June 1
Yohana 13:13
Tafakari yetu
leo tuangalie kwa nini Yesu amekuwa mwalimu bora kupita wote? Tuangalie hata
mafundisho yake yalikuwa na nguvu sana sana; tuangalie pale alipotoa hotuba
pale mlimani alipomaliza tukisoma kutoka Injili ya Mathayo 7:29 umati wote ulishangaa
kwani alikuwa anaongea kama mtu mwenye mamalaka na sio kama wanasheria. Tunajua
kuwa Yesu hakuingia darasani. Hakuwa na shahada yeyote kama ilivyo kwa wengi
wetu kwani usomi wetu na upapanuaji wetu wa vitu kwa usahihi lazima uende shule
kwanza; kwa vipengele hivi kwa kweli alikuwa mwalimu mzuri na bora kuliko
mwalimu mwingine yeyote Yule kwa wakati wote; Yesu ni mfano wa kila kitu kizuri
na kilichokamilika alikuwa hana makuu, mnyenyekevu, mpole na sio aliyekuwa
anafundisha ubinafsi katika mafundisho yake;
Tafakari yetu
inatukumbusha kuwa Yesu amefundisha sana na mafundisho yake yalikuwa yakipata
wasikilizaji wengi sana; ambao wengine walikuwa wakimfuata kila alipokuwa
akienda kuhubiri na kufundisha; wengi walimwona kuwa mafundisho yake kama mwalimu
bora yalikuwa yamejaa ufafanuzi ambao ulikuwa umejaa ukweli; alikuwa akikemea
maovu na kuleta mabaadiliko katika jamii ili waweze kubadilika. Yesu alianza
kufundisha akiwa na umri mdogo alipokuwa akiwajibu makuhani na walimu wa sheria
maswali hekaluni tukisoma kutoka Luka 2:46-47 au hata tukisoma
Luka 4: 21- 36 ni mwendeleo wa mafundisho yake na aliishia kufundisha kabla ya kufa msalabani pale ambapo
aliwafundisha kuhusu karamu ya mwisho.
Tafakari yetu
inaumuhimu mkubwa sana kwetu sisi kujifunza kuwa Yesu alikuwa mwalimu bora kwa
sababu watu wa kawaida waliweza kumwelewa vizuri sana; alikuwa hafundishi ili
ajikweze na kwa kutumia njia ngumu ili watu sio wamwelewe bali wamsifie kuwa
mafundisho yake huwezi yaelewa; alikuwa hafundishi kama walimu wa sheria na
makuhani kwa kutumia lugha kuapa na kuogopesha watu wengine; bali alikuwa
akifundisha kwa kutumia lugha ya kawaida kabisa;alikuwa akifundisha kwa kutoa
mifano ya kawaida hata wakulima waliweza mwelewa; hata pale ambapo mfano wake
haukueleweka bado alikuwa mpole na kutafuta njia rahisi ya kuwaeleza wasikilizaji
wake; warumi 5:2
Tafakari yetu inaendelea kutoonyesha kuwa hata baada ya kufa na
kufufuka alikaa na wafuasi wake kwa siku 40 akiwafundisha majukumu ambayo
watufanya baada ya yeye kuondoka katika dunia hii Matendo ya Mitume 1:3;
aliwafundisha kuwa itatakiwa waende dunia kote wakatangaze injili ya Yesu
wakiwabatiza watu kwa jina la baba na la mwana na Roho Mtakatifu Mathayo 28:
19- 20: hivyo tunaona kuwa Yesu alikuwa mwalimu ambaye aliweza kuwafundisha
watu wa elimu yeyote na wa mazingira yeyote bila shida yeyote. Na wote walikuwa
wakifuatilia mafundisho yake waliweza kumwelewa na kuyafurahia bila shida
yeyote ile.
Hii ni tafakri ya leo tunapotambua kwa kifupi uwezo na ubora wa Yesu kama Mwalimu bora sana; Amina
Emmanuel
Turuka
No comments:
Post a Comment