April 8
Warumi 1: 21
Ni tabia nzuri kila
siku kuanza chochote kwa kumshukuru Mungu kwa wema wake mwingi juu ya maisha yetu na mafanikio yetu; Mwenyezi
Mungu anatupenda sana pamoja na mapungufu yetu yote. Tafakari ya leo inatukumbusha kuendelea kuomba
neema ya kujishusha na kuendelea kuomba huruma ya Mungu. Wema wa mungu kwetu ni
wa ajabu sana kwani ametusamehe dhambi zetu zote; ametubariki kupita ufahamu
wetu; japo tumekumbolewa katika dambi lakini bado sisi tumekuwa wagumu na
tunaendelea kutembea katika dunia iliyo jaa dhambi; Mungu anajua khali za roho
zetu, anajua vishawishi vyote tunavyokumbana navyo. Lakini bado tunawajibu
mkubwa wa kumshukuru kila siku na katika matendo yetu yote.
Tafakari yetu leo
inatuongoza vile vile kusoma kutoka katika waraka wa Mtume Paulo 1Watheselonike
5:18 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika
Kristo Yesu; lakini kama hatutakuwa watu wa shukurani katika maisha yetu
Mtume Paulo katika waraka wake kwa warumi 1: 28-31 anatuasa kuwa Na kama
walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao
zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya;
wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye
kusengenya, wenye
kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye
majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio na ufahamu, wenye kuvunja
maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; hasara ya kutomshukuru Mungu kwa wema
na mafanikio yetu, hutujengea kiburi na kujiona; hutujengea ukosefu wa upendo
miongoni mwetu;
Tukisoma kitabu cha 1 Mambo ya Nyakati 29:10- 15 tunatuonyesha
maana halisi ya kumshukuru Mungu kwani vyote tulivyonavyo viantoka kwake yeye; Kwa hiyo Daudi
akamhimidi Bwana, mbele ya mkutano wote; naye Daudi akasema, Uhimidiwe, Ee
Bwana, Mungu wa Israeli baba yetu, milele na milele. Ee Bwana, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na kushinda, na
enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee
Bwana, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote. Utajiri na heshima hutoka kwako wewe, nawe watawala juu ya
vyote; na mkononi mwako mna uweza na nguvu; tena mkononi mwako mna kuwatukuza
na kuwawezesha wote. Basi sasa, Mungu wetu, twakushukuru na kulisifu jina lako
tukufu. Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa
kwa hiari hivi? Kwani vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe
tumekutolea. Kwani sisi tu wageni mbele zako, na wasafiri, kama
walivyokuwa baba zetu wote; ni kama kivuli siku zetu duniani, wala taraji ya
kukaa hapana.
Tafakari yetu leo
hii inaelekeza kuwa ni tendo la shukrani kwa Mungu huongeza zaidi Baraka tukisoma
Injili ya Luka 17:12 Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana
na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali, wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu! Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani.
Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika. Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku
akimtukuza Mungu kwa sauti kuu; akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa
Msamaria. Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa
wapi? Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni
huyu? Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa.
Tunapomshukuru Mungu
tunadhihirishia ulimwengu kuwa Bwana ni jabali langu, na boma langu, na
mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba; katika ukuu wake ndio kimbilio langu; na
nina kila sababu ya kumshukuru kati ya mataifa, na kuendelea kuliimba jina lake
la shukrani wakati wote.
Tuhitimishe Tafakari yetu kwa ujumbe huu mzito
kuwa Kushukuru sio jambo rahisi, na daima kitendo cha kushukuru kinatoka kwenye
moyo wa mwamini wa kweli ambaye daima anampa sifa yesu za ushindi katika kila
jambo na sio kujipa sifa yeye mwenyewe Warumi 1: 21 kwa sababu walipomjua Mungu
wala hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika
uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Tuatakiwa kujawa na Roho
mtakatifu daima, kwani bila nguvu ya Roho wa Bwana hatuwezi kuwa watu wa
shukrani daima. Najua tunajisahau san asana katika kutoa asante kwa Mungu
wakati wote; Je tunafanya hivyo? Je unawakumbuka wana wa Israeli pamoja na
kutolewa katika utumwa Misri bado walikuwa sio watu wa shukrani; walijawa na
malalamishi na dhihaka juu ya Mungu.
Hii ndio tafakari yetu ya leo - Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment