April 9
Yohana 1: 42
Tafakari ya leo
tunaangalia maisha ya Yesu na wafuasi wake hasa mkasa wetu siku ya leo utakuwa
kwa Mtume Petro, ambaye pamoja na udhaifu wake kama Binadamu yeye ndiye alikuwa
msingi wa kanisa la Kristo; tukisoma Yohana 1: 42 Petro alikuwa mfuasi wa kwanza wa Yesu; Naye Yesu
akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri
yake Petro, au Jiwe). Petro
alikuwa na sifa nyingi moja alikuwa msemaji, au mropokaji, alikuwa rafiki wa
karibu sana wa yesu; petro alikuwa mtu mwenye hari kubwa; nguvu za kuwateka
wengine; mwenye msukumo; jambo nzuri yesu aliendelea kumnyosha taratibu ili
kuwa kiongozi mzuri wa Kanisa wa baada yake;
Tafakari ya leo tunaona
kuwa Petro alikuwa ni mtu wa kwanza kukiri kuwa Yesu alikuwa ni mwana wa Mungu.
Petro alikuwa kati ya wale mitume watatu ambao Yesu alikuwa nao karibu sana, na
aliokuwa anafanya nao majukumu mazito ambayo yaliwadhihirishia kuwa yeye sio wa
kawaida. Ni hao watatu ambao walikuwapo Yesu alipomfufua Yule binti wa Jairus
tukisoma Marko 5:37; ni hao watatu walikuwa Yesu alipogeuka sura Mathayo 17: 1 na ni hao watatu walipewa
Jukumu la kuandaa karamu ya Mwisho Luka 22:8
Katika nyakati tofauti
Petro ameonekana mwenye ari ya kufanya jambo kubwa lakini punde anakuwa hana
imani tena na matokeo yake kupoteza lengo; Mathayo 14: 28-29 alipojaribu
kutembea juu ya maji kisha akaanza kuzama;
Alikuwa petro ambaye alitamani wajenge vibanda vitatu baada ya tukio la kugeuka
Sura Yesu lakini aliposikia sauti toka mbinguni aliogopa na kuanguka chini
kujificha. Mathayo 17:4; Ni huyu huyu Petro ambaye alimwita pembeni na
kumkataza yesu asizungumzie Kifo chake
Mathayo 16:22 lakini akasahihishwa na Yesu; Alikuwa Petro ambaye alimkata sikio mtumishi
wa Kuhani mkuu na kasha akaambiwa arudishe upanga wake Alani Yoana 18:10; na
alikuwa Petro ambaye alimwambia Yesu kamwe hatamwancha au kumsaliti Yesu wakti
wote wa Mateso yake. Mathayo 26:33
Tafakari yetu pamoja na mapungufu ya Petro bado Yesu alimpa cheo cha kuwa ndiye mwamba
na juu yake atalijenga kanisa lake; Mathayo 16: 18-19; tunachojifunza katika
maisha ya Yesu, na Petro alipata nguvu
kutoka kwa Yesu pale alipomwambia kuwa anaweza tembea juu ya maji na udhaifu
wake wa imani ndio ulimfanya aanze kuzama; 1 Yohana 4: 18 katika mifano yote
hii Yesu anaelewa udhaifu wetu ambao unatokana na akili zetu na miili yetu ya
kibinadamu; tunakosa nguvu na uwezo wa kufanya au kushawishi nini yatupasa
kufanya kwa haki; yesu alitambua kuwa mitume wake pamoja na Petro walikuwa hawana
nguvu hiyo bado; na hivyo walikuwa hawawezi kuona hata mapungufu yao katika
kutimiza kazi ya kitume pamoja naye;
Katika
tafakari ya maisha ya Petro tunaona kuwa alikuwa jasiri wa kuweza kujaribu
mambo mengi magumu ambayo wafuasi wenzake walikuwa hawawezi kuyafanya;
alimwambia Bwana wetu yesu Kristo kuwa bwana mimi nitakuwa nawe wakati wote wa
mateso yako; ni Petro Peke yake ambaye aliweza kutoa ahadi hiyo; Pamoja na kuwa
hakuweza kuitimiza lakini aliweza kumfuata Yesu katika safari yake ya mateso;
Bahati mbaya tendo la Kumkataa Yesu kuwa hamtambui ni sababu ya udhaifu wa
ubinadamu wetu; hata kama mimi na wewe tungekuwa katika viatu vya peter pengine
tusingeonekana tena mara baadaya kuulizwa mara ya Kwanza. Peter alilia sana
mara baada ya jogoo kuwika kwa sababu alijua kuwa amemsaliti Bwana wake na
Rafiki yake
Je
hadithi hii ya Petro inatufundisha nini sisi; Pamoja na kumwona Petro kuwa na
imani haba lakini aliweza kuthubutu alipomwomba Yesu naye atemebee juu ya Maji
aliweza kushuka kutoka katika Boti na kuanza kutembea lakini hakuweza kuendelea
kuamini kuwa amepewa nguvu na mamlaka ya kutembea juu ya Maji, alipopoteza tu
imani hiyo aliaanza kuzama na yesu akamwokoa. Katika maisha yetu ya kawaida
sisi tumekuwa ni sehemu ya Petro kwani hatusimami kwenye ukweli wa imani juu ya
matendo yetu dhidi ya wenzetu; tu rahisi sana kuacha njia bora ya Mungu kwa
kuangalia makando kando ya mapito ya dunia hii; hivyo bado tunaneema ya
kusaidiwa na mwokozi wetu pale tunapoelekea kuzama.
Je
leo hii katika nafasi ambazo tumezipata za kuweza kuwasaidia wenzetu katika
kumjua Kristo na kuishi maisha ya Upendo tunamtumainije Mungu? Je tunafanya
jitihada gani za kueneza wokovu wa Mungu kwa wenzetu? Je tumekuwa watu wa
kuogopa kulitaja jina la Yesu mbele ya wenzetu? Petro alionyesha mfano mzuri
kwani aliweza kuleta wokovu wa kweli kwa Mataifa hasa yale ambayo yalikuwa
hayamjui kabisa Mungu.
Tafakari yetu inatukumbusha
kuwa hadithi hii ya Petro inatukumbusha kuhusu maanguko yetu ya wakati tofauti
tofauti; kama ilivyokuwa kwa Petro tunajua jinsi vile Mungu alivyoweza
kumsamehe na kumtumia katika njia ya ajabu kwa ajili ya wokovu wa binadamu
ndivyo Mungu anavyotaka kukutumia wewe leo kwa ajili ya taifa lake; Mungu wetu
upendo wake hauna mipaka; neema yake haina mwisho; na msamaha wake ni wa
milele; tujikumbushe kuwa hata pale tunapokuwa tumeanguka tujue kuwa bado
Mwenyezi Mungu anatuweka katika hesabu yake;
Jambo la msingi leo
tunapoyaangalia maisha ya Petro na utumishi wake kwa Krito ni umuhimu wa kusali
bila kuchoka tukiruhusu tu maisha ya sala kufa tujue wazi kuwa tunajitengezea
maisha ya kushindwa katika vita yetu dhidi ya shetani; mafanikio ya kumpigania
Kristo yanapatikana tu kwa kuweka Mungu
mbele katika sala; Hivyo tafakari yetu ya leo inatukumbusha maisha ya sala ni
maisha pekee ambayo lazima tuyapiganie siku zote za maisha yetu. Lakini pale
ambapo hatufanyi jitihada za kumtafuta mungu kupitia sala tujue kuwa tunajitafutia matatizo makubwa katika maisha
yetu; lazima tutembea pamoja naye katika sala kama Petro alivyofanya; Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa hatuwezi
fanikiwa kwa nguvu na uwezo wetu pekeyetu; yesu alimwambia Petro ondoka mbele
yangu shetani wewe kwani alikuwa anataka kuzuia mipango ya Mungu ya wokovu wa
Mwanadamu, nasi tunawajibu mkubwa wa kufanya kwa kudumu katika sala wakati wote
– hii ndio tafakari yetu ya leo Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment