwa hiyo eneo hili la mafunzo linahitaji msukumo siyo tu wa kuongeza nafasi bali pia ubora wake.
Wazungu na kiingereza chao wanasema "Knowledge" comes from getting educated.
"Experience" comes from real life encounters. There is a famous saying that says.
"Experience is better than knowledge!" and "Experience is the Best Education In Life."
Experience and knowledge go hand in hand.
Knowledge is important, because it makes you aware of what is around you. Knowledge also enables a person to become wealthy.
The more knowledge we have, the more advanced we can become. Education can give you a good job and assure you a secure future. The world needs knowledge to discover new things to help everyone.
Msanii kama kioo halisi cha jamii inayomzunguka, anatakiwa kuuvaa uhalisia wa fani yake ili Yule anayeamua kumwangalia aweze kufaidika na tasnia hiyo. Ili kufikia malengo stahiki, wasanii mmoja mmoja au kwa pamoja wakipata upeo juu ya haya, wataweza kutekeleza ipasavyo majukumu yao na kuwa msaada mkubwa katika kuielimisha jamii juu ya mambo mbalimbali.
Nachukua nafasi kumpongeza Msanii Emmanuel Myamba aka Pastor Myamba kwa kuliona hili na kuanzisha chuo cha kuwaelemisha na kuwapa ujuzi unaostahili wasanii wengine ili waweze kukabili changamoto za kufanya kazia zao kwa makini na kwa uhalisia unaotakiwa katika tasinia ya filamu nchini kuptia Chuo kinachojulikana kwa jina Tanzania Film Training Center (TFTC) kilichopo Ubungo Dar Es Salaam ambacho hutoa mafunzo mbailimbali ya filamu,ikiwemo acting, directing, editing, production management,producing nk.
Nina imani chuo hiki tutawasaidia wasanii wachanga na wakongwe wapate fursa ya kujiongezea ujuzi kitaaluma ili kukabiliana na changamoto mbalimbali katika soko la filamu la ndani na la kimataifa. wazo hili la uanzishaji wa chuo maalum cha uigizaji ni uamuzi wa busara ambao hata serikali inatakiwa kuunga mkono jitihada hizi binafsi. Mungu ibariki Tanzania