May 3
Mwanzo 19:26
Tafakari ya leo tunatafakari maisha yetu hapa dunia kwa kuangalia
zaidi lengo letu kubwa na hatima ya maisha yetu tunaielekeza wapi? Yesu kupitia
injili ya Luka 17: 28-29 Na
kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa,
walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga; lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na
kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote. Bwana wetu Yesu Kristo alituonya kuwa Mke wa Lutu
alikuwa Baridi, hajali, hana utii sio tu kwa mumeo hata kwa Mungu ndio sababu
hukumu ya mungu alishuka juu yake; Kama uilivyokuwa kwa Adam na Hawa ndivyo
ilivyokuwa na Mke wa Lutu; Aliambiwa asigeuke nyuma na akageuka nguzo ya Chumvi
kwa kupenda kuishi katika ulimwengu wa dunia na sio ulimwengu wa Kimungu.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa tulio wengi leo hii ni kama Mke
wa Lutu, hatusikii sauti ya Mungu na maelekezo yake, na kama tunaisikia basi
hatuko tayari kufuata haya maelekezo yake na tunaishia kuwa Nguzo ya chumvi
ambazo zinatemebea na hazina huhai wa kimungu. Mathayo 24:12 inatukumbusha
kuwa na kwa sababu ya kuongezeka
maasi, upendo wa wengi utapoa; Kama ilivyokuwa kwa mke wa Lutu kuwa
pamoja na kuishi na mume ambaye alikuwa akimwogopa na kufanya kazi na Mungu kwa
imani kubwa na Mungu Kuwapa zawadi ya Kuishi zaidi pale alipoamua kuwasha moto
wa kibiriti na kuiingamiza Sodoma, Mke wake alishindwa kutembea katika Mwendo
huu wa imani na kumwogopa Mungu.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa wakati huu
Sodoma ilikuwa imejaa uchafu wa kila aina; hivyo mke wa Lutu sio tu alihamia
Sodoma bali Sodoma ilihamia ndani ya Nafsi yake; alikuwa mwanamke ambaye
alipenda na kuabudu anasa ambazo zilikuwa zikifanyika Sodoma; Ndio maana
hakuweza kusikia sauti ya Mungu ambayo ilikuwa ikimwokoa katika maangamizi
alijawa na kiburi cha anasa na hivyo alishindwa kutekeleza agizo la Mungu.
Hivyo tatizo kubwa ni nini hapa? Mke wa Lutu aliupenda zaidi ulimwengu kuliko
kumpenda zaidi Mungu;
Kama ilivyo kwa mke wa Lutu hata sisi leo
tumesongwa sana na anasa za dunia hata ile damu ya yesu ambayo imetukomboa
hatuipi thamani kwani matendo yetu hayafanani na thamani ya Damu hiyo. Hata
hatufanyi majukumu yetu vile inavyotakiwa; hatuna nafasi ya kuwalea watoto wetu
katika maadili ya kimungu; muda wetu mwingi tunapotezea katika maisha ya anasa
za dunia hii; sauti ya Mungu daima inatuambia kuwa “Jiponye nafsi yako
usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani,
usije ukapotea”. Lakini hatusikii sauti hiyo na tunaendelea na maisha yetu ya
anasa za duniii hii.
Tafakari yetu leo inaendelea kutukumbusha kuwa tuache dhambi ya
kiburi ambayo ndio msingi wa dhambi nyingine zote; Tuwe wanyenyekevu tusikie
sauti ya bwana na kutekeleza maagizo yake; tukumbuke kuwa utii ni sadaka ya juu
sana, Yesu alituagiza kama tunampenda tutazishika amri zake; kutotii ni dhambi
mbaya sana; Mungu anafurahishwa na utii wetu kwake na amri, mafundisho yake
kwetu sisi kupitia Mwokozi wetu yesu kristo. Tunakumbushwa kuwa tusiwe kama Mke
wa Lutu aliyeangalia nyuma kwa kufikiri kuwa dunia hii ndio zaidi kwetu kuliko
Mungu. Tunatakiwa kuacha dhambi ya kiburi na kutekeleza utii kwa Mungu katika
kuishi maisha yetu kama yeye anavyotaka sisi tuishi;
Tafakari yetu inatutadharisha na matendo yetu
ya kuangalia Nyuma; Tumeagizwa tuangalie mbele ili tuweze kufuzu kuingia katika
nyumba ya Mungu; lakini kwa kuangalia nyuma kama mke wa Lutu tunakuwa
tumejiondoa wenyewe katika kushiriki utukufu wa Mungu; tukisoma Luka 9: 61-62
Mtu mwingine pia akamwambia, Bwana, nitakufuata; lakini, nipe ruhusa kwanza
nikawaage watu wa nyumbani mwangu. Yesu akamwambia, Mtu
aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu.
Hatutakiwi kabisa kuangalia nyuma tunapoutafuta ufalme wa Mungu; Kuangalia
nyuma hapa maana yake ni nini? Tunayaangalia maisha yale ya zamani, ya ulevi,
uzinzi, uwongo, wizi, chuki, na kadhalika; tukumbuke kuwa hakuna maisha ya
baadae bila mipango hiyo kupokea maelekezo ya Mungu ndani ya Nyoyo zetu. Agizo
ambalo tunapata leo hatutakiw kugeuka nyuma na kuyarudia maisha yaliyojaa
dhambi. Tumepata Baraka ya kukombolewa na damu ya Yesu jukumu letu sasa ni
kusonga mbele na kamwe kuto geuka Nyuma.
Hii ndio tafakari yetu ya leo;
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment