March 16
Yohana 15: 14-15
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa tunatakiwa kutumia muda wetu mwingi kuongea na Mungu, kwani
Mungu ni msikilizaji mzuri sana na hutupa majibu ya maombi yetu. Tunavyoongea
na Mungu ni sawa kama tunavyotumia simu katika mawasiliano yetu ya kawaida.
Tunavyoongea kwenye simu hatumwoni mtu mwingine kutoka upande wa pili ili
tunasikia tu sauti hivyo jukumu letu katika mawasiliano ni kuongea na
kusikiliza. Hivyo uhusiano wetu na Mungu ni sawa hivyo hivyo. Tunaongea na Mungu
kupitia sala na tunamsikiliza Mungu
kupitia mafundisho ya bibilia kwenye jumuia zetu, nyumba za ibada na katika
masifu mbalimbali. Yakobo 5:16 uangameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na
kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa
bidii.
Yohana 15: 14:-15 ninyi
mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. Siwaiti tena watumwa; kwa maana
mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote
niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu. Yesu ametoonyesha hapa kuwa yey ni
rafiki bora kwani amekuwa msikilizaji mzuri katika maongezi yake na Mungu, kisha
ameweza kutuletea sisi ujumbe wa neema kwetu. Asingekuwa msikilizaji mzuri
asingeweza kutufahamisha sisi habari njema toka kwa Mungu. Hivyo Mungu ni
msikilizaji mzuri sana tunapoongea naye. Mungu anapenda nasi tuweze kuwasiliana
naye katika shida zetu na katika mafanikio yetu yote. Hata pale tunaposhindwa
katika mahangaiko yetu Mungu anapenda sisi tuongee naye na tumpe taarifa. Na jambo
nyingine Mungu anapenda sana sisi tumtarifu mipango yetu kabla hata hatujeanza
kufanya. Pale tunapotaka kununua chochote tumshirikishe Mungu kwani yeye yuko kutuongoza; pale tunapokuwa na
mipango ya kusafiri tuongee naye kwani yeye atatembea nasi na atatuongoza. Hata
katika maamuzi yetu magumu tuongee na Mungu yeye atatuonyesha njia ya kufikia
utekelezaji wa maamuzi yetu.
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa Mwenyezi Mungu
ametuagiza tunapongea naye na kumweleza shida zetu, mafanikio yetu au pale
tunapoomba msaada hataki sisi tuwe wanafiki hata kidogo; Mathayo 6: 5-7 ; tena
msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama
katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin
nawaambia wamekwisha kupata thawabu. Bali wewe usalipo, ingia katika chumba
chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako
aliyesirini; na baba yako aonaye sirini atakujazia. Nanyi mkiwa katika kusali
msipayuke payuke, kama watuwa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa
sababu yamaneno yao kuwa mengi.
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa tunapoongea na Mungu tunatakiwa tufanye mazungumzo yetu
kupitia sala kwa ufasaha kama tunavyongea na rafiki yako mpendwa na
unayemweshimu; kwani unapongea na mtu unayemweshimu huwezi tumia menono ya
kihuni ya kimtaa mtaa; au kwa sauti ya juu ambapo hata hamwezi kusikilizana;
kwa misamiati migumu ambayo hata mwenyewe unapata tabu kuikumbuka; hutaki kumhdaririsha hata kidogo hata watu
wengine wakikusikia ukiongea wafurahie mazungumzo yenu. Ni wazi kuwa kwa
kuongea kwa namna hii mwenyezi Mungu atakujibu maombi yako mara moja bila
kuchelewa.
Tafakari yetu leo
inaendelea kutukumbusha kuwa tunatakiwa sana tuisome bibilia na kuielewa ili
hata tunapoongea, kumsifu au kuomba msaada kwa Mungu tuwe tunajua mwongozo wa
namna ya kuongea naye. 1 Petro 3: 15 Muwe tayari siku zote kumjibu kila mtu
awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu. Na
tutaweza tu kuwa tayari kama tutaweza kulielewa na kulishika neno la Mungu; na
hata tutakapo kuwa tunaongea naye tutakuwa katika nafasi nzuri. Na ili
tuendeleze mahusiano mazuri na Mungu tunatakiwa tutumie muda wetu wa kutosha nay
eye, inaweza kuwa kwa kusali pamoja na familia, kusali pamoja na wanajumuia
wengine au kwa kusali pekeyako na kwa kufunga Mathayo 6:16-18 tena mfungapo
msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao,ili
waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin nawaambia, wameshakwisha kupata thawabu
yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na
watu kuwa unafunga, ila na Baba yako
aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazia. Yesu hapa anatufundisha
kuwa mfungo hutufanya sisi kuwa karibu
zaidi na mungu lakini kama tutaufanya
katika unyenyekevu Mkubwa
Tukumbuke kuwa mahusiano mazuri yanjengwa katika msingi wa
uaminifu; najua hakuna Ndoa yeyote
itadumu au kuwa na mafanikio bila wanandoa kuaminiana; mahusiano ya maisha yetu
yanajengwa katika kuaminiana na sio katika sheria. Tunajifunza kwa walimu wa
kanisa na wanasheria wakati wa yesu kila kitu chao kilikuwa kimejengwa katika
sheria, sheria, sheria. Yesu alituonyesha sisi muhimu wa kuwa waaminifu katika
kutekeleza majukumu yetu mbele ya Mungu. Mungu anaitaji Kuwa na Imani na kuwa
waaminifu katika kutekeleza maelekezo yake; kwa Imani na Kuamini tutamweka
Mungu Mbele katika majukumu yetu. Waebrania 11:1 basi Imani ni kuwa na hakika
ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya
mambo yasiyoonekana. Waebrania 11:6 Lakini pasipo imani haiwezekani
kumpendeza; Kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yey yuko, na
kwamba huwapa thawabu wale wamfuatao.
Tafakari yetu inatukumbusha
kuwa Kuamini ni sawa na Barabara mbili. Ni lazima tumwamini Mungu na Mungu
Mungu lazima atuamini sisi, tukizingatia kuwa Mungu ni Yule Yule Jana, leo na
Kesho. Mungu ni mwaminifu na wala hatabadilika hata kidogo.
Yesu alituonyesha kupitia agano
jipya maisha yake na mawasiliano yake na Mungu hakuwa unazingatia sana sheria Fulani,hata
wafuasi wake daima walikuwa wakimwangalia na walikuwa wakishangaa jinsi
alivyokuwa akiongea na Mungu kwa utulivu na kwa amani kubwa.
Tukumbuke kuwa mara nyingi tunavyoongea na Mungu tumekuwa watu ambao tunamwogopa tukifikiri kuwa Mungu hutisha, anahasira na sio rahisi kumridhisha; Lakini Yesu ametufundisha kuwa Mungu ni Rafiki yetu wa ajabu na ndio kimbilio letu la kudumu na Mungu anapenda sana kutumia muda wake mwingi nasi kupitia sala zetu na masifu katika ibada zetu;
Tafakari Ya leo inatushauri kuwa tuondoe vikwazo
tulivyojiwekea tunavyoongea na Mungu ili tuendelee kuona uzuri na wema wa Mungu
wetu; tunatakiwa tuimarishe mahusiano yetu na Mungu kwa kufuata mafundisho na
maagizo yake kama tulivyoelekezwa na Bwana wetu yesu kristo.
Tafakari ya
leo inatufundisha kuwa Katika maisha yake Hapa duniani Yesu alikuwa rafiki wa
kila mtu alikunywa na wenye dhambi, wakasema , mlafi huyu, na
mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Yesu aliwapenda watoto;
aliwajali Malaya alipokuwa akiwafundisha kuhusu wokovu ili waachane na dhambi
zao na wamrudie mungu; watoza ushuru, wenye dhambi, mwana mpotevu, mwanamke
msamalia; na mwanamke ambaye alifumaniwa akizini na ambaye alitakiwa apigwe na
mawe mpaka kufa lakini aliyaokoa maisha yake; yesu alimpenda kila mtu hata
walimu wa sheria ambao wao walikuwa adui wakuu wa Yesu. Jambo la msingi tunatakiwa tuimarishe
mawasiliano yetu na Mungu Kupitia sala.
Hii ndio Tafakari yetu ya
Leo Amina
No comments:
Post a Comment