June 22
Mwanzo 3:8
Yeramiha 23:24
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa mara nyingi kuwa
tunafikiri tunaweza kujificha mbele ya uso wa bwana lakini ukweli ni kuwa mwanadamu hawezi kujificha mbele ya uso wa
Mungu bali tunaweza kufichwa ndani ya
Utukufu wa Mungu. Bahati mbaya mawazo yetu yanatudanganya na kujiona kuwa
tunaweza kujificha na kufanya chochote tutakacho bila kuonekana mbele ya Macho
ya Mungu. Pengine hilo linawezekana kujificha mbele ya macho ya binadamu.
Tumekuwa na tabia za kuacha njia zipasazo kufuatwa na kwenda kinyume na utaratibu tuliokubali
kuufuata tukiamini kuwa hakuna anayeweza kuona au kugundua. Lakini tukumbuke
kuwa hakuna kwa namna yeyote ile
tunaweza kujificha mbele ya uso wake; tuwe kwenye ngiza; ndani ya chumba;
tumejificha kwenye kichaka kwa ujumla hakuna jambo litakalo tendeka ambalo
Mwenyezi Mungu asiweze ona. Chochote unachoangalia; kusoma; uanchoamua
kuangalia; unachofikiria; mahali popote mabapo unakwenda Mungu anajua kwa nini
uko mahali hapo na kwa sababu gani kamwe huwezi jificha mbele ya uso wake;
Tafakari yetu
inatukumbusha jinsi Yeramiha 23:24 Je, mtu ye yote aweza kujificha mahali pa siri,
nisimwone? Asema Bwana. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema Bwana. Yeramiha 49:10 Lakini
nimemwacha Esau hana kitu, nimepafunua mahali pake pa siri, wala hataweza
kujificha; kizazi chake kimeangamizwa, na ndugu zake, na jirani zake, naye
mwenyewe hayuko. Ezekieli 28:3 Tazama,
una hekima kuliko Danieli; hapana neno la siri watu wawezalo kukuficha; ufunuo 6:15-17 Na wafalme wa
dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na
mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya ilima, wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele
za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni
nani awezaye kusimama?
Tafakari yetu leo hebu tujikumbushe nini
kiliwatokea Adamu na Hawa tukisoma Mwanzo 3:8-10 Kisha wakasikia sauti ya Bwana
Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha
kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone. Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa
mimi ni uchi; nikajificha. Adamu
na Hawa baada ya kutenda dhambi waliamua kujificha wakitambua kuwa Mungu
hataweza waona na hivyo kuwa mbali kabisa na uso wa bwana; kumbe haikuwa hivyo
ndivyo yalivyo maisha yetu; akili zetu zinajaa ukungu na kufikiri kuwa tunaweza
kufanya dhambi yoyote na Haitaonekana mbele ya Mungu; Sababu kubwa ya kujificha
ni kwa sababu tunakuwa tumefanya dhambi mbele ya Mungu;
Tafakari yetu bado inatukumbusha kuwa dhambi na tendo la
kujificha hatuwezi kuvitenganisha na hilo ndilo anguko la mwanadamu; lakini
pamoja nahii tabia ambayo inasababisha anguko la mwanadamu Mungu daima bado
anataka kuturudisha katika njia iliyo bora kabisa; njia ya ukamilifu mkubwa
tukisoma Luka 19: 1-5 anasema hivi, Naye alipoingia Yeriko alipita katikati yake. Na tazama, palikuwa na mtu,
jina lake Zakayo, mkubwa mmoja katika watoza ushuru, naye ni tajiri. Huyu alikuwa akitafuta kumwona
Yesu ni mtu wa namna gani, asiweze kwa sababu ya umati wa watu, maana ni mfupi
wa kimo. Akatangulia mbio,
akapanda juu ya mkuyu apate kumwona, kwa kuwa atakuja kuipitia njia ile. Na Yesu, alipofika mahali pale,
alitazama juu, akamwambia, Zakayo, shuka upesi, kwa kuwa leo imenipasa kushinda
nyumbani mwako Naye alipoingia Yeriko alipita katikati yake. Na tazama, palikuwa na mtu, jina lake Zakayo, mkubwa mmoja
katika watozaushuru, naye ni tajiri. Huyu alikuwa akitafuta kumwona Yesu ni mtu wa namna gani,
asiweze kwa sababu ya umati wa watu, maana ni mfupi wa kimo. Akatangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu apate kumwona, kwa
kuwa atakuja kuipitia njia ile. Na Yesu, alipofika mahali pale, alitazama juu, akamwambia,
Zakayo, shuka upesi, kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani mwako.
Mungu yuko tayari kutushirikisha sisi katika ufalme wake, kama tutaacha tabia
ya kujificha pamoja na dhambi zetu, tukiwa kama Zakayo tutapata wokovu wa
kweli;
Tafakari yetu inatuonyesha kuwa Zakayo
alijitambua kwa alikuwa Ni Mtu mwenye dhambi na ambaye alikuwa akichukiwa na
watu kutokana na kazi yake. Hivyo baada ya kujificha yeye aliamua kumtafuta
Yesu amwone ni mtu wa aina gani. Alijua kuwa
kwa habari juu ya Yesu alijua kuwa atakuwa amekutana na mtu mbaye ataweza
msamehe dhambi zake na yeye kuanza kuishi maisha mapya ya wokovu. Hatutakiwi
kujificha tunapokosea bali tumkimbilie mwokozi wetu Yesu kristo ili aweze
kutusamehe na kutuondolea aibu ambayo inatupelekea sisi kujificha.
Tukumbuke kuwa hakuna yeyote ambaye anaweza
kujificha kukimbia uwembo wa Mungu na uwepo wa Bwana wetu Yesu Kristo juu ya
Matendo yetu; Tunatakiwa kubadilika kwa tuweze sasa kuwa wakamilifu kwa kuacha
dhambi na kuishi maisha mema yanayompendeza mungu.
Hii ndio tafakari yetu ya leo – Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment