May 15
Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa mafanikio yetu ambayo tunayo hayatakuwa salama kama hayatapata kibali na ulinzi wa Mungu. Leo hii wengi tunaona mafanikio yetu hayahitaji mkono wa mungu.
Lakini tumejisahau kuwa bila neema ya ulinzi wake mafanikio yetu hupotea. Tunahitaji ulinzi wake katika mafanikio yetu yote. Iwe ni swala la afya njema, Mali tulizopata, familia zetu. Vyeo ambavyo tunavyo na kadhalika.
Mungu ni upendo na upendo wa Mungu daima unatuzunguka katika ulinzi wa maisha yetu na mafanikio yetu. Hivyo ni wajibu wetu kuendelea kuomba ulinzi wa Mungu katika Mali na mafanikio yetu.
Tafakari yetu unaendelea kusisitiza kuwa bila mkono wa mungu tujihesabu kuwa hatuna mafanikio. Tutakuwa miongoni mwa wale wote waliofanikiwa lakini wakaona kuwa Mungu sio chochote, wakadharau na wakaishia katika maandalizi na anguko la miradi yao.
Ni jukumu letu kulinda mafanikio katika njia sahihi zinazompendeza Mungu. Ili baraka yake idumu, na ulinzi wake uwe wa endelevu. Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment