John
19:28-30
Leo ni Ijumaa kuu ni siku muhimu sana katika ukombozi wetu; ni siku muhimu
sana katika safari ya usindi wa ukombozi wa maisha yetu kama wakristo ambao
tegemeo la ukombozi wetu liko mikononi mwa Bwana wetu yesu kristo; ni siku
ambayo Yesu alisulubiwa msalabani kwa dhambi zetu. Ni siku ambayo maadui wake
walijua kuwa tayari wameshinda vita ya kumwangamiza baada ya kumtesa na
kumdhihaki katika kipindi chote cha mateso na kumsulubisha pale msalabani;
Tafakari yetu leo inatuhamasisha kuwa maadui wa Yesu mafarisayo na wakuu wa
sheria walijua wameshinda na wamemwangamiza Yesu kwa kifo cha Msalabani; wakati
huo huo wanafunzi wa yesu walikuwa na machungu wasijue nini cha kufanya na
walikuwa wamejificha na hawataki kuonekana hadharani; Lakini Yesu baada ya
kusulubiwa msalabani na maandiko kutimia aliinua macho mbinguni na kusema
yametimia; Ni neno muhimu kwa sababu kunaashiria mwisho mafanikio ya hatua
muhimu katika ukombozi wetu. Ni neno hili Yametimia hutumika wakati wa
ukamilifu ulio sahihi wa jambo fulani muhimu. Yesu alilitumia neno hili kwa
kumaliza kazi ngumu ambayo bwana wake waliompa kufanya , alikuwa akisema kwa
bwana - tetelestai - "Mimi kuondokana na matatizo yote ; Nimefanya kazi
kwa kadri ya uwezo wangu na nimelaiza salama kwa mafanikio makubwa ya ukombozi
wa binadamu. Naamini kuwa hakuna neno nyingine bora linaloweza kutuonyesha ukuu wa Yesu.
Tetelestai maana ya kumaliza, yametimia. Ni mara zote neno hili tunalitumia kama furaha na ushindi; Hapa tunasherekea ushindi wa kuishinda dhambi iliyoingia
ulimwenguni kupitia Adamu na Hawa na hitimisho lake ni siku hii ya Leo ya Ijumaa kuu.
Tafakari ya leo inaonyesha kuwa Mungu ni mwenye haki; Yeye pia ni
huruma ; Mungu ametoa njia ambayo tumekombolewa kwa damu mbadala ya mwokozi
wetu Bwana wetu Yesu Kristo. Mwenyezi Mungu ametupenda ametuamini sisi wana
wake kwa kumtoa Yesu kuwa ndio daraja letu la ukombozi: warumi 3: 24-26
wamehesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo
Yesu; ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika
damu yake ili aonyeshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili
wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa; apate kuonyesha haki yake wakati
huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabu haki yeye amwaminiye Yesu.
Tafakari yetu leo inatuonyesha jinsi Mungu alivyotimiza ahadi
ya kufanya malipo halisi ; Kwa kumtoa Yesu mbele kama malipo ya dhambi zetu.Yesu
amekuwa Kipatanisho chetu na Mungu kupitia
damu yake Takatifu; damu pekee ambayo inaweza kweli kulipia dhambi zetu. Hii
ilikuwa ni kuonyesha haki ya Mungu , kwani kwa uvumilivu wake wa Uungu amesafisha
dhambi zote zilizofanywa Kwa kipindi cha
muda kirefu toka kuumbwa kwa dunia , kwa sababu Mungu si mwepesi wa hasira na
mikopo yake iliyojaa huruma iko juu yetu siku zote; hivyo aliamua kutoa Yesu
ambaye alizaliwa kama binadamu awe malipo ya kweli kwa ajili ya dhambi zetu ,
hii ilikuwa kuonyeshaupendo wake kwetu.
Tafakari yetu tunamshukuru Yesu kwa Kilio chake cha ushindi Yametimia; Kwetu Yesu kufa msalabani ni
tendo la ushindi mkubwa sana, kwani alishatueleza kuwa Mwana wa Adamu atapata
mateso makali na kufa msalabani kisha aatafufuka kutoka kaburini na hiyo
inadhihirisha uishinda dhambi na mauti. Na
tukumbuke kuwa sisi ambao tunaamini kuwa Kwa kusulubiwa kwake Krsito tumepata
ushindi mkubwa sana ambao wanaamini, Kristo aliyesulubiwa ni neno la wokovu, ni
neno la ushindi. Na maneno ambayo Yeye anaongea hapa ni kelele za ushindi. Kwa
macho haya si ushindi kelele. Lakini kwa macho ya imani na tukiendela kushukuru
kwani kristo anaishi ndani yetu; hivyo mpango wa Mungu na madhumuni ya maisha
yangu sasa yametimia. Njia ya uvumilivu, unyenyekevu kusamehe na kuto shindwa
hata katika magumu ndio njia ambayo Mungu anataka sisi kuishi nasi mwisho wa
safari hii tuweze kusema kama Yesu alivyosema Msalabani YAMETIMIA;
Leo ni siku Muhimu sana katka maisha yetu kama Mkristo, askari shupavu wa
Yesu; hivyo Mungu anataka wewe kukamilisha na kuishi maisha yetu kama kristo
alivyoishi duniani; kupigana vita vizuri, na tuweze kumemaliza mbio za
kumtafuta Mungu kwa ushindi na kuvikwa taji katika makao ya milele; Kwa ushindi
wa Yesu tumeondolewa dhambi zote na tumelipwa kwa ukamilifu;
Hii ndi tafakari yetu ya leo katika Ijumaa hii Kuu ambayo ni muhimu sana
katika ukombozi wetu kama Wakristo – Amen
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment