May 23
Mathayo 6: 25-34
Tafakari ya leo
tujikumbushe mahubiri ya Yesu alipowahutubia watu zaidi ya 5000 mlimani;
Mwinjili Mathayo anaelezea mafundisho ya Yesu akizungumzia zaidi kuhusu
Umasikini, Utajiri na Mamlaka. Yesu anatuonyesha kuwa yeye alikuwa kiongozi
ambaye alikuwa anajali haki sawa kwa wote; ambaye alikuwa na mawazo ya kiuchumi
na ambaye alikuwa hapendi matabaka katika jamii; hasa pale masikini
wanapoonewa. Yesu alijidhihirisha kuwa yeye ni mkombozi wa wote; kwani alijua
kuwa watu masikini katika jamii wako nasi siku zote; yesu aliona tatizo la
tabaka ambalo lilikuwa likiendelea kukua miongoni mwa jamii kati ya walicho
nacho na wale ambao walikuwa hawana yaani masikini. Na yesu alionyesha wazi
kabisa kuwa anawachukia wanafiki; Yesu ameonyesha sana kuchukizwa na wale ambao
wanawadhulumu wengine hasa wanyonge;
ambao wanawatumia masikini katika kujitajirisha; Yeasu mafundisho yake
ni ya Haki kwani anapenda kuhubiri haki na kuishi haki;
Tafakari yetu leo inaonyesha
msimamo wa Yesu kuwa anataka sisi tuwe
na furaha siku zote lakini furaha yetu ijengwe katika misingi ya haki; kama
tunavyosoma katika kitabu cha zaburi 144:15 Bwana, ni nani atakayekaa Katika hema yako? Ni
nani atakayefanya maskani yake Katika kilima chako kitakatifu? Ni mtu aendaye kwa ukamilifu, Na kutenda haki. Asemaye kweli
kwa moyo wake, Asiyesingizia kwa ulimi wake. Wala hakumtenda mwenziwe
mabaya, Wala hakumsengenya jirani yake. Machoni pake mtu asiyefaa hudharauliwa, Bali huwaheshimu
wamchao Bwana Ingawa ameapa kwa hasara yake, Hayabadili maneno yake. Hakutoa fedha yake apate kula riba, Hakutwaa rushwa
amwangamize asiye na hatia. Mtu atendaye mambo hayo Hataondoshwa milele.
Hivi ndivyo sisi tunafapaswa kuwa na kwa umasikini huu war oho ni utajiri
mkubwa sana mbele ya mwenyezi Mungu;
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Mungu anataka kutubariki sisi lakini ila Baraka
zake zikae juu yetu lazima tuwe masinikini war oho; watu ambao tuko tayari
kufuata maelekezo ya Mungu. Ili kupata furaha ya ndani kabisa ya Kimungu lazima
tujiepushe na makando kando; furaha yetu daima iongozwe na miongozo ya Mungu na
sio mambo ya kidunia; Mafundisho ya Yesu Mlimani ni kielelezo cha wazi kuwa ili
uwe masikini wa roho na tajiri wa mbinguni watakiwa kufanya nini. Tuzikumbuke
zile HERI; kwa mafundisho ya yesu mlimani
Heri ni kunyume cha yale dunia inachofanya ili kuitafuta furaha. Na Bahati
mbaya furaha hiyo ya dunia ni ya muda mfupi tu; Yesu hakusema heri matajiri
lakini yeye alisema heri masikini, heri wanaolia. Heri wanaodhulumiwa, heri
wanyenyekevu,heri wenye njaa ya haki; hawa wote ambao wanaombewa heri hizi ni
watu ambao ni wanyonge hawana sauti katika mamalaka ya dunia hii na
wamekandamizwa na hawawezi kufurahia utukufu wa Mungu japo wanatamani kwa
sababu ya dhuluma na nguvu ya giza ambayo imekandamiza; Lakini kwa mafundisho
ya yesu Mlimani anawafungua na kuwaondoa gizani na kuwapa nuru mpya ya
kufurahia maisha ya yenye utukufu wa Mungu kwani ni masikini wa roho lakini ni matajiri
katika ufalme wa Mungu.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa daima sisi
wanadamu hata wale watumishi wa Mungu ambao wanadhani tayari ni masikini wa
roho daima wanabadilisha na ulimwengu; wanaingia katika tama za kiulimwengu na
katika tabia za kiulimwengu; na rahisi sana kubadilishwa tabia zetu kupitia matumizi
ya tekinoloji; muziki, tvs; sinema, mitandao ya kijamii ambayo kwa haraka tu
hukutoa kutoka katika maisha ya umasikini wa Kiroho na kukupeleka katika maisha
ya Kilimwengu; lazima tutambue kuwa furaha ya kweli hutoka kwa Mungu kwa kufuata
maagizo kupitia maandiko matakatifu; hivyo Mbinguni ni kielezo cha furaha;
kielelezo cha neema na furaha na neema hiyo itadumu milele na hiyo ndio faida
ya kuwa masikini wa Roho; Wokovu ambao tumepewa kupitia Msalaba ni kielelzo cha
furaha kubwa kwa masikini war oho lakini ili kufurahia wokovu huu ni lazima tutimize
kwa vitendo mahubiri ya Yesu Mlimani;
Tafakari ya leo inataka wewe na mimi tujiulize
katika zile kheri tunazitimizaje: je Tunazitimiza kwa vitendo au kwa maneno?
Hii ndio tafakari yetu ya Leo:
No comments:
Post a Comment