May 21
Ayubu 1:21
Tafakari ya leo tunangalia umuhimu wa kufanya agano na Mungu. Agano ni kitendo cha kukiri kuwa tayari kutimiza ahadi ambayo umeweka. Bibilia inatukumbusha kuwa agano la Ayubu na Mungu lilikuwa la kutomsaliti pamoja na mateso na shida zote ambazo alipata. Ayubu alisimama imara na kuitetea imani yake.
Tafakari yetu inatufundisha hata pale mke wake Ayubu alipo mbembeleza Ayubu kumwasi bwana alikataa kufuata ushauri huu akijua kuwa Bwana aliyetoa ndiye mwenye mamlaka ya kutwaa.
Tujiulize leo mimi na wewe tumemwekea Mungu agano gani? Je wakati wa majibu bado tunaweza tunza agano hilo? Ni wakati mzuri wa kujitafakari. Kama ni mama au baba wa familia agano la ndoa mnalitekeleza kulingana na kiapo na mafundisho ya bibilia? Je watoto wanatunzaje agano Lao la utii na kuwaheshimu wazazi wao?
Tafakari ya leo inanyesha kuwa hili ni somo muhimu sana katika maisha yetu ya kiroho jambo tunajua kutimiza agano ni jambo gumu. Tupo kwenye dunia ambayo imejaa majaribu ambayo hutufanya tusahau kutimiza maagano yetu na Mungu. Habari njema hatujechelewa kabisa wakati wa utekelezaji wa agano au maagano ni sasa. Tumwombe Mwenyezi Mungu atufunulie hekima za kuona na kutekeleza maagano yetu naye Amina.
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment