April 5
Mwanzo 18:9 -15
Tafakari ya leo tuangalie
jinsi imani inavyotuwezesha kutuletea kicheko; na kicheko cha imani ni kicheko
chenye ushindi mkubwa sana; kwani kinakuwa kimejaa matumaini ya Mungu yaliyojaa
ukamilifu wa ahadi yake kwako; ni kicheko ambacho kitadumu katika maisha yako
yote; Tukisoma Hadithi ya Abraham alivyotembelewa na wageni watatu kitabu cha
Mwanzo 18:9 -14 Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo hemani. Akamwambia, Hakika
nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa
kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake. Basi Ibrahimu na Sara
walikuwa wazee, na umri wao mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya
wanawake. Kwa
hiyo Sara akacheka moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na
bwana wangu mzee? Bwana
akamwambia Ibrahimu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa mwana,
nami ni mzee? Kuna
neno gani lililo gumu la kumshinda Bwana? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati
huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume. Akakana Sara, akisema,
Sikucheka, maana aliogopa. Naye akasema, Sivyo, umecheka.
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa pamoja na kicheko cha matumaini lakini Sara aliguna na kuwa
na mashaka juu ya uwezo wake wa kuzaa akiangalia ukuu wa umri wake akiwa
amesahau kuwa ahadi yiho ilikuwa imetolewa na Mungu katika umbo la kibinadamu
kama wageni ambao walitembelea nyumba yao. Sara bado anatuwakilisha sisi
binadamu pamoja na furaha kubwa ya imani
ambayo mungu huwa tayari ametuandalia ili tuweze kuifurahia bado hatuwezi
kucheka au kuifurahia bila kuwa na mashaka katika mioyo yetu. Abraham na Sara
walipata bahati ya kuwa Mungu alikula nao chakula pamoja nao na kutoa hiyo
ahadi nzuri kwa Sara. Tukumbuke kuwa habari njema wakati mwingine hatuzipokei
katika ukamilifu wake.
Katika maisha yetu
tunapopata habari nzuri ambazo tunatakiwa tuzipokea kwa furaha kwa imani yetu
sisi tunakuwa mbali na Mungu na kuanza kuwaza kibinadamu zaidi nakuona kuwa
hili haliwezekani; Ndio haliwezekani katika upeo na maono yetu bali kwa Mungu
hakuna linaloshindikana; Tunatakiwa tubadilike na tubadili uelewa na jinsi ambavyo
tunavyoamini vitu; Tuweke imani yetu mbele na daima tutacheka kicheko cha
ushindi na Bwana. Tukisoma Warumi 4:17 mbele zake yeye aliyemwamini, yaani
Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba
yamekuwako. Luka 1:37 kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.
Tafakari yetu pili inatuonyesha kuwa Sara
pamoja na kuwa na mashaka na maelekezo ya Mungu vile vile alicheka na akijua
kuwa hataweza onekana mbele ya macho ya watu; Lakini Mungu aliyaona matendo
yake na alimuuliza kwani ulicheaka Sara? Naye kwa woga akajibu sikucheka; Mungu
alisisitiza tena kuwa ulichena na kuonyesha wasiwasi moyoni mwako; fundisho
kubwa hapa hatuwezi kuficha matendo yetu au mawazo yetu mbele ya uso wa Mungu.
Tunatakiwa daima kukiri udhaifu wetu na kufanya toba ya kweli. Ndio maana Mtoto
aliyezaliwa aliitwa Isaka maana yake “ Utacheka”
Ni kweli ukiwa na imani utacheka na bwana; katika
mwaka mmoja tu Abraham na Sara walipata motto na wote pamoja walicheka na
kumshukuru Mungu baada ya miaka mingi ya Sara kuwa Mgumba Bwana ameshusha Baraka
zake kwake na kwa familia yake; Tukiwa na imani ya kweli tunaamini katika maono
ya kimungu na tunaondokana na wasiwasi
wa kibinadamu; tunaondokana na mashaka ambayo mwisho wake yanatuangamiza. Hata katika
shida zetu tunatakiwa tumtumaini Mungu na tucheke na Mungu katika imani ikiwa
ni ishara ya ushindi ya shida zetu; tukumbuke kuwa vicheko na furaha daima
vinatuonyesha ni Mungu gani ambaye sisi tunamwabudu kwani mungu wetu ni wa
upendo; hapendi watu ambao wamejaa mashaka na ukiwa na mashaka wasiwasi huwezi
kuwa na furaha. Ndio maana hata Injili ya Bwana wetu Yesu kristo inajulikana ni
habari njema kwa watu wote; ni habbari inayoleta matumaini ya kweli; imeleta
furaha ya kweli; imeleta wokovu wa kweli na faraja ya kweli kwetu sote.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa tunaweza kuwa
na shaka kama Sara kufuatia umri wake mkubwa kuweza kupata motto lakini alijua
kosa lake na alikiri na Mungu akamsamehe na kasha alipata motto katika kipindi
kile kile ambacho aliambiwa ili furaha yake ikamilike. Imani yake ndiyo
iliyompa furaha ya kudumu. Najua sasa hivi mimi na wewe tunamashaka makubwa
sana kuhusu shida zetu na tunalia na shida zetu, tunafadhaika na shida zetu,
tumesahau kuwa tukiwa na imani dhabiti na tukiamini katika nguvu ya msalaba
kamwe hatutakiwi kulia tunatakiwa kucheka kama Sara.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa kwanza tunatakiwa
kutafakari jinsi Mungu alivyotupenda na kutufikisha hapa tulipo leo; tukiweza
kulitafakari hili vizuri hatuna haja ya kuwa na mashaka wakati sauti ya Mungu
ikiongea nasi tunatakiwa kuamini na hivyo kufurahi kwa ushindi wa kushinda matatizo
yetu; Daima vicheko vyetu vinatakiwa view vya ushindi kwa sababu ya Imani yetu
katika uwezo wa Mungu juu yetu; Mungu ni mwaminifu katika ahadi zake; Sara
alicheka sana kwa furaha ya Imani baada ya Kumzaa Isaka motto wa ahadi ya
Imani; najua Mungu anatufanikisha sana katika masha yetu lakini tulio wengi
hatuko kama Sara hatutubu na kumshukuru Mungu na tunajawa na mashaka katika
Imani yetu. Hivyo tunakumbushwa leo kuwa ni wakati mzuri wa kutafakari mapito
yetu ili vicheko vyetu view vya Imani na vitakavyo dumu milele yote kama
tutasikia sauti ya Mungu na kuitii bila mashaka yeyote. Amen
Hii ni tafakari yetu ya Leo
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment