March 15
Wafilipi 2:5
Kwa
ujumla Mtazamo/tabia ni zao la ndani ya kila mmoja wetu tunapolinganisha na
mazingira yanayomzunguka kama watu na vitu; Tabia inatumika sana wakati
unapofanya kitu chochote nje yako mwenyewe yaani kitu ambacho akikuhusu wewe
mwenyewe. Neno la Mungu linatukumbusha katika hili kuwa kwa kuwa kwetu wakristo
tunatakiwa kuimarisha tabia na kuwa kama Yesu; Tukisoma Wafilipi 2:5 Iweni na
nia iyo ndani yenuambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu: Tukisoma Waefeso
4:22 mvue kwa habari ya Mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa
kuzifuata tama zenye kudanganya;
Wengi
wetu kwa urahisi tunaweza kutambua mitazamo mibaya kuonekana katika mazingira
tofauti kutoka na vitendo vyetu kama uasi, dharau, kukosekana kwa uvumilivu,
kukosekana kwa ushirikiano, kutojali, kuvunjika moyo, kokosekana uhuru, dhulma,
kiburi, ubinafsi, Hii ni mifano ya msimamo mbaya ambayo Wakristo wanapaswa
kukataa.
Mithali 23:7 hata mshale umchome maini; kama ndege
aendaye haraka mtegoni; wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake. Tukumbuke
kuwa mtazamo au tabia ni zao la mtu la ndani, limejificha ndani ya mtu ambalo
ndilo msingi wa matendo yetu tuyafanyayo. Hakuna mtu yeyote ambaye ajuaye wewe
unafikiria nini; ndio maana unaweza ukamchekea mtu na kumwonyesha kuwa wewe ni
mtu safi sana kwake bali mtazamo wako uko tofauti sana; kumbe wewe ni adui,
mkubwa; Lakini usijisahau kuwa Mungu anajua nini unawaza na nini unataka
kumfanyia mwenzako. Hivyo Mtazamo au tabia ni kitu ambacho Mungu tu ndiye
anayefahamu na yeye pekee anaweza kukusaidia kukurekebisha kwani mabadiliko
hayo lazima yaanzie ndani yako na kwa Masada wake.
Mifano
ya tabia mbaya iko mingi hasa kwa sisi wakristo kuna wale ambao wanakwenda
kanisani na kushiriki vitu vingi hata uimbaji wa kwaya, utoaji wa michango
mikubwa, wenye furaha wakati wote kwa sababu kila kitu kipo sawa kwa upande
wao; Kwa bahati mbaya mambo ya kigeuka hasa upande wa uchumi yakianza kwenda
vibaya kila kitu uanza kugeuka mahudhurio kanisani yanapungua; watu wanaanza kujijengea
chuki na watu wengine na hatimaye chuki hiyo hujengwa dhidi ya Mungu wakiamini
kuwa kwao Mungu ni sababu ya anguko lao; hivyo uasi unaanza hapo.
Lakini
tukumbuke kuwa mtazamo ulio bora wakati wa shida inatakiwa kwa tuwe karibu zaidi na Mungu - kuangukia
miguuni pa Yesu. Biblia inaeleza wazi kwamba Mungu hufanya mambo yote katika
wakati wote kwa upendo ule ule bila kubadilika katika mafanikio yetu na katika
shida zetu; tukumbuke kuwa shida kamwe haitamshinda mtu mwenye mtazamo sahihi
na mwenye kumtegemea Mungu.
Wagalatia
5:19-21 Matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi;
husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia
mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi
hiyo hawatauridhi ufalme wa Mungu.
Tutambue
kuwa mtu yeyote ambaye ana tabia mbayo inakwenda kinyume na mamlaka ya dunia
pia ana matatizo mbele ya Mungu.Wagalatia 5: 22-23 lakini tunda la roho ni
upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu, wema, fadhili. uaminifu; upole, kiasi, juu ya mambo kama hayo hakuna
sheria.
Mtazamo sahihi mbele ya Mungu:
Zaburi ya 111:10 kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima, wote wafanyao hayo
wana akili njema, sifa zake zakaa milele. Tukisoma Marko 12:30 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na
kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwan nguvu zako zote. Yohana
14:15 mkinipenda, mtazanishika amri zangu. Yakobo 4:7 Basi mtiini Mungu.
Mpigeni Shetani, naye atawakimbia. Mtazamo wetu lazima heshima, utii, upendo, uaminifu, unyenyekevu,
utii, worshipful, na sala.
Mtazamo wetu kuhusu watoto wa Mungu Yohana 13: 34-35 Amri mpya
nawapa, mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
Warumi 12:10 kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza
wenzenu. Wakolosai 3: 16 Neno la kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika
hekima yote, mkifundishana na kuonyana
kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa
neema mioyoni mwenu. Waebrania 3:13 lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo
leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa
udanganyifu wa dhambi.
Mtazamo wetu kuhusu watawala wa dunia unatakiwa wa kuheshimu mamlaka, kushirikiana na mamlaka,
kuwajibika ipasavyo, kuwa wenyeneyekevu, kutoa msaada unaotakiwa, kuhimizana na
kushirikiana. Waebrania 13:17 watiini wenye kuwaongoza na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama
watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua;
maana isingewafaa ninyi. 1 Peter 2:13-15 Tiini kila kiamriwacho na watu,kwa
ajili ya Bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa; ikiwa ni wakubwa,
kama wanaotumwa naye ili kuwalipizia kisasiwatenda mabaya na kuwasifu watenda
mema. Kwa sababundiyo mapenzi ya Mungu Kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya
ujinga vya watu wapumbavu.
Mtazamo wetu kuhusu
tukipatwa wakati Mgumu tunatakiwa kuwa wapole, watu wa kushukuru na kuamini
kuwa hakuna linaloshindikana mbele ya Mungu. Warumi 8:28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu
hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani wale
walioitwa kwa kusudi lake. Mungu anajua mitazamo yetu ndio maana kila mara
anawatuma wajumbe wake ambao ni manabii katika kutuelekeza katika mitazamo
iliyo bora: Yeramia 1: 17., 19 Haya Basi wewe jifunge viuno, ukaondoke
ukawaambie maneno yote niliyokuamuru; usifadhaike kwa ajili yao, nisije
nikakufadhaisha wewe mbele yao; Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda
maana; maana mimi nipo pamoja nawe, asema Bwana ili nikuokoe. Au alivyoongea na
Ezekieli 2:7 Nawe utawaambia maneno yangu; kwamba watakusikia au kwamba
hawataki kusikia; maana hao wanaasi sana.
Tafakari ya leo inaendelea
kutukumbusha kuwa tunatakiwa twende mbele ya Mungu na Mitazamo yenye, utii,
unyenyekevu, adabu; ya kushukuru na yenye kuomba msamaha. Mungu pekee yake
ambaye anatujua na tabia na mitazamo yetu ambayo iko mioyoni mwetu ambayo uzaa
matendo mema au mabaya. Tunatakiwa kutembea katika njia ya bwana ya kumtii, na
kutekeleza yale yote anayotuma kufanya au yale ambayo tayari yamekwisha ainishwa
katika vitabu vyake na mafundisho yote ambayo Yesu alitufundisha.
Hii ndio tafakari
yetu ya leo. Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment