May 26
Zaburi 32:8,
Tafakari ya leo hebu tujiulize swali moja je tunajua wapi tunakokwenda? Mwanazaburi anatukumbusha kuwa atatuongoza na kutufundisha njia mbayo yatupasayo kwenda. Kwa maneno mengine sisi hatujui tunakokwenda bila msaada wa Mungu. Kwa kweli japo tunajifanya tunajua wapi tunakutaka kuwa lakini Mungu anatukumbusha kuwa bila yeye sisi hatujui na wala hatuna hata hisia ya wapi tunapaswa kwenda. Kwa maisha ya kawaida tuonaona jinsi watu wanavyobadilisha kazi, kuhama makazi kila baada ya muda mfupi; ndio sababu kila baada ya muda mfupi inatupasa kuanza kuzoeana upya na majirani wapya tatitzo sisi kama binadamu hatujui wapi tunakwenda. Nafikiri japo tuko barabarani tunakwenda kwa vile hatujui tunakokwenda hata tunavyopotea hatujui. Uelewa wa kupotea lazima ujue mwisho wa safari yako; safari hii ya kiroho ambayo inachanganya watu wengi tunashindwa kujua wapi tunakokwenda kwa vile GPS ambayo tumepewa ili tuifuate hatujewasha kwa makusudi kwa kuona kuwa itatuchelewesha kwa vile inambambo mengi ya kuyafuata kabla ya kuanza safari.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa kwa kweli
safari hii kama hatutaruhusu miingiliano ambayo inachukua akili na mawazo yetu
kando ni rahisi san asana; tatizo letu tunaruhusu vitu ambavyo sio vya msingi
na lazima kuingilia safari hii na matokeo yake tunaishi kuto jua njia ipi
tunatakiwa kupita na kuisha kuwa hatujui wapi tunanataka kwenda. Wakati mwingine
ni woga na kuogopa maneno ya watu ambao watakucheka katika safari yako hii.
Tujajua kuwa Yesu alipoanza safari yake ya ukombozi alijua safari yake inaanzia
wapi na atapambana na vikwazo gani mpaka mwisho wa safari yake ilipowadia pale
Goligoata na kufa Msalabani na Damu yake ikamwagika kwa ajili ya wokovu wetu.
Hivyo hata maandalizia yake yalikuwa wazi aliongonzwa na roho Mtakatifu,
alifunga kwa siku 40, alikuwa akisali muda wote daiama alifuata maelekezo ya
Mungu ambaye alimtuma aje duniani kwa ajili ya wokovu wetu;
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Yesu pekee
alijua wapi ametoka na anakwenda wapi na nini alikuwa anatakiwa afanye wakati
wa safari; na hata wakati wa mapumziko wakati wa safari aliendelea kufanya
matendo mema ya kuwasaidia watu wengine ili waweze kujitambua kuwa kusafiri na
hasa safari ya ufalme wa Mungu lazima iweke nia madhubuti, lazima uwe na imani
madhubuti na lazima uwe tayari kushinda majaribu na vishawishi mbalimbali
ambavyo vitajitokeza vikiwa na lengo ya kukukwamisha ili usifike salama mwisho
wa safari yako; majaribu yatakuja kimwili, kiroho na hata kijamii; vitu kama
kupenda sana pesa ambazo zinatumika katika anasa; choyo; wivu; mauaji; wizi na
unyanganyi; vitu hivi vyote hupelekea watu kufanya unyama wa ajabu dhidi ya
binadamu mwenzao; lakini tukumbuke kuwa bado tunanafasi ya kuandaa safari hii
na kuifanya kuwa na mwelekeo unaotakiwa kwa neema ya Mungu. Mungu ni mwema
msamaha wake ni mkubwa kuliko dhambi zetu. Lakini lazima tujipende sisi wenyewe
ili tuweze kuzishika na kufuata alama zote za Barabarani kama Mwenyezi Mungu
anavyotaka sisi kufuata kupitia Mwokozi wetu yesu Kristo. Mungu daima yuko
pamoja nasi na anataka sisi tutembee naye ili kufika mwisho wa safari yetu
tukiwa washindi.
Tutafakari pamoja na tuanze kujifikiria leo kuwa je tuko katika
mwelekeo ambao ni sahihi katika safari hii maisha ya baadae? Hii ndio tafakari
yetu ya leo – Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment