April 1
Ephesians 5:23-27
Tafakari ya leo tuna kila
sababu ya kumshukuru Mungu kwa kutujalia kuwa na familia bora na imara kwa
kutajalia mke mwema. Bibilia kupitia Mithali 19: 14 Mke mwema hutoka kwa BWANA;
Kwa fundisho hili la bibilia inatukumbusha kuwa Mungu pekee ndiye
mwasisi wa ndoa ni; tukumbuke alivyomwambaia Adam na Hawa zaeni
mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege
wa angani na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Kwa maelekezo ya
Mungu katika uumbaji wake tunakubaliana kuwa mwanaume na mwanamke ni nguzo
mbili za msingi wa familia, lakini kwa kuwa wanaume wamepewa sifa maalum kwa
amri ya uumbaji, na kwa sababu ya uwezo wao wa mantiki ni imara zaidi ya ule wa
wanawake, wao huchukuliwa kama walezi wa familia zao na vichwa vya familia.
tukisoma 1 Wakorintho 11:3 Lakini napenda muelewe
kwamba Kristo ni kichwa cha kila mwanamume, kama vile mume alivyo kichwa cha
mkewe, na Mungu ni kichwa cha Kristo. Waefeso 5:23 Kwa
maana mume ni kichwa cha mke kama vile Kristo alivyo kichwa cha kanisa, ambalo
ni mwili wake, naye mwe nyewe ni Mwokozi wa kanisa. Ikumbukwe huyu ndiye ana
uamuzi wa mwisho katika familia akiamua kuukana ukristo, kurudi nyuma inakuwa
na athari kubwa sana katika familia. Hivyo hii ndio nguzo ya ndoa ya Kikristo.
Tafakari yetu ya leo msisitizo wetu uko katika
wajibu wa wanaume kwa wake zetu; Ni mwanaume ambaye kwa kutumia busara yake,
anaweza kuisadia familia yake na kutayarisha mazingira kwa ajili ya furaha yao,
na ni yeye ambaye anayeweza kuigeuza nyumba kuwa Pepo na mke wake kuwa kama
Malaika. Busara ya mwananume ni tuzo kubwa katika malezi ya
familia;Mwanaume ambaye anaisaidia familia yake, lazima atambue kwamba mwanamke
pia ni binadamu kama mwanaume. Siri ya ustawi wa familia inategemea na jinsi
mtu anavyomtunza mke wake, na hii ni kama ilivyowajibu wa mke kwa mume wake
ambao unaeleweka kuwa katika kiwango sawa na Jihadi, pia unatambua kama tendo
jema na lenye thamani sana. Lakini mwanaume ajifunze namna ya kumshughulisha
mke wake, katika namna ambayo atageuka kuwa na tabia kama Malaika.
Leo tunakumbushwa kuwa mwanaume lazima atafiti
kuhusu tabia na matakwa ya mke wake. Lazima apange maisha yake kufuatana na
matakwa ya mke wake na mahitaji sahihi. Mwanaume anaweza kwa tabia na msimamo
wake kumshawishi mke wake katika njia ile ambayo inampendeza yeye (mke wake),
kwake yeye mume na nyumba yake. Kama tunavyokumbushwa kutoka katika waraka
wa Waefeso 5:33 Hata hivyo kila mmoja wenu ampende
mkewe kama anavyoipenda nafsi yake. Upendo ni nguzo ya Pili na pia ni moja ya
tunda la Roho katika ndoa.
Tafakari yetu inawauliza
wanaume kama wanajua kuwa mwanamke amejaa wema na ni kiumbe chenye hisia kubwa
sana ya upendo na utunzaji wa nyumba? Tunatakiwa tukumbuke kuwa furaha yake hutegemea
huruma na upendo wa mume wake. Tukiwapenda wake zetu kwa upendo halisi ndivyo
wanavyofurahi zaidi. Kwa hiyo siri ya mwanamume aliyefuzu katika maisha ya
furaha ya ndoa ni jinsi anavyo onesha mapenzi kwa mke wake. 1
Wakorintho 13:4-8 Upendo huvumilia, upendo hufadhili; upendo hauna
wivu au majivuno. Hili ndilo jukumu letu katika kuwapenda wake zetu na hatuwezi
kulikwepa jukumu hili muhimu ili kukamilisha familia iliyo bora. Tukumbuke kuwa
tusipokuwa mwema kwa wake zetu, basi anaweza kupoteza mvuto kwenye nyumba zetu,
halikadhalika na watoto pia. Na zaidi ya yote kwako wewe mwenyewe. Wakati wote
nyumba zetu zitakuwa katika hali machafuko. Mwanamke hubadilika haraka na
hatakuwa tayari kufanya juhudi kwa ajili ya mtu asiyempenda.
Tafakari ya leo inatushauri akina baba kutumia mazuri yaliyo jaa
sifa na hisia kwa wake zetu tukumbuke kuwa maneno mazuri na matamu
ya kuwasifia wake zetu kamwe hayaondoki kamwe hayaondoki moyoni mwao. Kama
mambo yalivyo, mapenzi na huba lazima yawe halisi na kuvutia kwenye moyo wa
mwingine, lakini hata kupenda sana kwa mtu haitoshi, kwa kuwa ni muhimu
kuonesha huba. Kwa kuonesha hisia zako kwa maneno na vitendo vyako, mapenzi
unayoonesha, yatapata jibu zuri kutoka kwa mkeo na nyoyo zenu zitaimarisha
muungano wa mapenzi. Uwe wazi na udhihirishe mapenzi yako kwako bila kusita.
Wakati yupo au hayupo, msifie. Mwandikie barua unapokuwa safarini na mtaarifu
kwamba kutokuwa karibu naye unajihisi mpweke sana. Mara kwa mara mnunulie kitu
kama zawadi. Mpigie simu unapokuwa ofisini au shughuli zako na umuulize hali
yake. Wake zetu wanafurahi tunapowapa heshima iliyojaa upendo Heshima humfanya
mtu ajione unamjali, wanaume wengine atasema anapenda lakini anamwita mwenzie
hajasoma, ametoka familia duni, hafanani na hali yangu, kwakweli huku ni
kumdhalilisha mwenzio 1 Petro 3: 7 – 9 7Kadhalika ninyi
waume, ishini na wake zenu kwa kuwahurumia, mkitambua ya kuwa wao ni dhaifu na
hivyo muwape heshima, kwa maana ninyi ni warithi pamoja nao wa neema ya uzima.
Tafakari yetu ni msingi mkubwa sana wa familia
bora, jamii bora ni matokeo ya familia bora itokanayo na usimamizi mzuri wa
Mume; Marko 10:7 Na kwa sababu hii mume
atamwacha baba yake na mama yake na hao wawili, watakuwa mwili mmoja. Hivyo
nyumba yenu itakuwa msingi wa maisha bora; ijae msamaha tukumbuke kuwa hapana
mtu yeyote hapa duniani ambaye anazo sifa zote na hana makosa. Kwa ufupi,
hakuna mtu ambaye hana mapungufu, na hakuna mtu yeyote hapa duniani anayeweza
kuchukuliwa kama kiumbe kilichokamilika. Kwa kawaida, wanaume, kabla ya kuoa
hudhani kwamba atakaye muoa awe hana dosari yoyote. Hawajali ukweli huu kwamba
hakuna kiumbe kifananacho na malaika hapa ulimwenguni. Wanaume hawa, mara
waoapo huwaona wake zao waliodhani wakamilifu, si wakamilifu na hivyo huanza
kuonesha mapungufu yao. Hudiriki kuona kuwa ndoa zao hazikufuzu na wao wenyewe
kuwa na ‘bahati mbaya.’
Tafakari yetu inatukumbusha
kuwa tuishi katika msamaha wa kweli tusamehe na kusahau, kwa kufanya hivyo
tutakuwa tunatimiza maandiko 1 Wakorintho 13:4-8 5 Upendo hauna
kiburi na haukosi kuwa na adabu. Upendo hautafuti kujipendeza nafsi;
haukasiriki upesi, hauweki orodha ya mabaya. Bali tutajenga nyumba iliyo bora
lakini msingi wote wa Nyumba bora Amepewa mwanaume kuusimamia na kuufanikisha.
Wanaume tunajukumu kubwa na la msingi mkubwa san asana.
Hii ndio tafakari yetu ya
leo – Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment