Leo tunatimiza mwaka mmoja toka
mama yetu mpendwa mama Anna kinunda aka Mbuya atangulie mbele ya haki; furaha
yetu kubwa ilikuwa jinsi ambavyo aliweza kuipiga vita yake kwa ushindi mkubwa;
na kufanikiwa kushinda Tuzo na huku kuendelee kuilinda imani yake mpaka mwisho
wa safari yake kama vile Mtume Paulo alivyoandika katika waraka 2 Timotheo 4: 5-8.
Mwaka mmoja unatukumbusha jinsi
yeye alivyoyaweka maisha yake katika mwongozo wa Mungu akijua kuwa mapambano
ambayo alikuwa akipitia na kuyafanya yalikuwa ni juu yake na Muumba wake na
hakuna mtu mwingine yeyote ambaye angeweza kumzuia na kumshawishi tofauti ndio
maana aliamini kuwa imani ameilinda: Silaha yake katika ushindi wake ilikuwa ni
kutimiza amri kuu ya upendo, ambayo ukiitimiza vizuri utaishi maisha ya
uaminifu; hivyo hakukuwa tayari kumpa shetani nafasi kwani aliishi maisha yake
ili kumtumikia Mungu na sio maisha ya kujilinganisha na mtu au watu wengine:
aliishi vile Mungu alitaka sisi tuishi:
Daima alikuwa akimpendeza Mungu
zaidi; na sio kuwafurahisha watu wengine katika mambo ambayo sio ya kimungu;
aliishi maisha ya kuwasaida sana wahitaji wale ambao walikuwa wakihitaji
msaada; alikuwa tayari kujinyima yeye kwa faida ya taifa la Mungu hasa watoto
na wazee ambalo lilikuwa likihitaji msaada;
Mbuya Anna aliishi maisha ya
kutimiza wajibu wake kama mkristo kwa kumpigania Kristo: alitukumbusha wakati
wote tusikae chinina kusoneneka na kujilaumu kwa makosa ya jana wajibu wetu
daima ni kuomba msamaha na msaada wa Mungu; amakweli Mbuya yeye alichagua fungu
lililo sahihi kama Mary katika Luka 10:41-42 : je wewe na mimi ni akina
Martha tunahangaika sana na mambo ya kupita na ya Muda mfupi ya dunia hii?
Tukumbuke kuwa utawala wa Mungu
kamwe hautapotea au kufa kwani juu ya mwamba atalijenaga kanisa lake na
hakuna nguvu ya kuzimu ambayo inaweza kulishinda Mathayo 16:18;Mbuya alijua
kuwa neema ya Mungu na thamani ya Mungu ilikuwa kuwa zaidi katika maisha
yakendio maana aliipigania kwa nguvu zote; je wewe na mimi tunamsimamo gani? Ni
wakati wetu sasa wa kusimama imara kumwambia shetani sasa ondoka mbele yangu;
umepoteza furaha; upendo wangu; amani yangu na nuru ya uzima wa milele sasa
nimesimama na kumwomba anisamehe kwani mimi narudi katika njia iliyo sahihi
aipendezayo Mungu; tumwombe Mungu Msamaha kama Daudi alivyofanya katika zaburi
ya 51
Tuwe kama Mwana mpotevu
aliyetambua makosa yake na kuamua krudi kwa baba na kuomba msamaha wa makosa yake:Mwenyezi
Mungu anafurahi pale tunaporudi kwake na kuomba msamaha ili tuweze kushiriki karamu
nzuri ya mwana kondoo aliyechinywa kwa ajili yetu;
Raha ya milele mpe bwana na
Mwanga wa Milele uendelee kuyangaza maisha yake katika nuru ya Kimungu kwani
ameipigana vita vilivyo: Tuzo amepata; na Imani aliilinda na sasa amevikwa Taji
lile ambalo alikuwa ameandaliwa pamoja na wale wote ambao wametimiza wajibu wao
wa kuishi maisha yaliyompendeza Mungu
AMINA
AMINA