WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Thursday, March 24, 2016

PETRO: BWANA HUTA NIOSHA MIGUU YANGU?

       

Yohana 13: 8


Tafakari ya Leo  tunaangalia msimamo wa Peter alipomwambia Yesu Kuwa Bwana , wewe huta niosha miguu mimi?"  katika maisha ya Bwana wetu Yesu maisha yake pamoja na Mitume wake; Mara zote Peter ameonekana daima alileta kauli au hali tata katika Mambo mengi; ya kukataa au kujichanganya mwenyewe alipokuwa akipewa maelekezo na Yesu au kuulizwa swali; Peter pamoja na kukaa na Yesu bado kabisa alikuwa anatumia zaidi akili yake ya kibinadamu katika mambo mengi;  Tukumbuke Yesu alipowaambia mitume wake Mwana wa Adamu alipokuwa anakwenda Yerusalemu kuteseka na kufa: Peter alijibu nini Kamwe, Bwana! Si wewe!

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa tulio wengi tunafikiri kama Petro; tumefunuliwa lakini hatuoni ufunuo wa Mungu kwa ajili ya utukufuwa Mungu; tunataka ufuo ambao tunao bado ufanye kazi katika akili na mazingira ya kibinadamu; kwa maneno mengine tunaishi katika kizazi ambacho kina kiburi; kizazi ambacho hakipo tayari kufuata maelekezo; kizazi ambacho hakipi tayari kumtumikia Mungu kwa kuachana na uchafu wetu wa miguu yetu; na tunapotaka kusaidiwa kuoshwa bado tunapinga na hatuoni umuhimu kwa kupata msaada huo;  bado tumeendelea kuwa kizazi ambacho tunataka kuendelea kujisifu; kizazi ambacho hatuoni umuhimu wa nyenyekevu;

Tafakari ya Alhamis Kuu itukumbushe kuwa tunatakiwa  kujithamini, kujijengea upendo , na kutegemea utukufu wa Mungu katika maisha yetu; tukumbuke Yesu alivyoendelea kujibishana na Petro na alivyomwambia;Yeye aliyekwisha kuoga hahitaji kuoga tena bali kusafishwa miguu yake  kwa kuwa mwili wake bado uko safi ; Na wewe ni safi, lakini si nyote; Yesu hapa alionyesha kuwa mbali na kuwasafisha miguu bado sio wote wako safi kwani alijua kuwa yuko mmoja ambaye atamsaliti.

Tafakari ya Leo inatufundisha kuwa tunatakiwa kuwa na subira na kupokea maelekezo kwa unyenyekevu ili kuona baraka ya Mungu juu yetu; alionyesha upendo kwa mitume wake lakini alitaka na mitume waonyeshe upendo miongoni mwao na kwa wale wote ambao watakuwa pamoja nao. Tunatakiwa kutimiza upendo wetu kwa matendo na sio maneno matupu. Petro ametu onyesha kuwa alivyokuwa anamchukulia Yesu ilikuwa tofauti na Yesu alivyokuwa akitaka iwe au ifanyike; Petro alikuwa anamchukulia yesu kama Kiongozi ambaye hastahili kuwaosha miguu mitume wake kwani hiyo ilikuwa ni kazi ya Kitumwa; Mitume walitakiwa mwamwoshe miguu yesu; Lakini yesu anawaonyesha Mitume Hasa Petro kuwa Miguu ni sehemu ya Utakatifu; hivyo kuwaosha wao miguu yao  maisha yao; yesu aliwaosha Miguu yao bila kujali hali ya miguu yao na uchafu na harufu yake; alifanya kwa upendo mkubwa wa kuosha na kuifuta

Pamoja na Udhaifu mkubwa wa Petro kila anapofanya mazungumzo ya muda mrefu na Yesu alikuwa anaharibu , au anaongeza majukumu zaidi , kama alivyomwambia Yesu, sawa basi isiwe tu miguu yangu, bali mikono yangu, na kichwa change; petro ametuonyesha kuwa amlikuwa na unyenyekevu wa kukubali makosa na kasha kuomba msamaha na kutekeleza yale alioombiwa; tukumbuke kuwa safari yetu ya njia ya maisha ni chafu sana kuliko sisi tunavyofikiria. Maisha yetu yawe kama yale ya Yesu na mitume wake kwani daima alikuwa akiwaelekeza ili waondokane na uchafu wa maisha ya dunia hii; kukaa na kudumu katika usafi wa kiroho ni mtihani mzito kutokana na  ubinadamu wetu na tabia yetu ya kuwa tunajua zaidi na hatutaki kufuata maelekezo kama Petro. Tuendelee kukumbuka kuwa . Hakuna jambo ngumu kukaa katika usafi , sisi wote ni wachafu zaidi kuliko kuliko tulivyo sasa.  Ujio wa Yesu na kuwa tayari kufa msalabani ni sawa na kualikwa kwa hiari kwenda kuoga ili tuwe safi na tuweze kuvaa nguo safi ambazo zimesafisha kwa damu ya mwana kondoo; hivyo sisi bado tunahitaji kutakaswa kila siku kwa damu ya Kristo .

Tafakari yetu ya leo inatukumbusha kuwa kama vile ilivyokuwa kwa Mtume Petro, sisi sote ni wadhambi kwani Yesu katika Mazingira tofauti alishawahi kumwita Petro shetani, na kumwambia aondoke mbele ya uso wake; kwa mawazo na jinsi ambavyo Petro alikuwa akifikiri na kujibu bila kutafakari hata kama nia yake ilikuwa njema katika maona ya kibinadamu; hivyo sote yunaangukia katika mtego huu wa Petro kwani pamoja na nafasi ambayo tumepata kupitia wokovu wetu kwa damu ya Yesu Msalabani bado tunafanya mambo bila kufikiri; kwa njia za kibinadamu hivyo nasi bado tunahitaji msaada na huruma ya Mungu.

Tukumbuke kuwa sisi binadamu wote ni wadhaifu na tutabaki kuwa wadhaifu bado tunaelea katika dimbwi la zambi; tunaendelea kutawalaiwa, kuishi kwetu, kufikiri kwetu, hata wakti mwingine matendo yetu  yamegubikwa na maovu, na tumekuwa na kiburi hata cha kukiri kuwa ni wakosefu; baada yake tumeendelea kujiona kuwa tu watakatifu miongoni mwa wa watakatifu wa kweli japo matendo yetu yamejaa ushetani mtupu. Mtume Petro anatuonyesha kuwa pamoja na udhaifu wake kama binadamu aliweza kutoa maamuzi haraka hata kama yalikuwa yakikingana na mwono halisi wa Yesu lakini alionyesha Imani hata kama ni dhaifu. Alikuwa tayari, kutembea juu ya maji japo alianza kuzama kwa uhaba wa imani; bora yeye aliyejaribu kuliko wale kumi na moja ambao hata hawakutamani kujararibu;

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa sisi binadamu tunaishi katika maisha hatarishi sana bila kujitambua na hata pale tunapopatiwa msaada tunakuwa na mwelekeo wa kuukataa kama vile Petro alivyokuwa akimkatalia Yesu alipokuwa akitekeleza tendo kuu la unyenyekevu. Tukumbuke kuwa bila kuwa wanyenyekevu hatuwezi kujitambua kuwa tunatembea katika njia sahihi. Hivyo Alhamis hii Kuu itukumbushe dhana nzima ya kumtumikia Mungu Kupitia unyeneykevu ambao itatuondolea majisifu binafsi; kujiamini na kuto mtegemea Mungu wetu; Narudia tena leo tujikumbushe kuwa daima tunakuwa wepesi wa kuongea hata bila kufikiri matokeo ya baadae; Lakini uzuri wa Petro alikuwa Mtume Pekee ambaye aliweza kujaribu bila kuwa na mashaka. Pamoja na Petro kuitwa ni Mtu mwenye imani , lakini mwepesi wa kukiri na kuomba msamaha. Ndio maana Yesu alimchagua kuwa Nguzo ya Kanisa lake na kiongozi wa Kondoo wake duniani.  

Tafakari yetu ya leo inatuonyesha Yesu ametuonyesha njia ya upendo wa khali ya juu bila kubagua kwani alimwosha miguu hata msaliti wake wakati akijua ndiye atakaye msaliti. Hivyo findisho tunalolipata leo ni kuwa tayari kuwahudumia wengine hata kama hawatupendi, na tutapata kheri sana na faraja kubwa kwa kufanya hivyo; Najua kuna baadhi yetu huwezi kuosha miguu wenzako kwa sababu ya mafanikio ambayo mtu anakuwa anayo na hata kama atafanya hivyo atafanya kwa wale tu wanaofanana; hatuko tayari kuwasaidia yatima, wajane, masikini na wote wenye hitaji la kweli;
Tafakari ya siku hii ya leo ni muhimu sana katika maisha yetu ya kiroho; kwani baadhi yetu sit u tumekuwa wagumu kuwaosha miguu jirani zetu , tunajifunza kwa  Yesu ambaye aliosha miguu ya muuaji wake ( Judas ). 

Je tunaweza sisi kumtendea jema Yule ambaye tunajua hakupendi, anakusengenya, anakuchukia? Tunatakiwa tujifunze Ukarimu wa Yesu kwetu sote bila hakutubagua alitupenda jinsi tulivyo; tunachotakiwa kujifunza hapa ni kuwa  huwezi kuwa mkarimu kwa watu mpaka umejifunza kuwa na subira na kukubali kuwa mtu wa kawaida. Na kubwa zaidi huwezi kuwa Mkarimu bila kumkaribisha Mungu kwa njia ya Roho yake imeweze kuishi ndani yako; binadamu wengi ukarimu wetu tunajaribu kuuonyesha katika tabasamu lakini ndani ya mioyo yetu tu chui wa kuogopwa. Ndio maana mara zote katika mafundisho yake Yesu alisema waogopeni wanafiki na wale ambao wanapenda sana kujikweza;

Tafakari yetu inatuasa kuwa tunaishi katika ulimwengu unaojiendesha kwa kuto kumpa Mungu nafasi; tunawaona watoto wetu wakijiua wenyewe kwa kukata tamaa au kwa kujiingiza katika ulimwengu wa dhambi; Tunashuhudia wanasiasa wakiendelea kuwa waongo na kujilimbikizia mali huku wakiwaacha wajane , Yatima, na wamanchi masikini wakiwa wakiendelea kuteseaka; Hivi Alhamis hii kuu tujirudi kama Mtume Petro ambaye hatimaye alikubali kuoshwa miguu yake na Yesu na kutimiza amri ya upendo na hatimaye kuwa kichwa cha kanisa.

Hii ndio Tafakari yetu ya leo nawatakieni Juma kuu Lenye baraka na Upendo wa Kimungu- Amina


Emmanuel Turuka

No comments:

Post a Comment