Kutoka:20:12
March 10
Tafakari ya leo
tunaangalia wajibu wetu kama watoto kuwapenda kuwajali wazazi wetu; hili sio
ombi ni sheria ambayo Mungu ameiweka katika kitabu chake ambacho ndio mwongozo
wetu katika maisha yetu ya kila siku ya ukristo wetu. Kama tunavyo soma katika
kitabu cha kutoka 20:12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa
nyingi katika nchi upewayo na Bwana,
Mungu wako.
Hata katika 2 Timotheo 1-2
inatukumbusha kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu
wakuwa wenye kujipenda wenyewe, na kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi,
wenye kutukanana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio wasafi;
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa tunatakiwa kuwaheshimu wazazi wetu, na sio kuwaheshimu,
viongozi wa serikali, au walimu au marafiki, wafanyakazi wenzetu bali wazazi
wetu; siri kubwa hapa ni kuwa tukiweza kuwaheshimu wazazi wetu, tukifanya
hivyo mahusiano mengine yote yatakuwa
rahisi katika kuyatekeleza. Heshima inaanza nyumbani; kama huwezi kuwaheshimu
watu wa nyumba yako utawezaje kuwaheshimu watu wengine wa mbali? Ndio maana
shetani anafanya jitihada kubwa ya kuharibu uhusiano mzuri kati ya Wazazi na
watoto ili wasitimize adhima yao kutekeleza amei hii ya Mungu bali tuangamie;
Tafakari yetu leo hii inatukumbusha kuwa jinsi tunavyoweza kuwaheshimu na kuwapenda wazazi wetu ndivyo
itakavyo kuwa rahisi kwetu kumpenda na kumheshimu Mungu. Huu ni muhimili mkubwa
sana katika maisha yetu; wazazi ni kiungo muhimu sana kati yetu na Mungu na wao
wanamwakilisha Mungu hapa duniani. Hapa ndipo wazazi wetu wanatakiwa kuwa
makini kwa sababu Sisi watoto tunafahamu kwa wao ndio wawakilishi wetu wa
kwanza hapa duniani na jinsi taswira ya matendo yao kwetu inakuwa aina ya Mungu
ambaye sisi tunamwona kupitia kwao.
Kama wazazi wetu hawawezi kuonyesha mfano mzuri wa maisha yao kwa
watoto; sisi tunamjua Mungu wetu na Hulka zake; je sasa mungu tunayemwona
kupitia kwao ni Mungu wa upendo, neema, wa msahama, mafanikio? Au Mungu tunayemwona
kupitia kwao anageuka kuwa Mungu wa Tamaa za mwili, Uzinzi, hasira, wizi, mkatili,
mnyanyasaji na kadhalika?
Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa Baba na Mama wamepewa nafasi kubwa sana
katika maisha yetu; na tunatakiwa kuwaheshimu wote katika uzito sawa. Ni wajibu
wetu kuwatii na kuwaheshimu kwani Mzazi mwema hatakuwa sababu ya wewe ufanye
dhambi yeyote ile. Waefeso 6: 1-3 Enyi
watoto watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki: Waheshimuni baba yako na mama yako; amri hii
ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, upate heri, ukae siku nyingi katika dunia
Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa tunatakiwa kuonyesha adabu kwa wazazi
wetu tunapoongea nao hasa kwenye hadhara ya watu na hasa mbele ya watoto wetu;
hata kama hatukubaliani nao yale wanayosema bali tunaowajibu wa kuonyesha adabu
na uvumilivu. Tukumbuke kuwa jinsi ambavyo tutakuwa tunawawatendea wazazi wetu
ndivyo hata watoto wetu watakavyo
tutendea.
Tafakari ye leo inatukumbusha kuwa Mungu ndio asili ya uhai wetu lakini
wazazi wetu ni kiungo muhimu ambacho Mwenyezi Mungu alikichagua katika kutuleta
sisi duniani. Tunafahamu kuwa kuna baadhi ya wazazi kwa kweli wao ndio wanakuwa
waaribifu wa maisha ya watoto wao.
Lakini bado kama watoto tunatakiwa tuwaombee na wapate msamaha wa Mungu lakini
bado tunawajibu wa kuwaheshimu.
Mungu anajua machungu yote ya nyuma lakini anangalia leo yetu na kesho
yenye faraja katika maisha yako. Ndio maana anatuambie leteni mizigo yenu
kwangu name nitibeba kwa ajili yenu. Tukumbuke kuwa pamoja nay ale yote
yaliyotokea katika maisha yetu bado sisi ndio pekee tutayoyajenga maisha yetu.
Hivyo itakuwa vyema kama tutaweza kuishi maisha yenye uadilifu, mafanikio na
furaha ya kweli na wazazi wetu watutupenda kwa hilo.
Tunafahamu kuwa wakati mwingine inakuwa vigumu kutekeleza amri ya msamaha
dhidi ya wazazi wetu kwa makosa yao ya makusudi na kusababisha kukosekana kwa
upendo kati ya watoto na wazazi kama tatizo, la utoaji mimba, ubakaji na
kadhalika; matendo kama haya hupoteza kabisa upendo wa mzazi kwa motto; hivyo mtoto
anakua katika maisha hatarishi na mtoto anajenga hasiri ya kulipiza kisasi cha
kutaka kuua na kuwa huru kutoka katika minyororo ya wazazi wa namna hii. Mara
nyingi tunawaona wazazi wetu kama vikwazo katika maisha yetu na sio kisima cha
busara cha kutusaidia sisi kusonga mbele.
Ndio maana mwenyezi Mungu anatukumbushga leo katika mazingira ya namna yeyote
yale bado tunawajibu wa kuwaheshimu wazazi wetu na kuwaombea kwa Mungu. Huku
tukiwasamehe dhambi zao. Mungu alipoweka hii amri ya kuwaheshimu wazazi wetu
alijua kabisa wazazi ni chanzo cha familia na nyumba ndio msingi mkubwa wa jamii
na jumuia zetu; na hakuna jumuia zetu zinataweza kuwa na msingi imara kama
hatutakuwa na familia bora ambazo zinajenga jumuia hizo; kinachofanyika
nyumbani ndicho kinachofanyika katika jumuia zetu;
Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa tukiyaangalia maisha yetu huko nyuma
tunaona kuwa tumekuwa watoto ambao kwa namna moja au nyingine hatukuwapa
heshima inayotakiwa kwa wazazi wetu, tume waonyesha kiburi, dharau na hata kuto
fuata ushauri wao. Lakini bado ninakila sababu leo kusema asante sana Mungu kwa
kunijalia wazazi ambao wamenilea na kunifikisha hapa nilipo leo. Ni ukweli kuwa
katika namna moja au nyingine pengine hatukubaliana nao katika baadhi ya mambo;
na pengine walitutendea vibaya lakini yoye ya yote tunatakiwa kuwasamehe ili
tuweze kutembea katika amri hii ya Mungu tunatakiwa kuwaheshimu wazazi wetu na
kuwapenda. Hii ni amri na wala sio ombi na hatuna njia ya kukwepa amri hii. Wazazi
wetu wanastahili heshima kwa upendo wote ambao tunastahihi kuwapa.
Hii ndio tafakari yetu ya leo. Ameni
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment