June 14
Mathayo 7:11
Tafakari yetu leo tuangalie neema ya kubarikiwa. Mungu
alimwambia Abrahamu kuwa nami nitakufanya
wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; Mweneyezi
Mungu anatupa sisi Baraka ili nasi tuweze kuwabariki wengine; Kubarikiwa kwa
namna yeyote ile sio maana yake tu kujisikia vizuri, kuwa na furaha na utulivu
bali tunatakiwa nasi tuwabariki wengine pia; msingi huu wa Baraka tunayopata
ambayo hutusaidia sisi kuwa na amani na furaha tunatakiwa tuwahamishie na
wengine pia; Baraka lazima zitirike kwenda kwa wengine ambao nao wanahitaji
kubarikiwa.
Tafakari yetu leo inatukumbusha injili ya Luka
18:29-30 Akawaambia, Hakika nawaambia, hakuna mtu aliyeacha nyumba, au mke, au
ndugu, au wazazi, au wana, kwa ajili ya ufalme wa Mungu, asiyepokea zaidi mara nyingi katika zamani hizi, na katika
ulimwengu ujao uzima wa milele. Tukumbuke
kuwa tunapopata nafasi ya kuwabariki wengine nasi pia tunabarikiwa na Mungu
kamwe hataacha kutubariki. Kwa mtu ambaye yuko tayari kuwa saidia wengine kamwe
Mungu hata funga milango yake ya Baraka juu yake. Na Baraka za mungu zinakuja
kama mvua na neema yake kama juu;
Tafakari yetu inatukumbsha kuwa tuna kila sababu za kufurahi kwani tunapowakumbuka
wengine katika shida zao kwa wema ule ule ambao Mungu ametujalia sisi: Mungu
naye anachukua maujumu ya matatizo yetu nah ii baraka ya pekee nay a ajabu.
Tunajua kuwa Mungu ni hodari katika kushugulikia shida zetu kwa wakati wake ambao
ndio mwafaka kwetu. Tukumbuke kuwsa Baraka ambazo tutazitoa kwa wengine zitaturudia
sisi wenyewe zaidi ya vile tunavyowabariki wengine. Kadiri ambavyo sisi
tunawasaidia watu wengine ndivyo hivyo hivyo Mungu atakavyo tubariki sisi.
Tukisoma Luka 6:38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na
kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa
vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa. Hivyo ni wajibu wetu kuwabariki wengine ili tuweze
nasi kubarikiwa kwa namna yeyote ile ambayo ni njema na inayokubalika mikononi
mwa Mungu.
Tafakari yetu leo inatuonyesha kuwa Lengo la kwanza la Mungu ni
kutubariki; nasio kutulaani; au kutuangamiza; na tufahamu kuwa Mungu pekee
ndiye mwenye nguvu ya Kubariki na kuongoza Dunia yote; Mungu anaweza
fanya kitu chochote katika ulimwengu huu; ana nguvu na uwezo wa kubariki au
kuangamiza kama Wafilipi 3:20 inavyosema Kwa
maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi,
Bwana Yesu Kristo; Mungu ni mwema
na ahadi zake ni za ajabu sana; kama tunavyosoma Mathayo 7:11 Basi
ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi
sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?
Tukumbuke kuwa Mungu ni rafiki sio adui na kamwe hawezi kuzuia
Baraka yeye hutoa Baraka na sisi tunatakiwa kuzipokea na kuwasaidia wengine;
Hii ndio tafakari yetu ya leo tunahimizwa kufanya mema zaidi na sio maovu. Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment