March
2
JOSHUA 24: 14 -15
Tafakari ya leo
tunaangalie ujumbe huu mzito toka kwa
Mtumishi Joshua katika huu ujumbe huu mzito, kuwa yeye na nyumba yake,
watamtumikia Bwana. Tukumbuke kuwa Joshua mwana wa Nuni alikuwa amejaa roho ya
hekima; maana Musa alikuwa amemwekea mikono yake juu yake na aliishi miaka mia moja
na kumi, alimtumikia Mungu katika kipindi hicho chote, aliweza kuona jinsi watu
walivyoweza kushindwa kumtumikia Mungu kwa dhati.
Kwa nini Joshua alitambua
kuwa nyumba ndio msingi mkubwa wa ibada. Familia ndio msingi pekee wa imani,
lakini tunahitaji familia iliyo bora. Tunaona familia aliyokuwa na mfano mzuri
wa kuigwa ilikuwa ya Joseph, Mary na
Yesu.
Nyumba bora inajengwa katika
msingi bora tabia, na tabia njema ndio msingi mzuri wa familia bora ambayo ndio
msingi pekee wa ibada na imani. Bibilia inatufundisha kuwa familia lazima
ijengwe katika msingi wa Tabia bora. Tukumbuke kuwa familia ni msingi imara
kabisa wa imani yetu; katika Familia
wazazi wetu ndio msingi wa familia, ndio maana Joshua alisema kuwa yeye na
familia yake watamtumikia Bwana. Wazazi ndio kielelezo cha familia ndio maana
bibilia inatukumbusha kuwa tunatakiwa tuwaheshimu wa wazazi wetu ili tupate
Baraka ya kuishi mimi miaka mingi yenye kheri hapa dunia.
Joshua alipokuwa na wana
wa Israeli alitambua mapungufu haya; ndipo alipowaambia ni wakati wa kufanya
maamuzi ni nani utamtumikia Mungu au Miungu ya uongo; na aliwaambia kuwa Mungu
Kabwe alazimishi sisi kumtumikia yeye; anatupa sisi uhuru wa kuchagua ndio
maana Joshua alitumia hekima hiyo kuwaambia wana mtumikia nani? Lakini yeye na
nyumba yake watamtumikia Bwana.
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa kama wazazi tunamchango, mkubwa sana katika kutimiza wazo
hili la Joshua; Kama wazazi tunatakiwa kuwajengea watoto wetu, misingi mizuri
toka mwanzo wanavyokuwa kwa kuwafundisha maadili mema ya kibibilia na kushiriki
ibada kwa moyo ili nao wawe sehemu ya ujumbe wa Joshua. Ni jukumu letu wazazi
kuhakikisha kuwa tunatekeleza ujumbe kwa kujenga familia ambayo inampenda Mungu
na Kumwogopa Mungu.
Kama familia tunatakiwa
kuendelea kuomba ili tuweze kuwa na familia ambayo inasikiliza na kuishi
kulingana na bibilia inavyotufundisha. Tunatakiwa kuomba neema ya Mungu
itawale, familia zetu na neema yake daima yake ndiwe iwe ni dira ya maisha na
mafanikio yetu.
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa tunatakiwa tuyaangalie maisha yetu toka huko nyuma mpaka leo
hii na mafanikio ambayo tumepata je tumeona ukuu wa mungu?
Familia bora ni ile ambayo
inatambua kuwa mafanikio na mitihani yote ya maisha ni mpango wa mungu hivyo
tunawajibu wa kusema asante. Na hivyo kuwa tayari kumtumikia Mungu wakati wote.
Familia bora inamshukuru Mungu kwa kujaliwa neema za mafanikio na kuwa tayari
kutoa na kusaidia wahitaji;
Tafakari hii inatukumbusha
umuhimu wa kufanya ibada; hapo tunatimiza wajibu wetu wa kumwogopa Mungu, Joshua 24: 14a kumwogopa Mungu ni kuonyesha,
utii na unyenyekevu kuwa wafuasi ambao tunasali toka ndani kwa imani kubwa. Je
sisi wazazi tunaonyesha kuwa ni watu wenye Imani thabiti na wamwogopa Mungu?
Kama wazazi tutaonyesha
unyenyekevu juu ya Mungu wetu na watoto wetu watakuwa hivyo; Kama wazazi
tutakuwa mfano mzuri katika ibada na kuonyesha mfano mzuri wa kumtolea mungu
sadaka na zaka au fungu la kumi na watoto wetu watakuwa hivyo na Mungu
atatuneemesha kama kitabu cha malaki kinavyotufundisha. Ujenzi wa nyumba bora
ya kumtumikia Bwana inahitaji misingi Imara ya Imani ambayo inatokana na
wazazi.
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa mimi na nyumba yangu tutaweza tu kumtumikia Mungu kwa tutaweza
kutemebea katika matendo yetu mazuri na sio maneno matupu. Hivyo matendo ndiyo
yajengayo familia bora; Joshua 24:14b anatukumbusha kuwa kuwe na mwamko wa
pekee bila huruti, mwamko wa kiimani na kila sehemu ya maisha yetu lazima
ikabidhiwe kwake. Kusimkaribishe kabisa shetani. Familia ikisimama katika umoja
wake tutaweza kumtumikia Mungu kwa furaha na faraja kwa mafanikio makubwa sana
na neema ya Mungu itakuwa juu ya familia yote.
Tafakari ya leo
inatuonyesha jinsi familia nyingi leo hii zinavyoshindwa kwa umoja wake
kumtumikia Bwana. Familia zetu zimejaa mifarakano, magomvi tabia mbaya, wakati
huo huo wazazi wakionyesha mifano mibaya kwa watoto wao na kupelekea watoto pia
kuishi maisha ambayo hayampendezi kabisa Mungu. Wakati umefika tunatakiwa
kurudi katika misingi ya Imani kama Joshua alivyotuonyesha umuhimu wa familia
katika kumtumikia Bwana. Hatujechelewa tunachotakiwa ni kuanza sasa
kuziimarisha familia zetu na kumtumikia Bwana kwa moyo wetu wote.
Tafakari pia inatukumbusha
kuwa Mungu hapendi wanafiki, hivyo hili ni somo muhimu sana kwetu, kama kweli
tunaamua kumtumikia Mungu tufanye hivyo kwa dhati kabisa. Mungu anatujua sisi
kuwa sio wakamilifu, lakini anamchukia sana mtu mnafiki ambaye hujionyesha kwa
maneno bali matendo yake ni ya shetani. Mungu ametupa uchaguzi wa chochote
tunachotaka kukifanya au kukifuata, au jinsi ya kuishi na hatimaye hata njisi
ya kuabudu na kumsifu Mungu, lakini Mungu anapenda sisi tufanye uamuzi sahihi
kama Joshua na familia yake walivyofanya
wa kumtumikia BWANA hii ndio tafakari yetu ya leo.
AMINA
No comments:
Post a Comment