June 16
Isaya 6:8
Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa katika maisha yetu sasa je tu
sisi tuko tayari kama Isaya alivyo mwambia Mungu Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume
nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, Mimi hapa, nitume mimi. Mungu alikuwa
anatafuta mtu ambaye atakuwa mwakilishi wake, karani wake ambaye atakuwa
ataweza kutawanya ujumbe wake kwa mataifa. Ujumbe wa amani , ujumbe wa
matumaini, ujumbe wa upendo; bila wasiwasi na kusita Isaya alimwambia Mungu
Mimi hapa nitume; isaya kwa kukubali aliweza kuona nguvu ya ajabu ya
mungu na utataktifu wa Mungu; aliweza kuzisafisha kabisa dhambi zake
na kumfanya aweze kwenda kokote na kuhubiri neno la Mungu. Kumbuka lile kaa la
moto ambalo liligusa midomo ya Isaya, midomo ya Isaya ilikuwa yenye dhambi
hivyo kwa kaa la moto la kimungu lilisafisha dhambi zilizokuwa katika midomo
yake ili aweze sasa kutangaza ukweli wa Mungu.
Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa Mungu bado anataka mimi na
wewe leo tuwe miongoni mwa wale ambao amewaita na kama ilivyokuwa kwa isaya
basi tusisite au kuwa na mashaka ya kukubali wito huo; tunatakiwa leo hii
kuweka imani yetu kwa Yesu tukishukuru kuwa kwa damu yake sisi tumesafisha na
kuondolewa dhambi zetu; Lazima tuendelee kutafakari kuwa tunatakiwa kumrudia Mungu,
na kufuata sheria zake na sio kuendelea kuishi kwa namna na jinsi ambavyo
tunaona sisi inatupendeza kwa kuendelea kufanya hivyo tutatengwa na Baraka na
upendo wa Mungu; Gharama ya kufanya mambo kwa namna ambayo sisi tunataka ni
kubwa sana. Tunamwitaji Mungu na Mungu anatuhitaji sisi ili tuweze kutangaza
neno lake na kufikisha ujumbe wa upendo kwa mataifa. Tukumbuke bila
nguvu ya Mungu maisha yetu yatendelea kujaa ushetani wa ajabu na wa kutisha.
Tafakari yetu ya leo inatukumbusha kuwa kwa kupitia Malaki 3:6 Kwa kuwa mimi, Bwana, sina kigeugeu; ndio maana
ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo. Mungu yuko vile vile kama Isaya alivyomwona. Bahati mbaya wengi wetu
hatujewahi kupata maono kama alivyoshuhudia Isaya. Hatujemwona Mungu lakini kama tutakubali wito wake wa
kutangaza neno lake tutamwona Mungu katika karamu ya mwisho. Mungu anakuita leo
kwani anajua kuwa kuna watu wengi ambao wanatamani kusikia neno lake liletalo
faraja lakini wewe na mimi bado hatujeitikia wito wa Mungu na kusema MIMI HAPA;
NITUME MIMI: NITUME BWANA.
Tafakari yetu tuhitimishe kwa maneno haya Isaya 6:4-8 Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea;
kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye
midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, Bwana wa majeshi. Kisha mmoja wa maserafi wale akaruka akanikaribia; naye
alikuwa na kaa la moto mkononi mwake, ambalo alikuwa amelitwaa kwa makoleo toka
juu ya madhabahu; akanigusa kinywa changu kwa kaa hilo,
akaniambia, Tazama, hili limekugusa midomo yako, na uovu wako umeondolewa, na
dhambi yako imefunikwa. Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema,
Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, Mimi
hapa, nitume mimi.
Hii ndiyo Tafakari yetu ya Leo Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment