March 20
Mathayo 6:14-15
Tafakari ya leo tujikumbusha kuwa mwanandamu anahitaji upeo mkubwa
wa nuru ya kiroho ambayo itaweza kumfanya azike tamaa zake na hisia zote za
kulipiza kisasi; tunatakiwa kuwa na uwezo wa kujizuia na hasira, kuzikandamiza
hasira, chuki kwa moyo mpana na kujenga daraja la msamaha. Kusamehe mtu
ambaye amekukosea, kuwapenda ndugu na jamaa ambao wameukata uhusiano pamoja
nawe, na kuwa mkarimu kwa yule ambaye aliwahi kukunyima, kukutukana,
kukusababishia hasira,kukudharau, kukudhalilisha na kadhalika sio jambo rahisi.
Tumewaona hata watumishi wa Mungu ambao wanaielewa sana bibilia wakishindwa
kabisa kuktekeleza kanuni hii.
Tafakari
yetu leo tujikumbushe wajibu wa kumsamehe yule aliyekutendea yasiyo sahihi
hutusaidia kutupatanisha na Muumba wetu; vile vile msamaha hudumisha mshikamano
wa udugu ambao umeharibiwa. Kwa kusamehe tunaandaa njia ya kumwendea Mungu; Lakini pasipo imani haiwezekani (Waebrania
11:6). Inatufundisha kuwa mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu
wale wamtafutao,”. Msamaha hutujengea wa kumwendea na Kuishi na Mungu katika
Imani.
Kama ilivyoandikwa hakuna mwenye haki, hata mmoja” (Warumi 3:10). Mungu
yuko tayari na anasubiri kumsamehe mtu anaye omba msamaha imeelezwa katika
Zaburi 86:5 "Kama wewe Bwana u mwema, umekuwa tayari kusamehe, na mwingi
wa fadhili kwa watu wote wakuitao". Daudi aliweka wapi tumaini lake la
msamaha? Tukisoma Zaburi 51:1 "Ee Mungu unirehemu sawasawa na fadhili zako
kiasi cha wingi wa rehema zako uyafute makosa yangu. Mathayo 6:14-15 Kwa
maana mkiwasamehe watu makosa yao na Baba wenu wa mbinguni atawasamehe ninyi
bali msipowasamehe watu makosa yao wala Baba yenu hatawasamehe makosa
yenu." Wale wamesamehewa husamehe. imeandikwa Waefeso 4:32 "Tena
iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma ninyi mkasameheane kama na Mungu
katika kristo alivyowasamehe ninyi."
Kusamehe kwa kweli hakuhesabu makosa.
imeandikwa Mathayo 18:21-22 "Kisha petero akamwendea akamwambia Bwana
ndugu yangu anikose mara ngapi nami ni msamehe? hata mara saba? Yesu akamwambia
sikwambii mara saba bali hata saba mara sabini." Katika kusamehe Yesu
ametukomboa kutoka kwa dhambi na mshahara wa dhambi. Wakolosai 2:13-14
inatueleza kuwa "Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na
kutokutahiriwa kwa mwili wenu aliwafanya hai pamoja naye akisha kutusamehe
makosa yote akisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake
iliyo kuwa na uwadui kwetu akiondoa isiwepo tena akaigongomea msalabani."
Tafakari yetu inazidi kutufunsidha kuwa Zaburi
51:7-12 "Unisamehe nami nitakuwa safi, unioshe nami nitakuwa mweupe kuliko
dheluji unifanye kusikia furaha na shangwe, mifupa ilio ponda ifurahi. usitiri
uso wako usitazame dhambi zangu uzifute hatia zangu zote Ee Mungu uniumbie moyo
safi uifanye upya roho iliyo tulia ndani yangu usinitenge na uso wako wala roho
wako mtakatifu usiniondolee unirudishie furaha ya wakovu wako unitegemeze kwa
roho ya wepesi."
Zaburi 32:1-6 "Heri aliyesamehewa dhambi
na kusitiriwa makosa yake heri Bwana asiyemhesabia upotovu, ambaye rohoni mwake
hamna hila niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa kwa kuugua kwangu mchana kutwa
na kwa maana mchana na usiku mkono wako ulinilemea jasho langu likakauka hata
nikawa kama nchi kavu wakati wa kaskazi nalikujulisha dhambi yangu wala
sikuuficha upotovu wangu nalisema nitayari maasi yangu kwa Bwana
naweukanisamehe uoptovu wa dhambi yangu kwa hiyo kila mtu mtauwa akuombe wakati
unapopatikana hakika maji makuu yafurikapo hayatamfikia yeye."
Wale walio wanyonge moyo wako mbele ya Mungu na
wala kutambua hatia yangu, haijafika hali ya kwanza ya kukubalika. Tunahitaji
kuokolewa kutoka katika aina zote za tabia zetu mbaya pamoja na misukumo ya
ndani inayotushurutisha kufanya mambo fulani mabaya: kama vile, kusema uongo,
hasira inayomfanya mtu atukane watu, tamaa mbaya za mwili, uchungu, kutaja
machache tu.
Hatuwezi kujiokoa wenyewe kutoka katika dhambi
au kuigeuza tabia yetu kwa kujitegemea wenyewe kama vile Simba asivyoweza
kuamua awe mwana-kondoo (Warumi 7:18). Dhambi ina nguvu nyingi kuliko nia yetu
ya kufanya yale tuyatakayo. Lakini Kristo anaweza kukufanya wewe uwe
"imara kwa uweza wake, kwa kazi ya Roho wake katika utu [wako] wa
ndani" (Waefeso 3:16). Anafanya kazi yake ili kuondoa tabia zetu ziletazo
uharibifu na mahali pake kuweka tabia hizi nzuri: upendo, amani, furaha, upole,
uwezo wa kujitawala (Wagalatia 5:22,23). Kristo anaishi maisha yake kupitia
ndani yetu, kisha tunapokea uponyaji wa kiroho, tunarejeshwa katika maisha
mapya, na kuwezeshwa kuishi maisha hayo mapya.
Hakuna dhambi ambayo ni ya kutisha sana
asiyoweza kuisameka Yesu anatamani sana kwamba kila mmoja wetu hatimayeawe na
uhusiano mzuri na Yule aliyemkosea na kumsababishia majeraha ambayo yamejenga
chuki ambayo inahitaji msamaha. Yesu anataka tupokea msamaha na utakaso wa
Mungu ni; katika imani jambo ni rahisi na la maana sana
kama tunavyofurahia kumpokea motto mdogo aliyezaliwa na kumkumbatia. Lakini
kutokana na ubinadamu wetu, majivuno, kiburi, masengenyo inatuwia vigumu sana
kutoa msamaha wa kweli pale tunapokosewa, tunakuwa na kiburi ambacho
kinatufanya kuona kuwa Yule aliyetukosea hastaili msamaha wetu; lakini kama tunayafuata
mafundisho ya yesu na mifano ambayo ametutolea katika Bibilia Takatitifu
tunatakiwa tuondoe ugumu katika mioyo yetu na kuuvaa unyenyekevu kama yeye
alivyovaa unyenyekevu na kuuvua Umungu kwa ajili ya makosa yetu, na alikuja
kukaa nasi na ametutengenezea daraja la msamaha ambalo kila mwanadamu lazima
alipite ili kuweza kukamilisha safari yake ya kwenda mbingu.
Hebu jitafakari kwa nini umekuwa na kiburi cha
kushindwa kabisa kumsamehe, jirani yako, ndugu yako ambao wamekukosea kutokana
na ubinadamu wao, usijali amekukosea mara ngapi angalia je wewe uko tayari
kumsamehe wakati wowote ule?
Hii ndio Tafakari yetu ya leo katika Jumapili hii ya Matawi- Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment