April 29
Isaya 55:8-9
Tafakari ya tunaangalia
dhana nzima ya wokovu kama ni haki yetu. Ukiisoma na kuielewa Bibilia vizuri
inatufundisha kuwa wokovu sio haki yetu bali ni neema ya Mungu tu; tukiangalia
katika nyakati tofauti na kwa matukio tofauti Mwenyezi Mungu alitutengenezea
njia rahisi ya uokovu kwa kuweka misingi mizuri
ambayo alitutaka sisi tuifuate; lakini katika mazingira haya yote kwa
ujinga wetu; kwa kiburi chetu na kwa kukosa maarifa ya kimungu tuliishia
kupoteza neema hii ya Kimungu. Tumekuwa watu ambao hatuishi kwatika kiwango
ambacho Mungu anaweka sisi tuishi. Angali nini Kilitokea katika Bustani ya
Aden;
Tafakari yetu
inatukumbusha leo maneno ya Nabii Isaya 55:8-9
Maana mawazo
yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi,
kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko
mawazo yenu. Maneno haya mazito yanatoka na jinsi ambavyo sisi
tumeshindwa kutembea katika njia za bwana. Tulitayarishiwa makao mazuri ili
tutembee na bwana tumeshindwa kwa sababu ya Kiburi chetu.
Tafakari
yetu leo inatakiwa itukumbushe kuwa tunatakiwa kushukuru kuwa wokovu ni neema
ya peeke ambayo tumeipata na nguvu ambayo Mungu ameiweka ndani yake kwa wokovu
wetu; ni wajibu wetu kuendelea kufanya maungamo ya dhambi zetu katika
kuimarisha hii neema ya wakovu. Ni kweli kuwa sisi sote tumefanya dhambi na
kupungukiwa utukufu wa Mungu. Ndio maana kwa upendo wake Mungu bado ameendelea
kutuokoa kwa neema yake ili tusiingie katika moto wa milele. Huruma na neema ya
Mungu haina mfano sisi ni kama majani yanayopuputika katika mti lakini Mungu
kwa upendo wake anatuokota na kutupa sisi huruma ya ya kimungu ya wokovu.
Pamoja na dhambi zetu bado tumekaribishwa katika uzima wa milele;
Wakovu
wetu u mikononi mwa Bwana kwa upendo wake na huruma yake hataki hata mmoja wetu
apotee wajibu wetu ni kuomba msamaha na kuishi kulingana na njia zake; Je wewe
na mimi tunatumiaje neema hiiya wakovu. Hii ndio tafakari yetu ya Leo
Emmanuel
Turuka
No comments:
Post a Comment