June 21
Matthew 11:2-3
Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa kama nina
amini na kwa nina wasiwasi? Tukiangalia katika mazingira tofauti tofauti
simulizi katika vitabu vya Ayubu,
Mhubiri, maombolezo, zaburi na Habakuki vyote katia mazingira tofatuti
vimegusia dhana ya mashaka kwa hisia kuwa Mungu alikuwa amewaacha katika shida
zao; Katika mazingira ya maisha ya kuwa Mfuasi wa Kristo ni wazi kuwa dhana ya
kuwa na mashaka ni jambo la kawaida; tukumbuke kuwa hata imani ili iweze
kuimarika yatupasa kuwa mashaka ili kukomaza imani hiyo; kama wataalamu wengi
walivyopata ongea kuwa kama utakuwa na wasiwasi basi utakuwa umefika katika
mahali ambapo pa mwisho kabisa katika imani na mahali hapo ni mbinguni.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa mashaka
/wasiwasi tunaweza vielezea katika makundi makuu matatu; kuna wasiwasi ambayo
inaletwa na wasomi ambao wao mashaka yao wanayaelekeza nje ya imani yetu,
wakiuliza Mungu kweli yuko? Je bibilia ni neno la Mungu? Kweli yesu ni mwana wa
Mungu? Ni kweli kuwa Yesu alifufuka? Kundi la pili la wenye mashaka ni wale
ambao ni washiriki katika makanisa yetu; ambao wanajiuliza kama kweli wao ni
wakristo kweli? Je kweli wananamini? Kwa nini bado najisikia mdhambi? Kwa nini
inachukua muda mrefu kwangu kufanikiwa kupona, au shida yangu kutatuliwa. Na kundi
la tatu wale ambao mashaka yao yanalengwa na swali kwa nini? Kwa nini mototo wangu
alikufa? Kwa nini ndoa yangu imevunyika? Kwa nini sipati Mume? Kwa nini
marafiki zangu wananisaliti; Mungu alikuwa wapi wakati Mjomba wangu
aliponibaka? Haya ni maswali machache kati ya mengi; tunachokiona hapa ni
mwingiliana wa imani na maumivu ambayo yanapatikana katika maisha na kuleta
mashaka na tatizo ni pale sasa majibu hayapatikani hata wale wahusika ambao
wako ndani ya kanisa ambao walitakiwa kusaidia kuondoa mashaka haya nao wanamua
kudharau na kuto kutoa msada wa ufafanuzi mzuri ambao unamjenga mtu kiimani
zaidi na kuweza kuondoa mashaka ya namna hii. Kwa kushindwa kuyapatia ufumbuzi
maswali kama haya ndio mashaka ya kiimani au mashaka ya kiroho huanza kujitokeza
na watu wananza kukimbia kanisa.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa watu wengi
wanafikiri kuwa kuwa na mashaka ni kukosa imani; lakini kwa ujumla wake sio
kweli isipokuwa kama wewe huamini hivyo huna imani; kwa asiye amini ni tendo la
makusudi na lililo kusudiwa; lakini kuwa na mashaka ni kuwa na mashaka ya ndani ya nafsi yako;
mshaka yanasemehewa na mungu hatuazibu sisi tunapo jiuliza maswali mengi kuhusu
yeye; tuwakumbuke Ayubu na Daudi mara kadhaa walikuwa wanajiuliza maswali mengi
kuhusu Mungu lakini hata hawakuwalaani; Uwezo wa mungu ni wa ajabu kutatua
mashaka yetu na maswali yote yenye mashaka juu yake; watu wengi wanafikiri
jinsi tunavyo jiuliza maswali mengi kuhusu Mungu kwamba hatuna imani la hasha
tukumbuke kuwa bila kuwa na mashaka imani yetu haitakuwa inavyotakiwa.
Tafakari yetu inaendelea kufafanua kuhusu mashaka
kwa kuangalia mfano kutoka Mathayo 11:2-3 Naye Yohana aliposikia huko gerezani matendo
yake Kristo, alituma wanafunzi wake, kumwuliza, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine? Hili ni swali lenye nguvu sana; cha
kujiuliza hapa masha ya Yohana Mbatizaji yanatokea wapi; kumbuku kuwa yeye
wenyewe huko nyuma alishakiri kumjua Kristo kama masiha; ukisoma Yohana 1: Yohana
akawajibu akisema, Mimi nabatiza kwa maji. Katikati yenu amesimama yeye
msiyemjua ninyi. Ndiye yule ajaye nyuma yangu, ambaye mimi sistahili kuilegeza
gidamu ya kiatu chake. Siku ya
pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu,
aichukuaye dhambi ya ulimwengu! Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma
yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. Wala mimi sikumjua; lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli
ndiyo maana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji.... Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa
Mungu.
Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa
Mungu! Kwa maelezo haya toka
injili ya Yohana: Yohana Mbatizaji alikuwa anamjua Yesu kuwa ni nani; lakini
swali la kujiuliza ni hili kwa nini mtu ambaye alimfahamu sana Yesu aliishika
kuwa na Mashaka na mafundisho yake? Lakini tukumbuke kuwa watu wenye mashaka
ndio wanaokuwa watu wenye imani kubwa sana.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Mungu yuko tayari kutatua mashaka yote; kuondoa woga; na
kukujibu maswali yote ambayo unafikiria kuwa hayana majibu; anatawala mbingu na
dunia bila msaada; tujue kuwa mashaka yetu kamwe hayamletei hasiara yeyote;
yeye ni Mungu wetu sote katika khali yeyote ile; tunachopaswa kufanya ni kuishi
na kutekeleza majukumu yetu kwa Imani tumkumbuke Noha alipokuwa akijenga safina
alitenda kwa Imani; Abrahamu alipo acha ur na kwenda Chaldees alifanya kwa
imani bila mashaka; Abrahamu alipotakiwa kumtolea sadaka Isaki alifanya kwa
Imani bila mashaka; tunakumbuka Kisa cha Musa na alipotembea na wana wa Israeli katika ya
Bahari ya shamu kwa imani na sio mashaka; mwangalie samweli alipotupwa katikati
ya samba alikuwa na imani zaidi na sio mashaka. Hivyo pamoja na mashaka yetu
bali tunatakiwa kutanguliza imani zaidi na kutenda kwa imani na sio mashaka;
Hii ndio tafakari yetu ya leo – Amina-
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment