March 22,
Yohana 19:10 – 11
Tafakari ya Leo
tunaangalia jinsi Yesu alivyokuwa akiheshimu mamlaka ya dunia ni kweli kwamba
Utekelezaji wa sheria za kidunia ni
udhihirisho unaonekana wazi kuwa Mamlaka yao yanatoka kwa Mungu. Jukumu
la viongozi wa dunia ni kuwapa watu haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru
, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima upendo. Mathayo
22:21 Akawaambia Basi mlipeni Kaisari yaliyo ya
Kaisari na Mungu yaliyo ya Mungu. Yesu aliheshimu Mamlaka ya dunia na alikuwa akiikosoa pale
ilipokuwa ikikosea.
Tafakari inatuonyesha kuwa kwa upande mwingine hakuna mamlaka
isiyotoka kwa Mungu; na wale ambao hutumikia serikali hizo wamepata kibali cha
kuongoza toka kwa Mungu japo wakati mwingi hutenda kinyume na maelekezo ya
Mungu kwa ustawi wa jamii husika. Anayepinga mamlaka ya serikali ya kidunia
anakiuka agizo la Mungu. Sheria inatusaidia kufanya yaliyo mema; Watawala ni
watumishi wa Mungu , kujitoa wenyewe kwa utawala wa sheria; Mamlaka ni haki
halali ya kutekeleza utii. Ni nguvu ya kushawishi au tabia amri. Wagalatia 5:
22-23 Lakini tunda la Roho ni upendo,
furaha , amani, uvumilivu , wema, fadhili , uaminifu, upole na kujizuia. Juu ya
mambo kama hayo hakuna sheria.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Warumi 13:4 kwa kuwa yeye ni
mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema.
Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni
mtumishi wa bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda
mabaya kwa ajili ya ghadhabu. Mungu
ndiye mwenye mamlaka ya mwisho, na Mungu anatumia serikali za watu wenye
mamlaka kwa kusudi lake na letu pia. Biblia inatufundisha kwamba serikali zisizo
hudumia watu na kutimiza lengo ambalo Mungu amekusudia Mungu huziondoa.Waebrania 13:17 Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana
wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba
watu wafanye hivyo kwa furaha wala si
kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.
Warumi 13: 1 Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna
mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye
mwenye Mamlaka hushindana na agizo la mungu; nao washindanao watajipatia hukumu.
Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa
sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya.basi wataka
usimwogope mwenye mamlka? Fanya mema nawe utapata sifa kwake. Kwa sababu hiyo
tena mwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo
hiyo.
Tafakari
ya leo inaendelea kutubaanisha kuwa, Mithali 29:18 Pasipo maono watu huacha
kujizuia, Bali ana heri mtu Yule ashikaye sheria. Taifa bila nguvu ya Mungu
halina baki shagala bagala halifuati sheria. Heri wale wafuatao sheria. Mhubiri 10:17 Heri kwako, nchi mfalame wako akiwa motto wa
watu, na wakuu wako hula wakati ufaao, ili makusudi wapate nguvu wala si kwa
ajili ya ulevi. 28:2
Viongozi Mithali 11:14
Pasipo Mshauri mzuri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri hujawokovu;
mfalme awahukumuye maskini kwa uaminifu; kit chakecha enzi kitathibitika
milele. Mfalme huithibitisha nchi kwa
hukumu; bali yeye apokeaye rushwa huipindua. Yesu alipopelekwa mbele ya Pilato
Yohana 19: 10 – 11 Basi Pilato akamwambia husemi name? hujui ya kuwa mimi nina
mamlaka ya kukufungua, name nina mamlaka ya kukusulubisha? Yesu akamjibu, wewe
hungekuwa na mamlaka yoyote juu yangu kama usingepewa kutoka juu; kwa hiyo yeye
aliyenitia mikononi mwako ana dhambi iliyo kubwa zaidi. Yesu hapa anaendelea
kutonyesha kuwa mamlaka zote za dunia zinatoka kwa Mungu.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa
Mamlaka ya Pilato juu ya Yesu bado ilikuwa chini ya Nguvu ya Mungu ambaye
alibariki hukumu ya Yesu Kufa Msalabani kupitia mamlaka ya dunia hii kupitia
Pilato. Ili Yesu aweze kukamilisha kazi yake ya ukombozi wa Wanadamu ambao
walikuwa wamezama katika dimbwi la dhambi; Yesu alipata faraja yake katika
wakati huu si kwa sababu ni mapenzi ya Mungu yaliyotimia ndani ya Uongozi wa
Pilato; hivyo tunachojifunza hapa ni kuwa Yesu hakuwa na wasiwasi katika mikono
ya hofu Pilato , kwani alijua kuwa Pilato alikuwa katika mikono ya Baba Yesu. Kama 1 Peter 2: 13-17
Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya bwana; ikiwa ni mfalme, kama
mwenye cheo kikubwa. Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni mungu. Mpeni
heshima mfalme. Mfano wa kuteswa kwa Yesu.
Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa tusifadhaike na watawala
ambao wanaweza kuua miili yetu lakini hawana nguvu ya kuua roho zetu, uwezo
ambao wamepewa na Mungu unamipaka yake kwa ustawi wetu kama 2 Mambo ya Nyakati
7:14 ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu watanyinyenyekesha, na kuomba na
kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi nitaskikia toka mbinguni na
kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Pilato ana mamlaka; Herode ana mamlaka; Askari wana mamlaka; Shetani ana mamlaka; Lakini hakuna hata mmoja wao
ambaye anamamlaka yanayojitegemea yote wamepewa na Mungu hivyo hatuna sababu ya
kuogopa kwani mamalaka yao kwa wao wenyewe hayana nguvu; na Mungu kamwe
hatawapa nguvu za kutuangamiza sisi; Hivyo nasema tena hatutakiwi Kuogopa; tumshukuru Mungu kwa kutupa sisi
thamani kubwa kuliko yeyote lakini inatakiwa tutimize wajibu wetu;
Hii ni tafakari yetu ya leo Nawatakie maandalizi Mema ya Juma kuu kuelekea
sikukuu ya Pasaka Siku muhimu katika wokovu wetu Amen
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment