March 17
1 Wathesalonike 5:11
Tafakari ya leo tukiwa bado tunaendelea na mfungo wa Kwaresima tunatakiwa tuishi
kama Tai; Tai ni Ndege ambaye anaweza kuruka juu kuliko ndege
wengine wote na kwa kasi ya ajabu sana. Tai ni ndege ambao wanaruka pamoja bila
kubaguana kwa upendo mkubwa; Tai anaona umbali mara
saba zaidi ya jinsi anavyoona binadamu. Tai anaouwezo wa kuona chakula kama
vile samaki, kisha hulenga shabaa toka mbali na kumpata mlengwa. Tai ni ndege
mwenye nguvu kuliko ndege wengine. Tai makazi yake yako juu ya miti mirefu sana
kuliko ndege wengine. Je sisi kama wakristo maisha yetu ya Kumtumikia Mungu
yanalingana na mwenendo huu wa Tai wa kujiamini?
Tafakari ya leo
inaendelea kutufundisha kuwa tukiweza kutumia jicho la Tai katika maisha yetu
tuishi kwa kufikiria mambo ya badae tunatakiwa tuwe kama Tai tuwe wa moja
katika kumtumikia Mungu kama 1 Wathesalonike 5:11 Basifarajianeni na Kujengana
kila mtu na mwenzake, vile vile kama mnavyofanya. Ni ujumbe mzito amba Tai
wanaufanya pamoja katika maisha yao kama ndege. Hapa tunatakiwa kwanza ni kuithamini nafsi yako na
kuisikiliza sauti kubwa itokayo moyoni mwako,ikuongozae juu ya kutenda,hii ni
sauti ya Mungu iletayo mafanikio,furaha na kila lililo jema.Sauti hii inakupa
nguvu ya kutenda miujiza kila wakati,ndiyo inayofanya nuru ya maisha yako
ing'ae. Lazima ujikubali kwa kuwa mimi ni zaidi ya nilivyo.Ukiachilia mbali
mazingira ninayoishi na sura yangu,mimi ni wa thamani,kama wengine. Wewe ni wa
thamani jinsi ulivyo,na thamani yako ni sawa na binadamu wote.Unao uwezo wa
kuwa na kuishi maisha ya furaha na mafanikio. Unastahili, wewe ni Matokeo ya
kazi kubwa ya Mungu. Tunatakiwa kuanza kujikubali na kuepuka misukumo ya
wale wanaokuzunguka. Anza kutazama uwezo ulio nao,tazama chemchem ya mafanikio
iliyopo ndani mwako.Sisi sote ni bora .Sisi wote ni wamoja. Huu ni wakati wa
kujifunza kuwa wewe, kujikubali, kukua na kubadilika. Anzakujitambua wewe kisha
utatambulika kwa wengine. Kama vile Tai walivyojitambua kuwa wao ni ndege bora
na wanaweza kruka juu kabisa kuliko ndege mwingine yeyote.
Tafakari ya leo inataka sisi tuvumbue
uwezo ulionao.Tumia uwezo tulionao kupaa juu ya mipaka unayofikiri ipo
katika kuutafuta ufalme wa Mungu. Fanya yale unayoyakusudia maishani na uwe
vile unavyotaraji kuwa. Umezaliwa kuwa kiongozi wa maisha yako na kuyatawala
mazingira yako ili kuufikia uzima wa milele.Unaweza kupaa juu zaidi na zaidi
pasipo kudondoka. Vikwazo vijitokezavyo dhana ya kifikra tu. Hatupaswi kuruhusu
kuruhusu fikra za wanaokutuzunguka zitufanye tuwe na mawazo mgando ama yenye
mipaka na kutuletea mashaka katika safari yetu ya mbinguni. Huwezi kuruka juu
kama tutabaki na fikra kama za kuku na kuendelea kukwaruza na kudonoa tu. Amua
sasa kuruka juu ili kumtumikia Mungu.
Tunataadharishwa
kuwa lazima tuwe kama Tai kuwa na maono na nguvu ya kuamua, ili waweze kutambua
na kufanikiwa katika mawindo yetu na kufanikiwa kupata kila kutitakacho; Wakati
huo huo, tai unaweza kuona adui zake kutoka mbali, kama vile nyoka amabao anajaribu
kuvamia kiota chake ili aweze kuiba mayai yake au kuua vijana wake. Ingawa tai
kujenga viota vyao kwenye miamba ya juu na maeneo, nyoka kuwa na tabia na uwezo
wa kupanda kwao. Lakini maono kali ya tai yanaamsaidia kuona maadui kutoka mbali
na kiota chake. Tukisoma Warumi 14:17 maana ufalme wa Mungu si kula wala
kunywa, bali ni haki na amani na furahakatika roho Mtakatifu.
Sisi kama watoto
wa Mungu ni lazima kuzingatia malipo mambo mazuri ya amani, furaha, na haki. Tukumbuke
kuwa lazima tujiandae kwa nguvu zote tukijua kuwa shetani na wafuasi wake wana uwezo
wa kushambulia kiota chetu, ambayo ni Familia yetu, fedha, mahusiano, afya,
ustawi wa kiroho, Wakati ulimwengu mapepo ya enzi, mamlaka, na wakuu wa giza
hili ambao ni kujaribu kuiba, kuua na kuharibu maisha yetu tele ya Mungu ndani
ya familia zetu, wapendwa, na jamii yetu, tunaona ni kutoka mbali na mtizamo na
maono nguvu ya Mungu na kuanza kupinga hilo kwa kushambulia yake. adui ambaye
anajaribu kuja katika kuwa na hofu na kukimbia mbali 1 Peter 5:8 Muwe na Kiasi
na kukesha kwa kuwa mshitaki wenu ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka
zunguka, akitafuta mtu ammeze. Hivyo tunatakiwa tuwe na nguvu za kushindana na
adui kama Tai afanyavyo. Tunatakiwa kuendelea kuomba bila kuchoka; ili kwa
neema ya Mungu tuendele kupata faraja kubwa sana.
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa ushindi wetu uko juu ya Mwili na damu ya Bwana wetu Yesu
Kristo; Yohana 6: 55-57 Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli , na damu
yangu ni kinywaji cha kweli. Aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, akaa
ndani yangu, nami ndani yake. Kama vile Baba aliye hai alinituma, nami naishi
kwa sababu yake; vivyo hivyo anilaye Mimi wataishi kwa sababu yangu. Maana yake
ni nini? Sisi , waumini , ni mmoja
ambaye kula nyama safi ya maneno ya Yesu kutoka mbinguni kupitia mafundisho
Roho Mtakatifu , ambayo daima kutufanya kuishi maisha yake hapa duniani kifalme
kama vile tulivyopasa tuishi mbinguni; 1 Kor 2:13 Nayo twayanena, si kwa maneno
yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na
Roho,tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.
Tafakari ya leo
inatufundisha kuwa Tai ni ndege wanaopenda sana kuwa tayari wakati wa dhoruba.Tunafahamu kuwa ndege wengine wote hujaribu
kuto ruka wakati wa dhoruba na kujificha kwenye viota vyao au mapango yao kwa ukali
wa upepo, Lakini tai hupenda kuruka wakati huo kwa kutumia upepo wa dhoruba ili
waweze kuruka juu zaidi kwa muda mfupi. Tai ni wanjanja kwani wanjua kwa
kutumia upendo wa dhoruba wataruka juu dhaidi bila kutumia nguvu yao watakuwa
wanaelea tu na kusukumwa na upepo huo. Katika maisha yetu ya kila siku
tunakutana na dhoruba nyingi katika maisha yetu kama shida mbalimbali, majonzi,
na majaribu malimbali; tukisoma Yohana 16:33 Haya nimewaambieni mpate kuwa
naamani ndani yenu. Ulimwengu mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda
ulimwengu. Au Kitabu cha Yakobo1:12 Heri mtu astahimiliye maajaribu; kwa sababu
akiisha kukubaliwa atalipokea taji la uzima. Bwana alivyowaahidi wampendao. Lakini
tukumbuke kuwa tunatakiwa kuhesabu furaha tupu tukiangukia katika majaribu
mbalimbali, mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi
na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa
chochote.
James 1: 2-4. Tukumbuke
jini Mungu alivyomjaribu Ibrahimu kabla ya yeye kuaminiwa kwake kama rafiki
yake mpendwa kwa milele
Tulio wengi
tukijaribiwa kidogo tu; tunalalamika sana na kukata tamaa baadhi yetu tunakuwa
kama Waisraeli walivyokuwa wakimlalamikia Mungu alipowatoa katika nchi ya
Mateso Misri; tukumbuke kuwa Mungu anahitaji kutu pima kwa sababu sisi sio viumbe
kamili bali tunahitaji kusafishwa kupitia majaribu mbalimbali, na mateso ili tupate
kuwa wakamilifu; na mara baada yamajaribu, Mungu hutuimarisha sisi kwa milele yeto;
1 Petro 5: 10 Na mungu wa neema yote aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa
milelekatika kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yey mwenyewe
atawatengeneza na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu.
Je sisi ni kama tai ambao daima
kujenga viota vyao katika mahali pa juu ambapo adui hawezi kufikia kwa urahisi?
Mungu siku zote ana nguvu za kutuinua sisi juu lakini yatupasa kuwa Wanyenyekevu,
masikini wa roho,tuwe wapole na tuwe rehema ya Mungu; Tukumbuke kuwa kama tai
anavyowapenda watoto wake: Mungu alitupenda sisi zaidi, kwani ni upendo gani
mkubwa wa kumtuma Mwana wake wa pekee kuja dunia kuishi nasi na kasha kufa
katika kifo cha aibu msalabani ili nasi tuweze kingia katika ufalme wa mbinguni;
Tunafunga Tafakari yetu ya leo kuwa kwa
kutilia mkazo jambo kuwa kama ilivyo kwa tai katika anga inawakilisha siri ya
Mkristo ambaye amejifunza na kuwa tayari kumpigania Mungu katika khali yeyote
ile katika ulimwengu wa roho, tunafahamu kuwa tupo kwenye changamoto nyingi
kama upepo wa mashaka na dhoruba za maisha bali tunatakiwa kutegemea zaidi msaada
wa Mungu. Hivyo tukiweza kumtegemea Mungu yeye atatufanya sisi tuweze kupaa juu
zaidi na kuelee katika dhoruma yeyote ile bila shaka lolote.
Tunatakiwa kuwa kama Tai ili tuweze
kuweza kufurahia maisha utakatifu, ni moja ya siri kubwa ya imani. Tunatakiwa kutenda
kama Yesu na kuishi maisha ya mkristo kwa uadilifu mkuu na ili tuweze kushinda maisha ya ufalme wa mbinguni.
Tunatakiwa tuwe, si jogoo wala kuku .
Hii ndio tafakari yetu ya leo
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment