WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Tuesday, March 8, 2016

WEMA WA MUNGU KATIKA MAISHA YETU




March 8

Zaburi ya 119:68

Tafakari ya leo tunaangalia wa Mungu katika Maisha yetu; zaburi ya 119:68 wewe ni mwema na mtenda mema nifundishe amri zako. Hapa tunaona kabisa kuwa kwa asili Mungu ni Mwema sana katika kila upande tunaougusa katika msiaha yetu. Tukisoma Injili ya Marko 10:18  Yesu akawaambia, kw nini kuniita mwema? Hakunaaliye mwema ila mmoja ndiye Mungu. Na tunapotafsiri uzuri wa mungu pia tunaangalia Matendo; matendo ya Mungu yameajaa; Wema; Huruma; pendo lisilo kauka; ukarimu wa khali ya juu na daima hutupa sisi vyote tuviombavyo bila kinyongo.

Tafakari ya leo inatukumbusha je tumeweza kufukiria njinsi Mungu alivyo mwema kwetu pamoja na mizogo yetu yoye, matatizo yetu bado Mungu amekuwa mwema sana kwetu; kwani anasema kuwa pamoja na shida na kiburi chenu bado nataka nitawashushia Baraka ambazo zitatupa sisi furaha  sio kwa sababu tunastahili la hasha bali kwa sababu ya wema wangu. Ni kweli kuwa Mungu ni kwa ajili yetu. Yeye ndiye muhimili wa upendo wetu kwa asababu ya utakatifu wake na wema wake kwetu.

Hebu tuangalie zaburi ya 145: 9 Bwana ni mwema kwa watu wote, na rehema zake zi juu ya kazi zake zote. Hivyo jukumu letu ni kumuhimidia  yeye na kulisifu jina lake. Hivyo ni wajibu wetu kuonya jinsi bwana alivyo mwema. Sisi binadamu wote katika maisha yetu hapa dunia au tumepotea kwa dhambi zetu na kuwa mbali na Mungu au tumeokolewa kutokana na dhambi kwa msaama wa upendo wa Mungu kupiti Damu ya bwana wetu Yesu Kristo.
Tukisoma waraka wa Mtume wa Paulo kwa Warumi 2:4 Au waudharau wingi wa wema wake na ustahili wake na uvumilivu wake; usije ya kuwa wema wa Mungu wauvuta upate kutubu? Daima sisi wanadamu tunajiona kuwa tuko sahihi kwa matendo yetu ukweli ambao sio kama Mtume Paulo anavyotukumbusha Roman 1:18 kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanandamu waipingaokweli kwa uovu. Kwa kuwa mambo ya mungu yajulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia.
Tafakari ya leo Tunataadhirishwa kuwa pamoja na wema wote wa Mungu lakini anatuacha katika tama za mioyo yetu, tufuate uchafu, hata tukavunjiana heshima miili yetu. Anatuacha tuendelee na jeuri yetu , kiburi chetu, majivuno yetu, uongo na hata pale ambapo hatuwatii wazazi wetu.  Mungu anatuangalia tu bali wema wake uko palepale kama tuko tayari kumpokea na kufuata taratibu ambazo anataka sisi tufuate. Mungu daima huwaadhibu wakosefu lakini mara nyingi hukumu yake ya adhabu uchelewa ili wakosefu wapte kutubu; ama kweli Mungu ni mwema sana kwetu. Lakini tujue kuwa hakuna upendeleo yeye hutupa sisi nafasi zaidi ya kujirekebisha kupitia toba.
Tafakari ya leo pia inaendelea kutuonyesha wema wa Mungu kwetu,  hata alipotuandalia Bustani ya Adeni alijua kuwa mwanadamu atamgeuka lakini kwa wema wake hauacha kutekeleza mipango yake. Alijua kabisa Hawa atadanganywa na Nyoka naye atamdanganya Adamu na hatimaye Adamu atavunja agano lake na Mungu kwa dhambi ili kiburi cha kuto tii amri ya Mungu. Na mungu alijua maumivu yote ambayo yatatokana na dhambi hii ya Adamu na Hawa. Tunajifunza hapa kuwa bado Mungu ameendelea kuonyesha wema wake kwetu pamoja na kumchukia kwa dhambi zetu.
Pamoja na kuyaona haya kabla ya Kumuumba binadamu kwa wema wake alimuumba mwanadamu pamoja na usaliti wote ambao atafanya. Katika matendo yetu yote ambayo mengi yanamkasirisha Mungu wetu kama kitabu cha Kutoka 34.6-7 Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenyekumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenyekuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana waopia, hata kizazi cha tatu na cha nne.

Tafakari ya leo ina umuhimu mkubwa sana kwetu kwani inatufundisha kuwa Mungu kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; na ameweka hiyo milele ndani ya mioyo yao. Ndio maana mioyo yetu daima inakuwa katika mahangaiko mpaka pale inapata faraja ya Mungu kupiti wema wake ambao tunaupata kwa njia ya kitubio. Kwa hiyo tukiacha uovu wetu na kutenda yaliyo halali na haki tutaziponya roho zetu  na zitakuwa hai bali tukifanya machukizo yatokanayo na dhambi na kuto tubu, tutakufa na uovu wetu hapo tusitegemee wema wa Mungu. Yatupasa  tutupilie mbali kabisa makosa yetu, na tujifanyie moyo mpya ili kufurahia wema wa mungu.

Hii ni tafakari yetu ya leo. Amina




No comments:

Post a Comment