March 4
1 PETRO 5: 6
Tafakari ya leo
tunaangalia mkono wa Mungu na kazi yake kwetu; Mkono wa Mungu unaleta
unyenyekevu kwetu; Mungu anatumia namna mbali mbali za kutuletea na kutuonyesha
sisi unyenyekevu wake; kuna wakati anawatumia watu wengine katika kutuletea unyenyekevu
ambao Mungu anataka sisi tuwe nao. Wakati mwingine anatuletea maafa katika
maisha yetu na mali zetu hata pale tunapopoteza wapendwa wetu lakini lengo lake
ni kutufundisha jinsi gani tunaweza kuwa wanyenyekevu mbele yake na mbele ya
watu wengine. Kama tunavyosoma kutoka kwa Waroma 8: 28 Nasi twajua kuwa katika mambo
yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale
wampendao katika kuwapatia mema, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake.
Tafakari ya leo
inatumbusha kuwa kuishi kwa enyenyekevu sio jambo rahisi, ni kuwa tayari
kukubali kuwa Mungu ndiye mwenye mamlaka na maisha yako, yeye ndiye ayaendeshae
maisha yako. Jambo ambalo mara nyingi hatutaki kukubali au kulifuata. Sisi tunataka
tuishi maisha ya kujitawala wenyewe na kufanya mambo yetu vile ambavyo tunataka
iwe. Unyenyekevu unatukumbusha kuwa tunakuwa tayari kukubali kuwa kila
kinachotokea katika maisha yetu kimepata kibali cha Mungu. Na hivyo tunatakiwa
kushukuru na kukubaliana na matokeo hayo bila kulalamika hata kama matokeo yake
yanaumiza na ni vigumu kuyakubali na
wala Mungu hatupi sisi maelezo yeyote yale.
Ugumu wa kuishi kwa
unyenyekevu ni kushindwa kwetu kujishusha, asili yetu binadamu tunataka
kujikweza, tunataka kuonekana; tunapenda
kujulikana; kuheshimiwa na kuogopwa. Ndio maana ni neema
ya hali ya juu kwa wale wote ambao ni wanyenyekevu na wanaisha maisha ya
unyenyekevu.
Tafakari yetu ya leo
inatuonyesha kuwa sifa nyingine ya mtu
Mnyenyekevu ni kuwa mtegemea neema ya Mungu , Baraka na nguvu za Mungu kwa
mahitaji na shida zake zote. Mtu ambaye sio mnyenyekevu huwa na kiburi,
majivuno hayuko tayari kusubiri Baraka za Mungu katika maisha yake, kwani kwake
Mungu sio chochote; yeye anaweza kufanya ka kujitosheleza katika haja zake. Lakini
Zaburi ya 55.22 umtwike bwana mzigo wako naye atakutegemeza, hatamwacha mwenye
haki aondoshwe milele. Tunatakiwa kumpa bwana mizigo yote ambayo tunayo na yeye
ataibeba kwa ajili yetu, hata amuru wewe utabike.
Unyenyekevu ni kielezo cha
sisi kuona tuna mapungufu yetu, hivyo kutengeneza utegemezi wetu na kuomba au
kutegemea nguvu za Mungu katika kupata mafanikio ambayo tunayo yahitaji. Hivyo
madhaifu yetu ni sehemu ya mpango wa Mungu ili kutonyesha sisi yeye pekee ndio
kimbilio letu lakini twatakiwa kuwa wanyenyekevu mbele ya Mungu ili uwepo wa
Mungu ufanye kazi ndani yetu. Kwa hiyo palipo na Mungu na unyenyekevu upo pia,
na unyenyekevu unatemebea katika uwepo
wa Mungu.
1
Peter 5 hivyo hivyo ninyi vijana watiini wazee. Naam ninyi nyote jifungeni
unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu mungu huwapinga wenye kiburi, lakini
huwapa wanyenyekevu neema. Tunatakiwa kuwa wanyenyekevu ili tupate neema ya
Mungu.
Bali tusipokuwa hivyo na tukaleta kiburi chetu Mungu atakuwa
kinyume chetu, lakini tukiwa wanyeynyekevu Tutapewa neema kwa wakati muafaka na
Mungu atatimiza haja za mahitaji yetu na hatupaswi kuwa na mashaka.
Hosea 13: 4-6 Lakini mimi ni Bwana Mungu wako tangu Misri;
wala hutamjua Mungu mwingine ila mimi; wala zaidi ya mimi hakuna Mwokozi. Mimi
nilikuja katika jangwa katika nchi yenye kiu nyingi. Kwa kadiri ya malisho yao,
kwa kadiri iyo hiyo walishiba; walishiba
na moyo wao ukatukuka: ndiyo sababu wamenisahau mimi.
Tafakari yetu inatuonyesha Jinsi Musa alivyowaonya watu wa
Mungu tukisoma kutoka 8: 11-17 kuhusu nini kitatokea watakapo kuwa wametulia
katika nchi ya ahadi: jihadharini, usije ukamsahau Bwana, Mungu wako kwa
kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake ninazokuamuru leo. Angalia
utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake.
Na makundi yako ya ngombe na kondoo yatakapoongezeka, na
fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu ulicho nacho kitakapoongezeka;
basi hapo moyo wako usiinuke ukamsahau
Bwana, Mungu wako aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa;
aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na
nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji; aliyokutolea maji katika mwamba mgumu. Aliyekulisha
jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili
kukutendea mema mwisho wako. Hapo usiseme moyoni mwako, nguvu zangu na uwezo wa
mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo.
Yeramia 13: 9-10 jinsi hii nitakiharibu kiburi cha
yuda na kiburi kikuu cha yerusalem. Watu hawa waovu wanaokataa kusikilizamaneno
yangu, wanaokwenda kwa ushupavu wa mioyoyao, na kufuata miungu mingine ili
kuitumikia na kuiabudu, watakuwa hali moja na mshipi huu, usiofaa kwa lolote.
Tafakari yetu inatufundisha
kuwa watu wanyenyekevu hawataki makuu; hawapendi kujikweza kwani wanajua Mungu
atawekweza tu. Bali wasio wanyenyekevu wao hupenda kuonekana kama Mathew 23:6
inavyotufundisha; hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika
masinagogi.
Tafakari ya leo
inatuonyesha kuwa Mungu anapenda sisi wenyewe tumpe shida zetu, japo yeye
anazijua lakini anataka sisi tuonyeshe unyenyekevu wetu kwake. Tukumbuke kuwa
unenyekevu ni neema kutoka kwa Mungu; na kila kitu ambacho tunacho ni zawadi
pia toka kwa Mungu, uwezo ,mafanikio vipawa vyote tumepewa kama zawadi. Hivyo vyote
ambavyo tumepata angeweza pewa mtu mwingine. Je unaitumiaje zawadi yako kwa
manufaa ya Mungu.
1 Peter 5: 8-9 Tunatakiwa kumpelekea shida zetu mungu lakini
wakati huo huo kuwa makini na hila za shetani. Huku mkimtwika yeye fadhaa zenu
zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. Nanyi mpigenihuyo,
mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa
ndugu zenu walioko duniani.
Tukumbuke kuwa kila mmoja wetu ana mapungufu yake, inaweza
kuwa sehemu ya tabia mbaya, vishawishi
hivyo shetani naye anatumia mapungufu yetu katika kuondoa unyenyekevu wetu kwa
mungu kwani atatujengea kiburi na tutajiona kuwa hatuhitaji nguvu ya Mungu katika
maisha yetu yatupasa kuwa makini. Hii ni tafakari yetu ya leo –Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment