April 25
WAEFESO 4:31,32
Tafakari yetu ya leo tunaangalia ni zao la
chuki na hasara yake katika maisha yetu ya kiroho; tukumbuke kuwa zao la chuki
huzaa hasira na ghadhabu. Tukisoma Waefeso 4:31,32 inatukumbusha kuwa Uchungu wote
na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila
namna ya ubaya; tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheana kama na Mungu katika Kristo alivyosamehe ninyi. Lakini
tukumbuke kuwa sisi sote tumesulibiwa
pamoja na Kristo, hivyo hatutakiwi kukaribisha chuki ndani ya maisha yetu;
Tafakari yetu inaweka sawa kuwa zao la
chuki husababisha hasira ambayo huleta uchungu hivyo Mara
nyingi UCHUNGU husababisha akili kushindwa kufanya kazi ipasavyo. Ni
hali ya kutokuwa na furaha, kujawa hasira zilizotokana na kutendewa mabaya. Ni
hali ya kuhisi huzuni nzito ambayo wakati mwingine inaweza kuchangamana na
maumivu makali katika fahamu za mtu, ambayo yaweza kusababisha mwili
kunyong'onyea na kusababisha akili kupoteza uwezo wa kufikiri vizuri. Bibilia
inatukumbusha kuwa ili kuweza kuondokana na zao hili la chuki basi Wakolosai 3:1-3 basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo,
yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu,
yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.Kwa maana mlikufa, na uhai wenu
umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu
Tafakari yetu pia inatueleza kuwa zao la chuki
pia huleta ghadhabu ambayo nia hali ya mtu kuwa na maamuzi ya
pupa pasipo kujali madhara yake. Hali hiyo yaweza kumfanya mtu kuwa na majibu
ya mkato mkato, kutopenda kuulizwa ulizwa; humfanya mtu kuwa mgomvi na kutopenda
kuwa na subira; Chuki husababisha kuvunja amri za Mungu kwani bila
kutarajia hujikuta mtu kufanya matendo ambayo hayampendezi Mungu kama vile kuwa
chanzo cha matusi; hasira; kukosa upendo ndio maana tukisoama Mithali 22:24-25
inatukumbushja kuwa Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi;
Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi; Usije ukajifunza njia zake; Na
kujipatia nafsi yako mtego.
Tafakari yetu pia inatukumbusha kuwa zao la
chuki husababisha sadaka yako isipokelewe mbele ya madhabau ya Mungu; mathayo 5:23,24 Basi
ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno
juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na
ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako. Tukumbuke kuwa Mungu huchukizwa na
sadaka za mwenye dhambi. Sadaka za mtu mwenye dhambi hazipokelewi mbele za
Mungu. Chuki ni ubaya ambao Mungu haupendi; tukumbuke kuwa ubaya haushindwi na ubaya mwingine, bali unashindwa na
wema - kama vile dawa ya chuki si chuki bali upendo! Ndiyo maana Warumi 12:21
inasema; Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.
Tafakari yetu msisitizo mkubwa ni Chuki huleta
ubaya, na huleta kisasi kwa sababu ya ghadhabu hivyo tunakumbushwa kuwa
hatutakiwi kulipiza kisasi, bali tujiepushe na ghadhabu ambayo ni zao la chuki; Unapoamua kulipa kisasi, unajichumia dhambi! Hii ni kwa
sababu kulipa kisasi huja kwa njia ya chuki iliyojengeka ndani yako kwa ajili
ya mambo mabaya uliyofanyiwa. Huwezi kulipa kisasi bila ya kumchukia huyo
unayejilipizia kisasi kwake. Na Biblia inasema hivi: 1
Yohana 3:15 Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajuaya kuwa kila
mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake. Ni kweli Chuki huzaa kisasi, na
huzaa dhambi ya kuua! Isaya 59:2b inasema; dhambi zenu zimeuficha
uso wake msiuone, hata hataki kusikia.
Tafakari yetu inatutaka kujikosoa wenyewe
na kutubu kwa kujiepusha na dhambi ya chuki tunatakiwa tujenge upendo kwani
Upendo huvumilia, hufadhili, upendo hauhusudu; 1Wakorintho 13:4 – 8 upendo
hautakabari; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii
udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli huvumilia yote; huamini yote;
hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote. Tukumbuke kuwa upendo
huu umo ndani yako, na ndio unaokufanya uwe kiumbe kipya.
Tukumbuke maneno ya Yesu aliposema Mathayo
4:11, 12 Heri ninyi
watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo kwa ajili
yangu. Furahini, na kushangilia;kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa
maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
Hii ni tafakari yetu ya leo ni zao la chuki ni hasira, ghadhabu; na
kadhalika tujiepushe kusongwa na maudhi pamoja na makwazo mbali mbali
yatokanayo na chuki. Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment