March 5
Romans 12:20
Tafakari ya leo
tunaangalia maadui wa kiroho ni nani katika maisha yetu? Pengine maadui wa
kiroho si maadui bali na nani? Ninaposhambuliwa na adui wa kiroho katika maisha
yangu ya Kiroho na kuniumiza kwa wakati huo huo wananisaidia kupata neema ya
uvumilivu kutoka kwa Mungu. Tukisoma Mithali 27: 6 Jeraha utiwazo na rafiki ni
amini; bali kubusu kwa adui ni kwingi sana.
Tafakari yetu
inatukumbusha kuwa adui yetu anaweza kuwa rafiki mzuri wa kiroho kwani kwa
maumivu ambayo atakupatia yanaweza kukupa wewe saburi katika maisha yako ya
kiroho, anaweza kuwa msaada mkubwa kwa wewe kuanza kujitathimini na kuwa karibu
zaidi na Mungu kwa maumivu yake kwako. Ndio maana yesu alitufundisha tuwapenda
adui wetu. Tukisoma Luka 6:27 lakini nawaambia ninyi mnaosikia, wapendeni adui
zenu watendeeni mema wale ambao wanawachukia ninyi. Ni kweli kabisa ni rahisi
kusoma kuliko kutenda hasa ukiwa katikati ya mtafaruku au maumivu
yanayosababishwa na adui. Nafahamu kabisa haingii akilini kumpenda mtu ambaye
ameharibu maisha yako, je unaanzaje kusali na kumwombea mtu wa aina hiyo? Ni swali
gumu katika upeo wa kibinadamu lakini kwa neema ya Mungu hakuna
kinachoshindikana. Tukumbuke katika safari ya kiroho hatuwezi kulikwepa hili
pamoja na machungu yote, maamuvu yote, tabu zote alizosababisha bibilia
inatukumsha kuwa hatutakuwa hurumpaka tumewapenda adui zetu na Mwenyezi Mungu
atatubariki.
Tafakari yetu leo
inatukumbusha kuwa yatupasa kuwasalimia kwa upendo tunapokutana nao bila
kuwakimbia kuwaonyesha upendo wa Kristo katika uso wako na matendo yako;
tunapaswa kuongea nao vizuri kwa kuondoa hasira na kiburi na chuki ambayo tunayo
kama sehemu ya kulipiza kisasi. Tunatakiwa kuyakubali maumivu ambayo
wamesababisha na kuendelea kuomba neema ya mungu ili kuleta upatanishi wa
kweli. Kwa kufanya hivyo tutakuwa sehemu ya uponyaji wa maaumivu yetu . lakini
wewe au mimi tunatatkiwa kuwa watekelezaji wa kwanza kwa kuondoa daraja la
chuki miongoni mwenu.
Tukisoma Luka 6: 28
tunakumbushwa kuwa wabarikieni wale wote ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale
ambao wanawaonea ninyi. Tunakumbushwa hatuna sababu ya kuwasemea vibaya wale
wote waliowaumiza tukumbuke kuwa kila wakati tunapofungua mdomo mithali 18:21
mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; na wao waupendao watakula matunda
yake. Hivyo tunatakiwa kuomba neema ya msamaha na kupunguza kusema tena na tena
jinsi ulivyoumizwa kwani kwa kuendelea kusema inaleta wakati mgumu wa kusamehe
maumivu yaliyotokea.
Madui ambao nawaongelea
leo ni wale watu ambao daima tupo pamoja, tunaonana kila siku, tunafanya kazi
pamoja, tunasali pamoja na pengine tunaishi
karibu na tayari tumeshajiwekea ukaribu na undugu ambao unazidi urafiki
wa kawaida. Ni wale watu ambao tayari umeshawaamini sana ndio daima
wanaokuangusha na kukuumiza; watu unao wapenda sana wamaweza kuwa ndio sababu
ya anguko lako; marafiki ambao wanaweza geuka kuwa maadui ni kama watoto wako,
wazazi wako, mume au mke wako;
Tafakari ya leo inatuonyesha ugumu wa kutekeleza
hili kwani tunatakiwa kuwapenda japo wametuumiza kwa kiwango chochote kile
wanaweza wakawa wametunyanyasa, wametutesa, na kutuumiza kwa msingi wowote ule
ambao umesababisha kuharibu kabisa mwenendo wa maisha na imani pia. Lakini Bado
yesu anatilia mkazo Mpende adui yako. Tatizo amri hii haiepukiki kwani hii ni
hatua pekee kuelekea kwenye msamaha. Hatuwezi kubarikiwa mpaka tumewasamehe
waliotuumiza. Romans 12: 20 – 21 aduia yako akiwa na njaa mlishe akiwa na kiu
mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe
na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema
Tafakari ya leo inatuasa kuwa tuondoe mawazo
mabaya katika mioyo yetu, hakuna sababu ya kuwa na mawazo mabaya mioyoni mwetu
juu ya wengine, hata kama wewe sio muuaji lakini una mawazo mabaya ya chuki
ndani ya nafsi yako juu ya mwenzako ni sawa tu na kuua. Kama wewe sio mzinzi
lakini unamawazo machafu moyoni mwako yenye mwelekeo huo ni sawa tu ma kuzini.
Tunakumbusha kuwa uadui miongoni mwetu na kuumizana ni kwa sababu tu ya tabia
zetu mbaya ambazo husababishwa na mawazo mabaya ya ubinafsi. Wivu, choyo,
hasira na kutokuwa na hofu ya Mungu.
Kwa hiyo kuwapenda adui zetu haitulazimu sisi
kufanya vile wanavyofanya kwetu, bali kuwaonyesha upendo, kuwaonyesha msamahaa
wa makosa yao; sio lazima tukubaliane nao katika hoja zao lakini kuonyesha
upendo katika majadialaino nao kuwapa maelekezo kulingana na mwongozo wa Mungu.
Adui siku zote ana chuki na anataka akuone wewe unashindwa, unaanguka ,
unaaibika; wanapenda kusambaza sumu uchukiwe, ulipize kisasi na kadhalika.
Tafakari yetu inaonyesha lengo
la adui kuwa wewe uchukiwe na. Hivyo yesu
anatukumbusha kuwa tunaweza kusikitika juu yao au kukasirika kwa matendo yao
lakini bado tunatakiwa kuwapenda. Mithali 25: 21 -22 Adui yako akiwa ana njaa
mpe chakula; tena akiwa ana kiu mpe maji ya kunywa. Maana utatia makaa ya moto
kichwani pake, na bwana atakupa thawabu.
Hii ni tafakari yetu ya leo – AMINA
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment