May 30
Wagalatia 6:9
Tafakari ya leo tunaangalia dhana nzima ya maisha yetu tukijua
kuwa Maisha yetu yamezungukwa na mitihani mingi sana. Lakini ili tuweze
kukabiliana vizuri na mitihani hiyo ya maisha lazima tujijengee nidhamu ya hali
ya juu na nia madhubuti ili tuweze kushinda. Hivyo hivyo katika kuimarisha
ukristo wetu; lazima daima tuweke katika akili zetu malengo yetu ni yapi;
Tujifunze kusahau yaliyopita; lazima tuondoa katika akili yetu dhan zima ya
mambo magumu ambay tunafikiri hayawezekaniki; na kujiondole avipingamizi
vinavyokuzunguka wewe mwenyewe ambavyo kwa namna moja au nyingine hukurudisha
nyuma; hatutakiwi kufikiria mambo hasi; hatutakiwi kutaka tama na kuishi kwa
kunungunika;
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa lazima tuishi katika malengo
makuu mawili; kuishi maisha yenye mwelekeo na maisha yaliyojaa shauku; Mwenyezi
Mungu siku zote ametupa sisi njia na mbinu za kushinda; lakini wajibu wetu
lazima tuwe na nia ya ushindi; nia ambayo haiwezi kukatisha tama na yeyyote
Yule; Mwenyezi Mungu kwa kutambua ushindani wa maisha ambao uko mbele yetu
alitupa sisi maarifa kwani kwa maarifa sisi tutakuwa huru na kufanya maamuzi
sahihi; Ametupa sisi uhuru wa kufanya maamuzi yaliyo sahihi; lakini kwa udumafu
wetu hata pale ambapo maji ni mengi lakini bado tunalalamika kuwa tunaona kiu;
kwa nini khali kama hii inaweza tokea Jibu ni rahisi tu ni ukosefu wa Maarifa
sahihi na kujiamini.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa lazima tuachane na vitu vyote
ambavyo vinazuia na kuchelewesha utekelezaji wa mipango endelevu ya kuwa na nia
nzuri ya kufanya mazuri katika maisha yetu katika kuufikia uzima wa kweli; Ili
tuweze kufanya vizuri tunahitaji kutayarisha akili zetu ili ziweze kuwa tayari kupokea matokeo ya matendo mazuri. Tukikumbuka kuwa
kuweka Nia ni kitu muhimu katika maisha yetu; ni tendo linalotufanya sisi
kuendelea kutenda jmabo wakati tayari tulikuwa tumeanza kukata tama; Kuweka nia
kutufanya sisi tusiwe na mawazo ya kuacha kutenda jambo iwe katika kazi; maisha
ya kawaida na hata kwenye ndoa zetu; Kuweka nia kunatusaidia sisi kupambana na
dhoruma za maisha na vishawishi mbali mbali; hakuna kati yetu anaweza kufanikiwa bila kuwa na nia dhabiti. Hata
kuishi kwa mafanikio katika maisha ya kumpigania Kristo kunahitaji kuwa na nia
dhabiti; wagalatia 6:9 inatufundisha kuwa Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa
wakati wake, tusipozimia roho.
Tafakari yetu inatufundisha kuwa ujasili unategemezwa na nguvu ya
Mungu kwa kuomba na kumtegemea yeye kwani
katika 2 Wakorinto 12:9 anatuhakikishia kuwa Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu
hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili
uweza wa Kristo ukae juu yangu. Tunachotakiwa
kukumbuka kuwa wakati wako Mungu aliokupa katika kufanikiwa haya ya moyo wako
ni wakati wako na unatakiwa kuufanyia kazi bila kuogopa; tukumbuke kuwa
unapokabiliwa na vipingamizi vyovyote unachotakiwa kusema kuwa kwa nguvu za
Mungu hakuna awezaye kusimamisha hiki ambacho nimepanga au lengo ambalo
nimetaka kulifikia. Nguvu za Mungu zimenijengea nia madhubuti katika moyo wangu
na utendaji wangu; Popote nitakapo kanyaga nguvu na Baraka na Mwongozo wa Mungu
u juu yangu.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa sisi binadamu
tukumbuke kuwa kitu cha thamani sana ambacho tunakimiliki ni kuwa na NIA
thabiti; hata kama utakuwa na Pesa lakini huna NIA ni kazi bure mali zako
zitapotea bure. Hivyo hatak kama tutakuwa tukitembea katika bonde la uvuli wa
mauti kama tuna nia na tunamtegemea Mungu hakuna kitu ambacho kitaturudisha
nyuma lazima tuwe na NIA thabiti ya kuvuka na kufika katika uvuli ambao umejaa
majani mabichi.
Hii ndio tafakari yetu ya leo;
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment