May 8
Mithali 14; 1
Tafakari
ya leo tunakumbuka kiungo kikubwa sana cha familia yetu. Siku ya
kuwaenzi akina mama wote Duniani. Tukumbuke kuwa mchango wa
mama zetu na akina mama wote ni mkubwa katika makuzi ya
familia. Familia ni kielelezo cha juu kabisa cha jamii yetu.
Tukumbuke kuwa jamii ni zao la familia. kielelezo cha familia
zetu hakiwezi kukamilika kama hatutaenzi wajibu wa mama ndani
ya familia. Kama kitabu cha
mithali 11- 6 kinavyosema Mwanamke mwenye moyo wa huruma hupata
heshima, Apataye mke apata kitu chema naye ajipatia kibali kwa
BWANA;huu ni ukweli mtupu ndio maana tuna kila sababu ya kusema asante sana kwa
upendo wenu huo.
Je umuhimu wa
mama katika familia umejikita zaidi katika malezi? Jibu la swali Hilo
ni hapana. Wajibu wa mama pamoja na ukuu wao katika malezi
kwa kweli wamevuka mipaka. Ndio maana waswahili hunena kwenye
mafanikio makubwa ya mwanaume yeyote nyuma yake kuna nguvu ya
mwanamke. Kama Mtaalam mmoja aliwahi sema
kuwa pindi mtoto anapozaliwa na mama anazaliwa pia, mama hakuishi kabla;
bali mwanamke anaishi muda wote lakini mama ni kitu kipya kinachokuja baada ya
mtoto kuzaliwa;lakini ndio wajenzi wakuu wa familia Mithali 14; 1
inatutaadhalisha kuwa Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake,
bali mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake
mwenyewe.
Tafakari yetu Leo siku ya kuwashukuru
sana “ Mama” kwa jinsi wanavyojitolea katika kuhakisha kuwa kila kitu
ndani ya familia kinakwenda vizuri, kama mama ni legelege ndani ya familia na
familia itayumba tu; Ni ukweli usiopingika kuwa katika kila mafanikio makubwa
ndani ya familia nyuma yake yuko Mama; Mitahali 5-
18 inaendelea kutufundisha kuwa Chemchemi yako na ibarikiwe na ufurahie
mke wa ujana wako;
Tunamshukuru sana
Mwenyezi Mungu kwa kuwajalieni busara, upendo, ujasili na unyenyekevu ambao ni
daraja la msingi sana katika kuimarisha nyumba bora yenye upendo mkubwa. Kwa namna ya pekee leo napenda kuwakumbuka na kuwashukuru sana na nazidi
kumwomba Mungu azidi kuwajalia afya njema na amani katika maisha yenu ya kila
siku hii ya kumbukumbu yenu mmekuwa daima kiungo muhimu sana katika
maisha yetu na katika ukuaji wa familia. Hekima yenu haina mipaka, upendo wenu
hauna mipaka, msamaha wenu hauna mipaka; nasi tunaendelea kumshukuru Mungu
katika kuenzi ukuu na ujenzi wa familia zetu;
hii ndio tafakari yetu ya leo Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment