March 7
1 WAKORINTHO 12: 1
Tafakari ya leo
tunaangalia jinsi ambavyo tumejaliwa karama nyingi za kiroho na utumiaji wetu;
Mtume Paulo anatutabanaisha kupitia waraka kwa Warumi 1:11-12 kuwa natamani
sana kuwaona nipate kuwapa karama ya
rohoni, ili mfanwe imara. Yaani tufarajiane mimi na ninyi kila mtu kwa imani ya
mwenzake, yenu na yangu. Kwa ujumbe huu kutoka kwa Mtume paulo karama ya kiroho
kazi yake ya kwanza ni kuwaimarisha
wengine. Je karama yako inasaidiaje uimarishaji wa imani ya mtu mwingine? Huluka ya ubinadamu wetu uko
zaidi katika kubomoa na sio katika kujenga au kusaidia wengine.
Tafakari ya leo inatuuliza
karama ni nini? Tukisoma 1 Wakoritho 7 inatufafanulia kuwa karama ni ufunuo wa
Roho; Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. Ni kitu ambacho
Roho ukiweka wazi; kinangara katika maisha yako na wengine, ni ufunuo ambao
umejaliwa kwa ufupi nu ushuhuda ambao Roho ameufunua kwako kuwa yeye anafanya
kazi ndani ya Mwili wako ili kutenda mema au kuleta amani ambayo Mungu amekusudia.
Tunafurahia sana kuwa
sehemu ya walalamikaji, wachonganishi, wambea, kuhukumu kuliko kuwa tayari kujenga
mahusiano mazuri miongoni mwetu. Kipimo kikubwa kabisa cha karama ya kiroho, ni
unyenyekevu na kuwa tayari tuamkapo asubuhi kumshukuru mungu kwa kuimarisha karama yako na
kuitendea kazi nzuri kama ipasavyo kutumika.
Kama waraka kwa Wagalatia
3:5 basi yeye awapaye Roho na kufanya
miujiza kati yenu, je Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? Waroma 12: 6-
8 Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa;
ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya Imani; ikiwa huduma tuwemo katikahuduma
yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; mwenye kuonya katika kuonya
kwake; mwenye kusimamia kwa bidii, mwenye kusimamia kwa bidii,mwenye kurehemu,
kwa furaha. Sifa za Mkristo.
Tukumbuke Musa alivyowaambia wana wa Israeli kwenye
kitabu cha kumukumbu la sheria 8:17 hapo usisema moyoni mwako nguvu zangu na
uwezo wa mkono wangu ndio ulio nipatia utajiri huo. Musa anatuambia kuwa tusiwe
na tabia za kujisufu wenyewe kwa mafanikio ambayo yana nguvu na mkono wa mungu
kupitia karama zake kwetu. Jukumu letu la msingi kwa karama ambayo umejaliwa
unatakiwa kwanza uitumie kwa aji li ya utukufu wa Mungu, na kama tutaweza
kuzitumia karama zetu vizuri katika jamii yetu na nafasi ambazo tumepewandani ya jamii yetu, basi
tusitegemee kuwa na viongozi wabadhilifu wala rushwa au wazembe; kwani Miongozo
ya mungu iko wazi kwetu ni ya
uadilifu na upendo wa ajabu kwetu wenyewe
na kwa jamii yetu nzima.
Tunasoma kutoka 1Peter
4-10 kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama utumieni kwa kuhudumiana; kama
mawakili wema wa neema balimbali za Mungu.
Mtu akisema na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akihudumu na ahudumu kwa
nguvu anazojaliwa na Mungu na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa
Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata
milele na milele. Amina
Karama ambazo mwenyezi
Mungu ametujali ziko katika utumishi mbalimbalikama unabii Waroma 12:6 basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali,
kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii tutoe unabii kadiri ya imani kwa
kuwajenga kuwafariji na kuwatia Moyo. Karama ya huduma kama waraka wa waroma
12:7 unavyotufundisha kuwa ikiwa huduma,
tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake.
Karama ya kufundisha naye
aitoa wengi kuwa mitume na wengine kuwa manabii na wengine kuwa wainjilisti na
wengine kuwa wachungaji na waalimu. Swali ambao mtume pauloali uliza kuwa je
wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni walimu? Wote watenda miujiza? Karama
ya kufundishi ni muhimu kwa vile inaeleza kwa ukweli na uwazi kuhusu ukweli
kuhusu Mungu ili kuwasaidia wengine kujifunza pia. Karama ya kutoa ni uwezo wa
kutoa kwa moyo na kwa upendo kwa sifa na utukufu wa mungu kwa wale wote ambao
wana shida na uhitaji.
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa karama yako ndio ufunguo wa mafanikio yako; na tunapotumia karama
zetu kwa utaratibu ambao Mungu ametujalia sio tu kuwa ulimwengu utafurahia bali
neema itarudi kwako. 1 Timotheo 4: 14-15 usiache kuitumia Karama ile iliyomo
ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono ya wazee. Uyatafakari
hayo; ukae katika hayo; ili kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu. Tukumbuke kuwa
Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka. Ni zawadi toka
kwa mungu kwako la msingi tunatakiwa kutambua je ni karama gani Mungu
amekujalia?
Waraka wa mtume Paulo kwa
Wagalatia 3:5 unatufafanulia vizuri sana
kuwa Bais, kama yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je Anafanyahayo
kwa matendo ya sheria au kusikia kutokana na imani? Miujiza ambayo hufanyika
katika imani hudumisha na ukuza imani yaw engine ndilo jambo ambalo karama
hutenda. Je karama yako unaitumiaje? Je unaijua Karama yako kwa kazi ya Mungu.
Je unaweza kuomba Mungu akuonyeshe Karama yak oleo ili utende kazi ya
kuimarisha imani ya watu wengine? Na kwa kufanya hivyo tutaweza kumtukuza Mungu
kupitia Bwana wetu yesu kristo ambaye yeye alituonyesha kwa matendo namna ya
kutumia Karama hizi kwa sifa na utukufu wa Mungu.
Tumwombe leo Mungu atufulie
karama zetu kuptia roho Mtakatifu ili tuweze kutekeleza wajibu wetu kwa
kuimarisha imani yetu na kwa wenzetu, tukijua kuwa Pamoja naye; katia yake and ndani yake hakuna kinachoshindikana tukijua
kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uwezo wake, tena vinarejea kwake. Utukufu
unayeye milele na milele amina.
Hii ndio tafakari yetu ya
leo. AMINA
No comments:
Post a Comment