May 19
Zaburi 46:10
Tafakari ya leo inataka
tujiulize kuwa je umewahi kujisikia kuwa maisha yamekuchakaza? Na ukajiona kuwa
umebanwa katika ulingo na huna mahali pa kutokea au kujiokoa? Na unajishangaa kwa
nini umefika katika wakati kama huo na huna msaada wa njisi ya kujinasua? Hata tukisoma
katia katika kutoka katika Bibilia tunawaona wana wa Israeli walifikia hatua
hii katika Sura ya 14 hawakuweza kujinasua kwa kurudi nyuma au kwenda mbele
walikuwa na mwelekeo wa upande mmoja tu na hawakujua nini cha kufanya. Tujiulize
tena je umwewahi kukumbwa na khali kama hii katika maisha yako? Unakuwa katika
khali ya kupooza, huwezi kwenda kulia wala kushoto na hujui nini cha kufanya;
angalisho hapa kuwa hata sisi ambao ni wakristo tunaweza kumbwa na khali kama
hii lakini biblia inatufundisha kuwa tukipatwa na khali kama hii kimbilio
lisiwe kujiua kama watu wa mataifa wafanyavyo.
Tafakari inatukumbusha
kuwa kama wakristo tunatakiwa kuwa watu wa furaha wakati wote na hatutakiwi
kuhofu chochote; bali kuwa watu wa shukrani wakati wote; najua tatizo kubwa
ambalo linalutusumbua je utakuwaje na furaha wakati uko kwenye dimbwi la
matatizo? Je utakuwaje na furaha wakati unamwomba Mwenyezi Mungu akutoe kwenye
hizo shida na huoni dalili ya unafuu na shida zinaongezeka? Lakini bado
tunasisitizwa na bibilia na mafundisho ya Yesu kuwa tunatakiwa kufungasha
matatizo yetu na kumkabidhi Mungu ili yeye pekee abadilishe matatizo yetu kuwa
kicheko. Hivyo hatutakiwi kabisa kugeuza mioyo yetu kuwa jehanamu. Tukumbuke kuwa
shida nyingi ambazo tunakumbana nazo katika maisha yetu ni sababu ya sauti
nyingi ambazo tunazongana nazo katika vichwa vetu, ambazo zimejaa Mawazo Hasi:
mara nyingi mawazo yetu hasi yanatokana na ugumu wetu wa kusubiri neema ya Mungu katika kututoa katika ugumu
wetu wa maisha. Tunakuwa hatuna subira hata kidogo; tunalinganisha neema ya Mungu
kama vile tunasubiri ahadi ya rafiki ambaye wakati mwingine hana uhakika kama
atatekeleza; Tumesahau kuwa ahadi ya Mungu ni ya uhakika.
Tafakari yetu
inatukumbusha kuwa tujifunze kusubiri ili kuona neema ya Mungu ndani ya maisha
yetu na shida zetu; Hapo ndipo tunapotakiwa kusimaa IMARA na kuondoa tabia za
kibinadamu za kujiamulia na kutekeleza hatima yetu ambayo mwisho wake
haitusaidii kwani haituondoi katika matatizo. Tukishika usukani vibaya
tukumbuke kuwa Mungu wakati wote anatusaidia kuonyesha na kuongoza njia ili
tusinase katika tope; hataki tuendelee kuzama
Jukumu letu ni kuwa tayari pale Mungu anapoongea nasi na kutoa maelekezo
ya namna ya kufanya. Ni jukumu letu kufanya na kusubiri wakati wa Mungu na si
wakati wetu. Tumkumbuke Musa alipowavusha wana wa Isarel katika bahari ya sham
pamoja na woga na kelele za kuwa tutaangamia; hawakufanikiwa kuvuka mpaka pale
Mungu alipomwambia Musa sasa Nyosha Mkono wako , na alifuata maelekezo ya Mungu
na Bahari ya sham ikagawanyika sehemu mbili na wakapata njia ya kupita.
Tukumbuke kuwa imani
haisikilizi, viashiria vya nita nita, imani haisikilizi watu ambao hawana
uvumilivu, imani haisikilizi waoga, walio kata tama bali Imani husikiliza Roho
wa Mungu ambaye katika majaribu na shida zote Imani itakuambia Simama Imara na
uamini kuwa mimi ndiye mwanzo na mwisho wa Maisha yako. Tukumbuka Hadithi ya
Yairo; kama ilivyosimuliwa katika Luka sura ya 8. Alipomlilia Yesu akamponye
Binti yake ambaye alikuwa anaumwa sana. Kwa sababu ya umati mkubwa wa watu
Yairo hakufanikiwa kuongea na Yesu na alipokuwa tayari kuongea na Yesu alipwea
taarifa kuwa Binti yake amefariki. Hapa Yairo alikuwa kwenye matatizo makubwa
ambayo hawezi kujitoa mwenyewe, lakini yesu alimwambia usihofu alikwenda naye
nyumbani kwake na Kumfufu Yule Binti yake wa miaka 12. Lisilowezekana kwetu kwa
halishindikani kwa Mungu ndio maana tunatakiwa kusisma Imara.
Kwa hiyo tutakumbusha kuwa
katika khali yoyote ile ya matatizo yetu tunatakiwa kutanguliza imani mbele na
kumtumaini Mungu tukifuata maelekezo ya kusimama Imara na kumwachia Mungu
atuongoze na afanye kazi yake kwetu. Yeye anayafahamu maisha yetu na kila hatua
ambayo tunakanyaga. Yeye ambaye anajua idadi ya nywele zetu ; hii ndi tafakari
yetu ya leo- Amina
Emmanuel Turuka
.
No comments:
Post a Comment