WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Thursday, March 3, 2016

AMBAYE HANA DHAMBI AWE WA KWANZA KURUSHA JIWE;


March 3

John 8:7

Tafakari ya leo tunaomba ujiulize kwa nini unabeba Jiwe mkononi mwako? Je jiwe ambalo umelibeba katika mkono wako unataka kulitumia vipi na utakuwa wa kwanza kulirusha?

Yesu aliwaambia wakuu wa mafarisayo na walimu washeria na kundi la watu ambao walikuwa wamemfumania mwanamke akiwa katika uzinzi kuwa yeyote anayejiona hana dhambi awe wa kwanza kumrushia mwanamke huyu Jiwe. Walijitafakari wao wenyewe na wakajitambua kuwa walikosa usafi wa moyo na waliondoka na kumwacha mwanamke Yule peke yake.

Injili hii ya Yohana inatukumbusha jinsi ambavyo tunatakiwa kuwa makini tunapokuwa tayari kuhukumu kwa mapokeo au sheria ambazo zinahusiana na weledi wa Mungu. Tunatakiwa tutambue kuwa dunia au umati wa watu wakati wote unakuja na hukumu ambayo wakati mwingine sio ya haki Kama Mafarisayo wote tuna hatia ya kusema mapungufu ya wengine wakati kupuuza mapungufu ya watu wengine. Tunaona katika hadithi hii jinsi watu walivyokuwa na hasira; hiki ni kielezo kizuri cha dunia na tuishiokubwa katika kutekeleza maagizo ya  kuisha kama mkristo bora

Tafakari ya leo inataka kutonyesha kuwa tunatakiwa kujisafisha kwanza wenyewe kabla ya kuwahukumu wengine; vile vile  tuzingatie kuwa sisi kuhukumu sio kazi yetu Mungu mwenyewe ndiye mwenye mamlaka ya kutoa hukumu; tulishaonywa tusihukumu ili nasi tusijehukumiwa. Tumepoteza uaminifu kwa matendo yetu daima yanaelekea katika  kunyosheana mikono, na kubeba mawe mikononi mwetu kwa ajili ya kuwaadhibu wengine jambo ambalo sio sahihi. Mathayo 7: 1-4 msihukumu, msije mkahukumiwa. Kwa kuwa hukumuile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa. Basi mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndaniya jicho lako; na kumbe Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?

Tafakari ya leo inaasa jamii yetu kuto kuwa miongoni mwa kundi hili la watu wenye hasira ambao wamebeba mawe ya  chuki, kisasi, hasira, mafarakano na kio ya kufanya maovu. Tunachukua matendo haya maovu katika mioyo yetu na kasha kuwanyoshea vidole watu wengine na tayari kuwahukumu na kuwapa adhabu kwa mawe yetu, jambo ambalo sio sahahi mbele ya macho ya Bwana. James 4:11 Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake au kumhukumu ndugu yake, huisingizia shera na kuihukumu sherai. Lakini ukiihukumu sheria,huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu.

Yesu anatuonyesha mfano mzuri, sio kuwa Yule mwanamke hakufanya dhambi la hasha alifanya dhambi, lakini hukumu aliyokuwa akikabiliana nayo ilikuwa inatakiwa kutolewa na watu ambao walikuwa na mapungufu katika taratibu za utekelezaji wa adhabu hiyo, walimleta mtuhimiwa mmoja na sio wote wawili; hivyo yatupasa kuwa makini katika utoaji wa hukumu kwa wengine. Romani 14:12 Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu. Usimkwaze Mwingine.

Tafakari ya leo Bwana wetu yesu kristo anatuonyesha kuwa tunatakiwa tubebe mawe ya upendo, huruma kwa yatima na wagonjwa, mawe ya maelewano, mawe ya kujitolea kwa ajili ya ufalme wa Mungu; mawe yetu yawe yale yanayojenga sio yanayoangamiza; Mawe yetu yawe sio ya Kuhukumu yawe ya kufariji na kufundisha na kuonyesha kasoro ambazo jirani yako anapata nafasi ya kujirekebisha ili naye aweze kufurahia utukufu wa Mungu. Yesu ametuonyesha mfano mzuri sana kwani Mwanamke alikuwa na kosa nay eye amekiri na Bwana wetu Yesu Kristo alimpa nafasi ya kubadilika ili asitende tena hilo kosa.
Tafakari ya leo ni wakati mzuri wa kujitathimini sisi wenyewe juu ya matendo yetu ambayo  kama je sisi ni bora kuliko wale ambao tunataka kuwa tupia mawe?

Tunachoendelea kujifunza katika hadithi hii sio kuwa Yesu alipuuza dhambi  lakini injili haitufundishi kuwa kwa kuwatumia watu wengine kama jiwe la kurukia wanazidi ni kumkashifu Mungu Mtakatifu.  Dhambi  inakera zaidi ilivyoelezwa katika hadithi hii si tu uasherati;  bali hapa tunajifunza tatizo la kiburi, na ujinga wa Mafarisayo kutumia dhambi, ya mtu mwingine kwa faida binafsi wakati kupuuza dhambi ambayo ipo ndani ya nafsi yao wenyewe .

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa; Wewe ni nani kuniita mimi mwenye dhambi? Hivyo usirushe jiwe kwangu isipokuwa tu kama huna dhambi;Mtazamo yaliyotolewa na maelezo ya hapo juu kabisa inakosa jambo katika hadithi hii. mwanamke katika hadithi alikuwa na hatia. Hata walipomwacha mwanamke peke yake hakukumpunguzia yule mwananmke kosa lake la kitendo cha kuzini; lakini sheria pia ilitoa njia ya msamaha. Biblia ina mifano ya wenye dhambi waliotubu na kupokea msamaha; kwa mfano Mfalme Daudi alikuwa mkosefu ambaye alipata msamaha wa Mungu kama mwanamke mzinzi alivyopata msamaha kwa Yesu.

Tafadhali kumbuka kuwa Yesu anawaambia mwanamke kuacha kutenda dhambi na kutembea katika mwanga wake. Hata kama mwanamke yule alitenda dhambi kwa sababu ya ugumu wa maisha yake binafsi au yaliyotoka na mume wake lakini Yesu alimwambie asitende dhambi tena. La msingi Yesu alimtambua Mwanamke kuwa ni mwenye dhambi na alimsamaha zambi zake.

Tafakari ya leo tunachojifunza hapa ni kuwa mwitikio wetu kwa dhambi lazima kukubali hali yetu ya dhambi mbele ya Mungu Mtakatifu . Biblia ni wazi juu ya hatua hii. Wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu (Rum. 3:23). Pili tunajifunza kwamba tunapaswa kutambua matokeo kwamba dhambi ni uharibifu. Baadhi jaribio la kuwasilisha dhambi kama hakuna mpango mkubwa.

Hiyo ni hatua ya mafundisho ya Yesu katika somo letu leo. Tukumbuke kuwa hakuna hata mmoja  ambaye ni kamili na tunapaswa kukumbuka kwamba wakati tunataka kunyoosha vidole au kutupa mawe kwa mtu mwingine kuna jiwe nyingine ambalo linaelekezwa kwako tusiwe na tabia ya kupenda kuwahukumu wenzetu kwa makosa yao wakati hata sisi tuna mapungufu yetu tena mengi tu. Hii ni tafakari ya leo tuifanyie kazi AMINA



Emmanuel Turuka                

No comments:

Post a Comment