June 30
Tafakari yetu leo
tunaangalia matumizi ya uhuru ambao mwenyezi Mungu ametujalia sisi wana wa
Adamu; (free will) tukijikita zaidi katika uhuru wa wakovu katika maamuzi yetu
na utumishi wetu mbele ya Mungu; kwa maneno mengine ni uwezo wetu huru wa
kufanya maamuzi ya vipawa mbele ambavyo sisi tunataka view; na uchaguzi wetu
sisi binadamu misingi yake iko kwenye, furaha, mapenzi, upendo na matamanio
yetu kulingana na vionyo vyetu. Tunachagua kila ambacho tunaona sisi
kinatupendeza zaidi na kutupa raha zaidi kwa wakati huo husika. Kuna wale
wanaojiuliza kama Mungu anajua mawazo na nini tunataka kufanya kwa nini sasa
ametupa sisi huo uhuru wa kufanya tutakavyo; Anajua nini kitatokea mbele yetu
katika dakika au sekunde inayokuja; sasa kwa nini ametupa huu uhuru wa kuamua?
Tafakari yetu inatukumbusha
kuwa tukisoma Bibilia Mungu haoni furaha kumwona mwenye dhambi akifa katika
dhambi na kuishia kupata adhabu ya milele; Tukisoma Ezekieli 33:11 Waambie, Kama
mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali
aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini,
mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa, Enyi nyumba ya Israeli? Kinyume chake tunakiona tukisoma
kitabu cha ufunuo 4:11 Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu,
kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu
vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa. Kwa
nini sasa Mungu ametupa sisi uhuru wa kuamua ili tuweze kufurahia uumbaji wake,
tuwe na furaha kamili, furaha ambayo nasi ni sehemu ya kuiamua na kuiishi.
Upendo ambao hauna uhuru sio upendo wa kweli; Upendo wa kweli ukupa wewe nafasi
ya kufanya maamuzi. Tatizo letu ni busara ya maamuzi yetu.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa hata tukiangalia kazi ya uumbaji ambao Mungu aliufanya katika siku sita kabal ya kupumzika siku ya saba alivitazama vyote alivyofanya pamoja na uhuru aliompa binadamu wa kufanya maamuzi kuwa vyote vilikuwa ni vitu vyema. Sisi wenyewe tunatakiwa tuutumia vizuri uhuru huu kwa kuishi maisha yale yanayompendeza Mungu na kuachana na dhambi zetu. Kuishi katika dhambi sio lengo la Mungu kwetu, bali anataka sisi wenyewe tupime na kufanya maamuzi sahihi ambayo yatampendeza Mungu na sisi wenyewe. Dhambi ni zao uhuru wa maamuzi wa binadamu, zawadi ya Mungu kwetu ya kuishi maisha bila dhambi daima tumekuwa tukiidharau, matokeo yake kwetu dhambi ndio imekuwa zao letu tulipendalo na zao ndani ya Mioyo yetu, ndio maana hata maamuzi yetu yametawaliwa na dhambi. Matokeo ya uchaguzi wetu ni kilio na kusaga meno kwani Mungu hauvumilia matumizi mabaya ya maamuzi yetu.

Tafakari yetu leo tukumbuke
kuwa Mungu anajua kila kitu kwani ni yeye ndiye aliumba vitu vyote. Na tazama
vyote vilikuwa vikipendeza kama waraka wa waefeso 1:11 unavyosema na ndani yake
sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi
lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake. Hivyo anajua
mawazo yetu na nini tunatka kufanya kwani ni yeye ambaye alitupa sisi uhuru wa
kuamua nini tufanye; anaona jinsi ambavyo tunafanya maamuzi yetu tukiangukia
kwenye dhambi na kwa upendo wake alituletea Mkombozi wetu yesu Kristo aje
kuishi nasi na kutufundisha jinsi ya kufanya maamuzi sahihi ambayo yanampendeza
Mungu. Na isitoshe alikubali kupita katika njia ya Mateso na kufa msalabani ili
tu tusamehewe dhambi zetu ambazo zilitokana na maamuzi mabaya. Ni wajibu wetu
sasa kubadilika na kuanza sasa kufanya maamuzi ambayo yanampendeza Mungu kwa kuacha
kufanya maamuzi katika njia ya dhambi.
Hii ndio tafakari yetu ya leo –Amina_
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment