March 21
Wafilipi 3:13,14
Tafakari ya leo tunaangalia kazi kubwa ya Kamera ambayo ni kupiga picha
mbali mbali, ili kuweze kupata picha nzuri mpiga anatakiwa kuwa makini kwa
kulenga vizuri (focus) ili kuondoa vivuli ambavyo vinasababisha picha kuto kuwa
nzuri; hii inaonyesha umuhimu wa kuweke mtazamo wake juu ya nini anatakiwa afanye kuweza kupata
picha nzuri. Maisha yetu ya Kiroho ni sawa na Matumizi ya kamera ni muhimu sana
tunavyotekeleza maisha yetu ya Kiroho kuhakikisha wewe ni kulenga jambo sahihi.
Lazima tukubali kuwa tunaishi katika wakati ambao kuna vitu vingi ambavyo
vinaendelea katika maisha yetu na vinatutoa katika mwelekeo sahihi wa kuishi
kama wakristo.
Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa katika maisha yetu ya kila siku, tumekuwa
watu ambao tumejawa na wasiwasi na kusumbukiaa kwa mambo mengi ambayo sio muhimu,
na tumesahau kuzingatia au kulenga zaidi katika maisha tunayotakiwa kuishi ya
kumtumikia Yesu, Mwenyezi Mungu anataka sisi kuzingatia/kulenga (focus) zaidi katika dhumuni hasa la maisha yetu hapa
duniani; Tukumbuke kuwa maisha yetu daima yanalinganishwa na Kamera ili iweze
kutoa picha nzuri inahitaji umakini; Je
tunajua kwa nini Mungu anataka sisi kuzingatia Maisha yetu? Jibu ni rahisi sana kwa sababu Maisha yetu ni
kama kamera; ili kufaninikisha lazima tujipange vizuri; katika upigaji, eneo la
kupigia picha, khali ya hewa; na mwelekeo wa mpiga picha.Hivyo maisha yetu tunatakiwa uchaguzi mzuri katika kila hatua ambayo tunayoishi kwa utukufu wa
Mungu .
Tafakari yetu katka Juma hili kuu inaendelea kutukumbusha kwamba katika
kila jambo lolote tunalofanya tufanye mambo mazuri ambayo kuongeza thamani
chanya kwa maisha yetu; Mambo mema yataongeza kumbukumbu zetu nzuri na uzoefu
chanya; kwa kuzingatia nini ni muhimu tukichambua
kama kamera inavyofanya kazi na kutoa picha nzuri. Sisi tunatakiwa tumlenge
Yesu uli tuweze kupata picha yetu nzuri, hata pale tunapo patwa na ugumu wa
maisha,na shida mbali mbali katika maisha yetu bado tunatakiwa tuondoe hivyo
vivuli ili bado iwe kwa yesu. Hatutakiwi tuondoe focus yetu kwa Yesu eti kwa
sababu tu ya Maumivu ambayo tumeyapata
katika maumivu yetu;
Zaburi 1:1 Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la
wasio haki, wala hakusimama katika njia ya wakosaji; wala hakuketi barazani pa
wenye mizaha. Daima sisi tunaishia kuchukua picha mbaya kwa vile hatuko tayari
kuzingatia taratibu nzuri za kupiga picha. Lazima tukubali kufuata utaratibu
ambao kristo anataka sisi tufuate tunapopiga picha za kiroho; tukifanya hivyo
tutaweza kutimiza kutimiza furaha
yake ni katika sheria ya Bwana, na juu ya sheria sisi yatupasa kuitafakari
mchana na usiku.
Tafakari yetu inaendelea kutukumbusha kuwa mkazo/mlengo/Focus itukumbushe
kwamba hatupaswi kuendesha maisha yetu kulingana na maoni au mifano ya marafiki
zetu. Tunajua hivi sasa dunia yetu iko katika kipindi ambacho kila kitu cha
kibinadamu vinakwenda kwa speed ya haraka sana na tunajiona kuwa sisi ndio
wamiliki wa dunia hii na tunaweza kufanya chochote tukipendacho bila msaada wa Mungu. Kama Warumi 12: 1 Basi hivyo, ndugu na zangu , nawasihi kwa huruma zake itoeni miili yenu iwe
dhabibu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye
Maana. Luka 9:23 Akawaambia wote, yeyote akitaka kunifuata, na ajikane
mwenyewe, ajitwike msalaba wake anifuate, hii inatufundisha kuwa kama
tutamtanguliza Yesu Mbele ya maisha yetu na tutayatoa maisha yetu kwa ajili ya
ufalme wa mungu tutapata Picha nzuri sana katika maisha yetu ya hapa duniani na
hata mbinguni. Tunatakiwa kujitoa kabisa kwa Mungu na kutenda haki kwa utukufu wa Mungu.
Tafakari ya leo inatuelekeza katika
ukamilifu wa kweli tunapojiandaa kutumia maisha yetu kama kamera katika maisha
yetu ya Kiroho; Tunatakiwa kuendelea kujitathimini sisi wenyewe, kuiangalia
taswira ya Picha katika kamera kabla ya kuipiga kwa kuangalia kila upande na
kila kona hata kuikuza ili kupata taswira halisi kabla ya kukamilisha kitendo
cha kupiga picha. Kabla ya kupiga picha tunatakiwa kurekebisha taswira kwa
kujiuliza maswali yafuatayo; Je uhusiano wangu na Mungu Ukoje? Je uhusiano na
familia yangu pia ukoje? Je uhusiano wangu Kazini ukoje? Je natimiza mwito wa
Mungu kama alivyonielekeza kufanya? Je nina mheshimu Mungu pamoja na amri zake?
Je nimeweza kufanya kazi yeyote ambayo imekuwa na matunda ya kiroho katika
Jamii yangu na kwangu Mwenyewe?
Hii ndio Tafakari yetu ya leo ; kama tutajibu maswali hayo inavyopasa basi
matumizi ya kamera ayetu ni ya kuigiwa mfano na Mwenyezi Mungu atakujalia
maisha mazuri sana na hata baadae Mbinguni.
Amen
Emmanuel Turuka
(life is like Camera)
No comments:
Post a Comment