June 29
2 Wakoritho 2:11
Tafakari ya leo tuangalia
jinsi shetani anavyotumia silaha ambazo tunazo kutuangusha sisi wenyewe;
shetani anapinu nyingi sana za kutuangamiza kabisa kama hatuko makini; tukisoma
2 Wakoritho 2:11 Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi
kuzijua fikira zake. Huu ni wajibu wetu kuzuia mbinu zote za shetani
kwani tunamjua vizuri, na mikakati yake yote; silaha moja nzito sana ya shetani
ni kuwa na majivuno silaha hiyo ni hatari sana katika maisha yetu kama wafuasi
wa kristo; mara nyingi sisi kama binadamu hatuoni tofauti yeyote pale mambo
yanapokwenda vizuri tukifurahia utajiri na amani mfano mzuri tukimwangalia
Lucifer mkuu wa malaika ambaye alikuwa akiishi vizuri chini ya utawala Mungu;
hatimaye tama na majidai yalimjia kupingana na Mungu. Timoteo 3:6 Wala asiwe
mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi.
Tukisoma Ezekieli 28: 14-17 Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami
nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko
kati ya mawe ya moto. Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa,
hata uovu ulipoonekana ndani yako. Kwa
wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda
dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho
najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya
moto. Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu
hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya
wafalme, wapate kukutazama.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa hatuna sababu ya kuwa na
majivuno kama 1 Wakoritho: 13:8 inavyosema Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo
hautakabari; haujivuni; tunatakiwa kujiepusha na huluka ya majivuno
yatokanayo na kufanya mambo mazuri kama Yesu alivyokuwa akiwafundisha wafuasi
wake katika Luka 18:9-14 Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni
wenye haki, wakiwadharau wengine wote. Watu wawili walipanda kwenda hekaluni
kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru. Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake;
Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang'anyi,
wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi nafunga mara mbili kwa
juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote. Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala
hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema,
Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi. Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake
amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye
ajidhiliye atakwezwa. Hatutakiwa kujihesabia haki wenyewe hata kama
tunafanya mema Mungu peke yake ndiye ajuae matendo yetu na anakipimo sahihi cha
kutupima na kutupa thawabu tunayostahili.
Tafakari yetu
inatusisitiza kuwa lazima tuendelee kuchukua taadhari dhidi ya adui wa roho zetu. Tukisoma 1 Petro
5:8 Mwe na kiasi na
kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka,
akitafuta mtu ammeze. Ni ukweli
ambao haupingiki kuwa unapopigana vita na unataarifa za kutosha juu ya adui
yako, hukusaidia na kupunguza ugumu wa vita yako na uwezekano mkubwa sana wa
ushindi; tukumbuke kuwa Mungu alikuwako tangu kuumbwa kwa dunia lakini shetani shetani
hakuwako toka mwanzo wa dunia; Mungu kamwe haumbi kitu chochote kibaya; Mungu
huumba vitu vyote katikaukamilifu mkuu; Adamu na Hawa waliumbwa katika
ukamilifu na ubora uleule kama yeye alivyo; hata shetani alipoumbwa alikuwa
katika ubora wa ukamilifu na alikuwa haitwi shetani; na alikuwa akijulikana
kama Nyota ya asubuhi tukisoma
Tafakari yetu inatukumbusha anguko la Lusuferi ( Nyota ya
Asubuhi) tukisoma kitabu cha Isaya 14:11-12 Fahari yako
imeshushwa hata kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza wametandazwa chini
yako, Na vidudu vinakufunika. Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri,
mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa. Kabla
ya kuwa Shetani alikuwa mkuu wa malaika wote, alikuwa akiwaongoza malaika
katika masifu mbele ya Mungu; alijaliwa nguvu nyingi na uwezo mkubwa kutoka kwa
Mungu; Lakini alianguka katika dhambi alipotaka kufanana na Mungu na kugeuka
kuwa shetani. Hivyo huyu adui bado ni mbaya katika maisha yetu ya kiroho kwa
sababu ananguvu nyingi bado na Mungu hakuziondoa nguvu hizo. Kwa nini lakini
Mungu hakuzichukua hizo nguvu za shetani ambazo zinatutesa leo; kwa sababu
Mungu hachukui zawadi ambazo anakupa wewe hata pale unaposhindwa kutimiza yale
ambayo yeye anataka wewe utimize mbele yako. Je wewe ukimpa mtu zawadi pale
mnapotofautiana unaichukua ile zawadi tena; kwa ujumla jibu ni hapana;
Tafakari yetu
inatukumbusha kuwa tujiepushe na majivuno, mwonekano wetu, nafasi ambazo tunazo
kimaisha,akili zetu, uwezo wetu kifedha kwani hivyo ni baadhi tu vitu ambavyo
shetani anavitumia katika vita vya kutuangusha ili tusiweze kumtumikia Mungu
vile itupasavyo sisi kuishi; tunatakiwa tutumie uwezo wa kiakili tuliojaliwa
katika kumtumikia Mungu na sio shetani; tunatakiwa kuwa makini na kuendelea
kuzitambua silaha ambazo shetani anazitumia juu yetu katika kutuangamiza; Amka
leo na uwe mshindi wa maisha ya kiroho na maisha ya baadae.
Hii ndio tafakari yetu
ya leo – Amina-
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment