March 1
Tafakari ya leo tuangalie
wazo nzima la kuwa Mungu ni mwanga na ndani yake hakuna giza. Kwa msingi huu
kama sisi tunajiona kuwa tuna ushirika na Mungu hivyo nasi tunapaswa kutembea
kwenye mwanga na kuishi kulingana na maelekezo ya Mungu ambayo ni ukweli.
Tukisoma 1Yohana 6-7
tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tena tukienenda gizani, twasema
uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli; bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo
katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi na damu yake Yesu, Mwana wake
yatusafisha dhambi yoye.
Tukumbuke kuwa kwa dhambi
zetu tulikuwa gizani lakini kwa kifo cha Mkombozi wetu msalabani Damu yake
imetusafisha na kutuondoa katika giza la dhambi ambalo limetuzunguka kwa siku
nyingi sana; tatizo letu wanadamu pamoja na kazi kubwa ya Bwana wetu Yesu Kristo
kutufia bado tunakawaida ya kurudi katika dimbwi la dhambi na hivyo kuendelea
kutembea katika giza.
Tafakari ya leo
inatukumbusha kwa mara nyingine tuache kutamani kutembea katika giza bali tutuembee
katika mwanga wa kweli tukibadilisha matendo yetu; swali la msingi je tuko tayari kuziacha
dhambi zetu na kumrudia Mungu?
Tukisoma kitabu cha
Mithali 1:7 kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, bali wapumbavu huhdarau hekima
na adabu. Maonyo dhidi ya kushirikiana na waovu.
Tunapotembea katika mwanga
wa Mungu huko tunapata ukweli, amani na matumaini. Tunajua kazi ya mwanga katika maisha yetu. Na
tunajua madhara ya giza katika maisha yetu. Nuru au mwanga ni jambo au kitu
ambacho sisi binadamu wote tunakihitaji kwani mwanga utusaidia sisi kufika pale
tunapotaka kufika bila matatizo au bila kupata shida yoyote ya kupapasa au
kujikwaa. Lakini tunapotembea katika giza mashaka hutawala, uhakika wa kufika
safari yetu salama hutoweka, kwani huna ukakika pale unapokanyaga ni mahali
sahihi hivyo tunaishia kujigonga, na hata kutumbukia kwenye korongo.
Tafakari ya leo inatukumbusha
kuwa Giza limejaa vitisho, giza linasababishamsongo wa ubongo, giza linakwamisha uwezo wako wa kufikia
lengo. Kinyume chake ukitembea kwenye mwanga unafanikiwa kufikia malengo
haraka, mwanga unakupa amani, mwanga unakupa afya njema, mwanga unakusaidia
kuona kilicho cha hatari mbele yako. Kwa kweli mwanga ni chanzo cha uhuru na
furaha. Hivyo ukitembea katika Nuru ya Bwana mateso yote yatokanayo na giza
kwamwe hayawezi kukusumbua.
Tafakari ya leo
inatushauri kuwa ili kuishi katika furaha ya kweli lazima tupate kibali cha
Mungu kupitia mwanga wake, bali tukiendelea kulikumbatia giza kamwe hatutuaweza
kupata furaha hiyo. Kwani yeye ndiye njia ya uzima na lazima tupitie katika
njia hiyo kwani ndio njia pekee ya uhakika na hiana mashaka hata kidogo hivyo
mwanga ni tumaini la kweli katika furaha ya kweli. Yakobo 4:4 Enyi wazinzi,
hamjui kuwa ya kwakba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila
atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.
Tunaposema kutembea kwenye
mwanga maana yake ni kuishi kulingana na maelekezo na utawala wa Mungu na sio
wa kidunia Tunatakiwa kuona vitu jinsi mungu anavyoona na kutekeleza kadiri ya
maelekezo yake. Mathayo 6: 22-23 Taa ya mwili ni jicho basi jicho lako likiwa
safi, mwili wako wote utakuwa na nuru. Lakini jicho lako likiwa bovu. Basi mwili
wako wote utakuwa na giza. Basi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza
hilo. Utawala wa giza ni utawala ule ambao ni kinyume na matendo mazuri ya
mungu
Tafakari ya leo
inatufundisha kuwa Giza linatutenganisha na neema ya Mungu: tukumbuke kuwa
Mungu ni NURU na ametukaribisha sote katika kuipokea na kuifurahia hii nuru; tukumbuke
kuwa pale tunapokubali kutembea katika mwanga wa bwana uwepo wake unatemebea
nasi daima; Mungu daima hutuongoza tupitapo, tatizo letu tunajifanya tunajua
njia ya kupita wakati kumbe sio kweli hivyo tunaishia kwenye giza; Zaburi ya 27:1 bwana ni nuru yangu na wokovu angu,Nimwogope
nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu ,
Nimhofu nani?
Tunakumbusha kuwa giza ni
matendo yote yanayopingana na maelekezo au utendaji mzuri wa Mungu juu yetu;
tumepewa akili ili tuweze kufikiri na kutenda vile Mungu anavyotaka sisi
tutende ili tuyafurahie maisha ya hapa dunia na kasha mwisho wa safari yetu
huko Mbinguni. Giza huaribu akili zetu na utusababishia sisi kupata tabu ya
milele.
Tukumbuke Habakuki 1: 13
wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama
ukaidi, mbona unawangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu
ammezapo mtu aliye mwenye haki kuliko yeye.
Tafakari ya leo
inatusisitizia kuwa tunatakiwa tusimame upande wa Mungu na kumtumikia yeye kwa
ukweli ili kufanana na mwanga aliotujalia. Tunapaswa kuwa wakweli kwa matendo
yetu na kukiri kuwa giza halina nafasi katika maisha yetu Amen.
No comments:
Post a Comment