April 3
Waefeso 4:32
Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa kwa hakika mwanandamu anahitaji
upeo mkubwa wa nuru ya kiroho ambayo itaweza kumfanya azike tamaa zake na hisia
zote za kulipiza kisasi; tunatakiwa kuwa na uwezo wa kujizuia na
hasira, kuzikandamiza hasira, chuki kwa moyo mpana na kujenga daraja la
msamaha.
Kusamehe mtu ambaye amekukosea,
kuwapenda ndugu na jamaa ambao wameukata uhusiano pamoja nawe, na kuwa mkarimu
kwa yule ambaye aliwahi kukunyima, kukutukana, kukusababishia hasira,kukudharau,
kukudhalilisha na kadhalika sio jambo rahisi. Tumewaona hata watumishi wa Mungu
ambao wanaielewa sana bibilia wakishindwa kabisa kuktekeleza kanuni hii. Kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyofanya pale msalabani, aliwasamehe wote waliompiga, mdhihaki, hata yule jambazi ambaye alisulubiwa pamoja naye alimsamehe dhambi zake na alimkaribisha katika utukufu wa mbinguni.
Kumsamehe yule aliyekutendea yasiyo sahihi
hutusaidia kutupatanisha na Muumba wetu; vile vile msamaha hudumisha mshikamano
wa udugu ambao umeharibiwa. Kwa kusamehe tunaandaa njia ya kumwendea Mungu; Lakini
pasipo imani haiwezekani
(Waebrania 11:6). Inatufundisha kuwa mtu
amwendeaye Mungu lazima aamini
kwamba yeye yuko,
na kwamba huwapa
thawabu wale wamtafutao,”. Msamaha hutujengea wa kumwendea na Kuishi na
Mungu katika Imani.
Kama ilivyoandikwa
hakuna mwenye haki, hata mmoja” (Warumi 3:10). Mungu yuko tayari na anasubiri kumsamehe mtu anaye omba msamaha imeelezwa
katika Zaburi 86:5 "Kama wewe Bwana u mwema, umekuwa tayari kusamehe, na
mwingi wa fadhili kwa watu wote wakuitao". Daudi aliweka wapi tumaini lake
la msamaha? Tukisoma Zaburi 51:1 "Ee Mungu unirehemu sawasawa na fadhili
zako kiasi cha wingi wa rehema zako uyafute makosa yangu. Mathayo 6:14-15 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao na
Baba wenu wa mbinguni atawasamehe ninyi bali msipowasamehe watu makosa yao wala
Baba yenu hatawasamehe makosa yenu." Wale wamesamehewa husamehe.
imeandikwa Waefeso 4:32 "Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye
huruma ninyi mkasameheane kama na Mungu katika kristo alivyowasamehe
ninyi."
Kusamehe kwa kweli hakuhesabu makosa.
imeandikwa Mathayo 18:21-22 "Kisha petero akamwendea akamwambia Bwana
ndugu yangu anikose mara ngapi nami ni msamehe? hata mara saba? Yesu akamwambia
sikwambii mara saba bali hata saba mara sabini." Katika kusamehe Yesu
ametukomboa kutoka kwa dhambi na mshahara wa dhambi. Wakolosai 2:13-14
inatueleza kuwa "Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na
kutokutahiriwa kwa mwili wenu aliwafanya hai pamoja naye akisha kutusamehe
makosa yote akisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake
iliyo kuwa na uwadui kwetu akiondoa isiwepo tena akaigongomea msalabani."
Zaburi 51:7-12 "Unisamehe nami
nitakuwa safi, unioshe nami nitakuwa mweupe kuliko dheluji unifanye kusikia
furaha na shangwe, mifupa ilio ponda ifurahi. usitiri uso wako usitazame dhambi
zangu uzifute hatia zangu zote Ee Mungu uniumbie moyo safi uifanye upya roho
iliyo tulia ndani yangu usinitenge na uso wako wala roho wako mtakatifu
usiniondolee unirudishie furaha ya wakovu wako unitegemeze kwa roho ya
wepesi."
Zaburi 32:1-6 "Heri
aliyesamehewa dhambi na kusitiriwa makosa yake heri Bwana asiyemhesabia
upotovu, ambaye rohoni mwake hamna hila niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa
kwa kuugua kwangu mchana kutwa na kwa maana mchana na usiku mkono wako
ulinilemea jasho langu likakauka hata nikawa kama nchi kavu wakati wa kaskazi
nalikujulisha dhambi yangu wala sikuuficha upotovu wangu nalisema nitayari maasi
yangu kwa Bwana naweukanisamehe uoptovu wa dhambi yangu kwa hiyo kila mtu
mtauwa akuombe wakati unapopatikana hakika maji makuu yafurikapo hayatamfikia
yeye."
Wale walio wanyonge moyo wako mbele ya
Mungu na wala kutambua hatia yangu, haijafika hali ya kwanza ya kukubalika.
Tunahitaji kuokolewa kutoka katika aina zote za tabia zetu mbaya pamoja na
misukumo ya ndani inayotushurutisha kufanya mambo fulani mabaya: kama vile,
kusema uongo, hasira inayomfanya mtu atukane watu, tamaa mbaya za mwili,
uchungu, kutaja machache tu.
Tafakari yetu leo inatuonya kuwa hatuwezi
kujiokoa wenyewe kutoka katika dhambi au kuigeuza tabia yetu kwa kujitegemea
wenyewe kama vile Simba asivyoweza kuamua awe mwana-kondoo (Warumi 7:18).
Dhambi ina nguvu nyingi kuliko nia yetu ya kufanya yale tuyatakayo. Lakini
Kristo anaweza kukufanya wewe uwe "imara kwa uweza wake, kwa kazi ya Roho
wake katika utu [wako] wa ndani" (Waefeso 3:16). Anafanya kazi yake ili
kuondoa tabia zetu ziletazo uharibifu na mahali pake kuweka tabia hizi nzuri:
upendo, amani, furaha, upole, uwezo wa kujitawala (Wagalatia 5:22,23). Kristo
anaishi maisha yake kupitia ndani yetu, kisha tunapokea uponyaji wa kiroho,
tunarejeshwa katika maisha mapya, na kuwezeshwa kuishi maisha hayo mapya.
Hakuna dhambi ambayo ni ya kutisha sana
asiyoweza kuisameka Yesu anatamani sana kwamba kila mmoja wetu hatimayeawe na
uhusiano mzuri na Yule aliyemkosea na kumsababishia majeraha ambayo yamejenga
chuki ambayo inahitaji msamaha. Yesu anataka tupokea msamaha na utakaso wa
Mungu ni; katika imani jambo ni rahisi na la maana sana kama tunavyofurahia
kumpokea motto mdogo aliyezaliwa na kumkumbatia. Lakini kutokana na ubinadamu
wetu, majivuno, kiburi, masengenyo inatuwia vigumu sana kutoa msamaha wa kweli
pale tunapokosewa, tunakuwa na kiburi ambacho kinatufanya kuona kuwa Yule aliyetukosea
hastaili msamaha wetu; lakini kama tunayafuata mafundisho ya yesu na mifano
ambayo ametutolea katika Bibilia Takatitifu tunatakiwa tuondoe ugumu katika
mioyo yetu na kuuvaa unyenyekevu kama yeye alivyovaa unyenyekevu na kuuvua
Umungu kwa ajili ya makosa yetu, na alikuja kukaa nasi na ametutengenezea
daraja la msamaha ambalo kila mwanadamu lazima alipite ili kuweza kukamilisha
safari yake ya kwenda mbingu.
Hebu jitafakari kwa nini umekuwa na
kiburi cha kushindwa kabisa kumsamehe, jirani yako, ndugu yako ambao
wamekukosea kutokana na ubinadamu wao, usijali amekukosea mara ngapi angalia je
wewe uko tayari kumsamehe wakati wowote ule? Lakini kama umefunikwa ndani ya damu ya Yesu yote yanawezekana kabisa. kwani Damu yake ndio ondoleo la dhambi zetu zote na faraja ya kweli wa maisha yetu bora. Lazima tutekeleze zana ya msamaha.
Hii ndio tafakari yetu ya
leo Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment