March 31
Yohana 3:20
Kwa nini tunamkimbia Mungu Tafakari ya leo inatupa jibu
rahisi sana kwa nini tunamkimbia Mungu,
tunamkimbia Mungu kwa sababu sisi binadamu tunataka kufanya au kuendelea kuishi
katika misha ya dhambi ambayo yako kinyume na maagizo yake; Yohana 3:20 kwa kuwa kila mtu atendaye mabaya huichukia
nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.
Tafakari ya leo inatueleza sababu nyingine ambayo
tunamkimbia Mungu ni kwa sababu ya Machungu tunayo yapata katika maisha yetu
kwa sababu tunaona Mungu hana msaada kwetu kutokana na maisha ambayo tunaishi
na tabu zote ambazo ziko mbele yetu. Sasa Mungu yuko wapi? Kwa nini amekubali
mimi nipate shida zote hizi.
Tafakari inatuongoza kuwa pamoja na yote
yanayotokea katika maisha yetu; Lakini bado tunatakiwa kumpa sifa Mungu pamoja
na mateso au shida zozote zile kama tunavyosoma katika zaburi 107:1 Mshukuruni
Bwana kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake ni za milele; bado tunatakiwa
kushukuru wema wa Mungu na sio kumkimbia au kukata tamaa katika majaribu yetu;
Tafakari yetu ya leo inatukumusha kuwa tunamkimbia
mungu kutoka na maisha au mazingira
ambayo yanatuzunguka leo hii; 1Peter 5:7 na tumesahau kuwa sisi tumeumbwa
katika ulimwengu huu ili mwenyezi Mungu atupime namna gani tunaendelea
kumshukuru na kumsifu pamoja na shida zote zinazotuzunguka. Tumepewa akili na
uhuru tuutumie tutakavyo lakini bado tunawajibu wa kujaribiwa katika yale ambayo
tunayoyafanya; Mungu ameshatoa maelekezo ya nini tufanye na nini tusifanye? Mathayo
10:28 msiwaogope wauao mwil, wasiweze
kuiua na roho; afadhali mwogopeni Yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia
katika jehanum
Lakini sisi binadamu tunakuwa na tabia ya kiburi na
kuchagua kutenda yale tupendeya ambayo hayampendezi Mungu na hivyo kujiwekea
sifa ya Kumkimbia. Waebrania 11:6 lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza;
kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko , na kwamba
huwapa thawabu wale wamfuatao. Tukisoma waraka wa 1 Peter 1:7 ili kwamba
kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo,
ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na
heshima katika kufunuliwa kwake yesu Krsito. sehemu hii ya bibilia inatuonya
kuwa hatuna sababu ya kukimbia na kumkimbia Mungu;
Tafari ya leo inatuunganisha vile vile na kisa cha
Yona alikimbia wito wa Mungu na akafikiri kuwa amefanikiwa kumbe sio kweli;
Tukijua kuwa Mungu ni Alpha na Omega kuwa yeye huishi nyakati zote, na kwa
msingi huu kamwe hatuwezi kuukimbia uso
wa Mungu hata kama tutakuwa wanjanja kama nini: mara nyingi tunawaogopa wanaua
mwili; tunawaheshima na kuwanyeyekea lakini tunamdharau au kumpuza yule ambaye
anao uwezo wa kuua Roho kwa vile hatumwoni kwa Macho hivyo tunafikiri kuwa ni
rahisi kumkimbia;
Tafakari yetu vile vile inatukumbusha Maisha
ya ya Mtume Paulo wakati ule akiwa
anaitwa Saulo njinsi alivyokuwa mkatiri na muuaji mkubwa wa watu wa Mungu.
Matendo ya Mitume 9:3-5 hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski;
ghafula ikamwangaza kote nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini akasikia sauti
ikimwambia Sauli Sauli mbona waniudhi? Akasema u nani wewe Bwana? Naye akajibu
mimi ndiye Yesu unayeniudhi wewe. Paulo kwa matendo yake mabaya alikuwa
anaukimbia uso wa Mungu kwa mauvo yake kwa kutenda vitu ambavyo vilikuwa
kinyume na maagizo ya Mumgu.
Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa hatuwezi
kumkimbia Mungu kwa kiburi chetu, majivuno, utajiri, chuki au kuwafanyia maangamizo watu wa Mungu; kinachotokea
tunajiangamiza wenyewe, kwa matendo yetu. Ni bora tuachane na tabia hizi mbaya
na kumrudia Mungu kwani Mungu ni rafiki wa kweli anayetupenda sana, na
anatamani sana kututuma kwenda kufanya kazi yake katika shamba lake. Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment