Wafilipi 2: 4
APRIL 4
Tafakari yetu ya leo tujiulize
kuwa je kuna serikali yeyote ya kidunia ambayo inaweza kuwa madarakani
bila kuwa na kutumikia rushwa na ufisadi? Tukumbuke kuwa mwisho wa siku
watumishi wa serikali bado ni raia wa nchi husika na zao la taifa husika; Je
kwa mantiki hii viongozi ambao wanaunda serikali wanaweza kuepukana na vitendo
vya rushwa na ufisadi? Je unakubaliana nami kuwa serikali za kidunia zimejaa
rushwa na ufisadi ambao ni ubatili mtupu? Je tunaweza kuwa na serikali ambayo
haina tabia hizi katika dunia hii? Bibilia inatukumbusha kuwa serikali
ambayo haitakuwa na harufu ya rushwa lazima itoke nje ya serilaki za
kibinadamu;
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa serikali za kidunia ambazo hatimaye zinatawaliwa kwa rushwa
na ufisadi, zinasaidiwa kuingia madarakani na raia ambao wanakuwa na malengo
tofauti kwa masilahi yao binafsi; wengine wakijua wazi kuwa endapo serikali
hiyo itaingia madarakani basi haja zao za kukwepa ushuru, au kuendesha biashara
yao bila kufuata masilahi mapana ya nchi yatafanikiwa; hivyo na serikali
itatengeneza mianya ya wao kuendelea kujinufaisha na kuwaacha wananchi wanyonge
masikini katika umasikini wao kwani nguvu nyingi zitaelekezwa kwao. Tumeona
sehemu kubwa za tawala hizi watu ambao ni waaminifu ndio wanaoumia zaidi.
Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa ili tuweze kuangamiza rushwa na
ufisadi lazima nguvu za kutokomeza zianzie kwa viongozi wa juu ambao wamepewa
mamlaka juu ya nchi na Mwenyezi Mungu. Serikali yeyote ile ambayo itakuwa
tayari kupambana na rushwa na ufisadi ujue kuwa itapoteza umaarufu wake; katika
hili bibilia tukisoma Mhuburi 7:20 bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa
duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.
Tafakari yetu bado
inatuongoza kuwa tukiondoa wanadamu ambao sio wakamilifu; Yesu Kristo
ambaye Mungu alimchagua kutawala ufalme wake, hakuweza kushawishika katika yale
ambayo yalikuwa sio sahihi kutenda; Yesu alionyesha hili pale alipokataa
rushwa kubwa ambazo alipewa na shetani juu ya kukabidhiwa utawala wote wa
kinunia na fahari zake kwa kuambiwa kumsujudia shetani Mathayo 4: 8-10
kisha ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha miliki zote za
ulimwengu na fahari yake; akamwambia haya yote nitakupa , ukianguka
kunisujudia; Ndipo Yesu akamwambia Nenda zako shetani, kwa maana uimeandikwa
msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. Katika shida na mateso yote
bado Yesu aliendelea kudumisha msimamo wake ulio sahihi wa kumtumikia Mungu
bila kushawishiwa na mtu mwingine yeyote kwa ukombozi wetu sisi.
Ni ukweli mtupu kuwa nchi
nyingi zinafanya uchaguzi ambao nadharia inaruhusu watu kuwachagua viongozi
ambao wataingia ofisini/madarakani kwa ajili ya kuendesha nchi; lakini ukiangalia
chaguzi nyingi na taratibu za chaguzi hizo hizo ambazo tunaona kampeni
zake nanatawaliwa kwa rushwa kwa kiasi kikubwa sana, hivyo wale wenye
uwezo ndio wanaowaingiza watawala madarakani; hapa nafikiri utakubaliana na
mimi vyama vya siasa ndivyo vinavyoongoza kwa matendo makubwa sana ya rushwa
katika kuhakisha kuwa viongozi tukona vyama vyao ndio wanakuwa washindi ili
waweze kuongoza serikali, hivyo watafanya kila hila ili waweze kushinda.
Tafakari yetu ya leo inawaasa viongozi wetu kuwa ili kuweza kuepukana
na tabia zote za rushwa na kifisadi; lazima watekeleze amri kuu ya upendo
ambayo ni amri ya dhahabu; kile ambacho wewe unataka ufanyiwe mfanyie mwenzako
hivyo hivyo; Mathayo 7:12 Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu; nanyi
watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii. Na ya pili yafanana
nayo, nayo ni hii Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hili kwa viongozi wetu
wengi ambao ndio tegemeo la kuondoa umasikini wa watu wao wameshindwa
kutekeleza hili; wao wanapenda kutendewa vizuri na kundi dogo la watu
waliowaingiza madarakani na kunufaishana wao kwa wao; wameshindwa kabisa
kutekeleza hii Golden Rule.
Kwa msingi huu rushwa na ufisadi unaimarishwa zaidi na choyo ya
mali na ubinafsi wa kujilimbikizia mali; hapa tunaona kuwa viongozi wako tayari
kupokea rushwa mfano kutoka kwa makandarasi, nao makandarasi wanapata nafasi ya
mwanya wa rushwa katika kutumia vifaa ambavyo havina ubora unaotakiwa ili
waweze kujilipa na kupata faida kubwa; kwa msingi huu rushwa na ufisadi utaweza
tu kwisha kama tutaondoka na dhana ya ubinafsi na choyo ya kujitajirisha; kama
Waefeso 4:23 inavyotufundisha na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu:
tunatakiwa kuvua uongo na tunatakiwa kusema kweli daima ili tuweze kuvaa utu
mpya ulioumbwa katika mungu ili kutekeleza wajibu wetu ipasavyo na kuwa na hofu
ya Mungu. Na ujumbe huu kutoka katika waraka wa Paulo kwa Wafilipi 2:4 ni
muhimu sana ambapo anatufundishwa kuwa Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe
bali kila mtu aangalie mambo yaw engine.
Tatizo la tawala za kiduani hata kama wakati mwinginwe wanaweza
patiwa elimu nzuri ya kupambana na rushwa na ufisadi bado viongozi wetu
wanapenda kushiriki katika vitendo vya rushwa. Kwa msingi huu ni vigumu kwa
serikali zetu kupambana na rushwa; tukumbuke mafundisho ya bibilia kuwa watu
wenye uchu wa mali, na waongo hawataingia mbinguni; mara nyingi viongozi wala
rushwa wana hizi tabia mbili ya Uchoyo wa mali na uongo wanapowadanganya watu
wake ili kuhalalisha uovu wao na kikundi kidogo kilicho waingiza madarakani kwa
masilahi yao;
Hii ndio tafakari yetu ya leo Amina
Emmanuel Turuka
Corrupt Government
No comments:
Post a Comment