May 2
1Peter 3:8
Tafakari ya leo inatukumbusha kuhusu umuhimu wa wa kuishi pamoja
kwa upendo na maelewano; kama waraka wa 1 Petro 3:8 unavosema Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye
kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu; kama Waraka wa Waefeso 4: 2-8 unavyoyukumbusha kuwa
sote lazima tuishi kwa upendo na kuwa wamoja tukizingatia kuishi katika unyenyekevu
wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; na kujitahidi
kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani. Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika
tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na
katika yote na ndani ya yote. Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo
cha kipawa chake Kristo. Hivyo
husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa.
Tafakari yetu vile vile inasisitiza kuwa bibilia
inatukumbusha kuwa tunatakiwa kuishi kwa kupendana pamoja kama waraka wa Warumi
12: 15- 18 Furahini pamoja nao wafurahio;
lieni pamoja nao waliao. Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie
yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa
kujivunia akili. Msimlipe
mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu
wote. Tukumbuke kuwa pale penye
amani na upendo furaha ya bwana utawala na watu wanakua katika neema ya Mungu
na maarafa ya mungu; umoja wa kweli huzaliwa miongoni mwetu. Lakini pale ambapo
pana chuki amani hutoweka neema ya Mungu na maarifa yake hutoweka pia; woga
hutawala, uwazi hupotea shetani natawala na kuleta maangamizo ambayo mwisho
wake humwangamiza mwanadamu na kumfanya kujenga kiburi na majivuno.
Tafakari ya leo neno la msingi katika kuishi
kwa upendo na wezetu linatawalia na neno heshima; tukiweza kuwaheshimu wezetu
na kuwapa haki wanayostahili upendo utatawala maisha yetu, na hakuna kiburi
wala chuki kitapata nafasi katika maisha yetu; mwenyezi Mungu anatamani sana
sisi tuwe tofauti katika dhana nzima ya kuishi pamoja kwa kupendana; Mungu
anataka sisi tuwe chanzo cha Baraka kwa wenzetu; tuwe watu ambao hatutamani
wenzetu wapate shida au tabu; na pale wanapofanikiwa tusiwe watu wa kwanza
kuwaonea wivu na kuwachukia. Bali tushangilie pamoja katika mafanikio yao na
tulie pamoja na kuwapa nguvu katika shida zao.
Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa ili tuweze
kufanikiwa lazima tukubali na kujikataa wenyewe; tusiwe watu ambao tunajijali
wenyewe na kuona vitu bora vyote ni vyako na wengine hawastahili; bali
tunahitaji kuwa wenyenyekevu na kuweka matakwa ya wengine mbele zaidi katika
kuleta maisha ya upendo wa kweli miongoni mwenu na kufanikisha amri ya upendo
wa kuishi pamoja. Ni jambo gumu ambalo linasumbua katika utekelezaji wake. Maisha
yetu yamejaa choyo, umimi, wivu na unafiki; ni neema tu itakayo tusaidia
kutekeleza dhana ya kuishi kwa pamoja kama ndugu kama tutaweza kusoma na
kuelewa nyakati za Mungu na maarifa yake, katika kutekeleza upendo wa kweli .
Hii ndio tafakari yetu ya leo; Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment